UTAWALA WA ROMA YA KIDINI

 UTAWALA WA ROMA YA KIDINI:

      

              (Roman Catholic)



1. Ulipokea kiti chake cha Enzi kutoka kwa Joka(shetani)


👉🏻Ufunuo 13:2  👉🏻 Na yule mnyajma niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule Joka (shetani) akampa nguvu zake na kiti chake cha Enzi na uwezo mwingi.



Hakuna ufalme wa kidini hapa duniani unaosujudiwa na ulio na mvuto kwa Wanadamu wengi na serikali zote za dunia hii kama roma ya kidini ambayo makao yake makuu ni #Vatican, hapa ndipo makao makuu ya ufalme huu wa kidini ambao unaiita dunia yote kuwa kitu kimoja bila kubaguana ukiongozwa na askofu wa roma (Papa).



2. Ufalme huu wa kidini uliitawala dunia kwa miaka 1260 huko nyuma. Na sasa unajiimarisha kuitawala dunia yote kwa mara nyingine lakini kwa mda mfupi tu na kisha MUNGU aliye Juu atauangusha na kuuangamiza milele.



3. Ufalme huu wa kidini uliwahi kupata jeraha la mauti mnamo mwaka 1798 wakati wa mapinduzi ya ufaransa. Jemedari Bethier wa ufaransa alimteka papa Pius mwaka 1798 na kumfunga huko ufaransa gerezani na Papa pius wa 16 aliyekuwa akitawala akafia jela. 



👉🏻Ufunuo 13:3


               Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona.Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.



👉🏻jeraha la mauti ni kuangushwa kwa utawala wa upapa mwaka 1798. Ufalme wa upapa uliitawala dunia toka mwaka 538AD hadi 1798.



Jeraha la mauti la upapa lilipona mwaka 1929. Serikali ya waitali iliurudisha mji mkuu wa Vatican ujisimamie kama serikali.



4. Ufalme huu una kofia mbili, kofia ya kidini na kofia ya serikali. Papa ni kiongozi wa serikali ya Vatican (Rais) lakini pia ni Askofu mkuu wa dini. Ufunuo 13:4



5. Ufalme huu ulishabadili AMRI za MUNGU . Danieli 7:25



6. Kiongozi mkuu wa utawala huu hujiita kuwa yeye ni MUNGU na anasamehe dhambi pia.


Ufunuo 13:1.


Ni kufuru mwanadamu kujiita MUNGU na pia kujichukulia uwezo wa kusamehe dhambi.



7. Ni kanisa mama wa makahaba na machukizo ya nchi. Ufunuo 17:5



8. Kanisa hili lilifanya vita na watakatifu na kuwashinda.  Ufunuo 13:7



9. Ni utawala/ufalme uliotawala dunia ukastaajabiwa na utatawala tena kwa mara nyingine, serikali zote duniani zitapata maelekezo kutoka kwake, na Wanadamu wataustaajabia. Ufunuo 13:3-4



10. Ufalme huu wa kidini una mtu anayeuongoza, na si mwingine ni PAPA wa Vatican .



Mda unakuja na tutashuhudia haya tuandikayo. MUNGU hajawahi kukosea hata siku moja.


MUNGU ni mpole wa moyo na kila wakati hunena yaliyo mema na kweli.



Wito wa MUNGU ni huu👉🏻👉🏻 Tokeni kwake enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata MBINGUNI na MUNGU amekumbuka maovu yake. Ufunuo 18:4-5



YESU anakuja, na kabla ya kuja kwake lazima utawala wa ufalme huu wa upapa ushike hatamu duniani na kuwaletea dhiki watu wa MUNGU wazishikao AMRI kumi za MUNGU na imani ya YESU . Na kwa mda mfupi huu utawala mwovu utaangushwa kwa kutokea kwa YESU mawinguni.


👉🏻 Habari zitokazo #Mashariki zitaufadhaisha utawala huu wa upapa/roma ya kidini.



BWANA awabariki mnapousambaza ujumbe huu wa malaika watatu wenye karipio kali.



Mungu akubariki 


Comments