MAPOKEO KATIKA SIKU YA SABATO:

MAPOKEO KATIKA SIKU YA SABATO:

Kati ya kundi lililokuwa na upinzani katika huduma za Yesu lilikuwa ni kundi la Waandishi na Mafarisayo, Mafarisayo walijitahidi kwa kila mbinu kutafuta makosa kwa Yesu ili wapate sababu ya kumshtaki lakini hawakupata.

Sasa hawa Mafarisayo ambao ni Wayahudi ndio walisema Yesu kavunja Sabato, kwa sababu ya kumponya mtu siku ya sabato na kumruhusu yule mtu kubeba godoro  siku ya sabato..
#Yohana 5:18  Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu.

Changamoto ya kwanza Wayahudi walikuwa wameifanya sabato kuwa mzigo kwa watu, yaani sabato baadala ya kuwa siku ya furaha ikageuka kuwa siku ya suluba, na mateso kwa sababu ya mapokeo yao waliyoyaingiza. Na hivyo Yesu ilibidi aanze kuondoa mapokeo yote yaliyokuwa yanaifanya sabato kuwa kongwa kwa watu. #Mathayo 15:13
Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang’olewa.

Wayahudi waliingiza mapokeo kwamba siku ya Sabato mtu hata kama Unaumwa kiasi gani haupaswi kuhudumiwa mpaka sabato iishe, jambo ambalo halikuwa agizo la Mungu, na ndio maana Yesu anawaambia siku ya sabato ni Bora kuokoa uhai wa mtu kuliko kuua. Ina maana kwamba uponyaji wa mtu wa Kimwili au wa Kiroho au wa mnyama hauna siku maalumu ni siku zote ni za kuponya pindi huduma hiyo inapohitajika: na ndio maana Yesu akawaambia hata Mungu anafanya kazi ya kuokoa Roho siku zote: #Yohana 5:17 Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi.

Ili kutia uzito zaidi Yesu akawatolea mfano wa Makuhani ambao walikuwa wakifanya kazi ya Upatanisho Hekaluni siku zote, hadi siku ya sabato, na hawakuwa wanahesabiwa kwamba wanavunja sabato kwa sababu walikuwa wanaokoa uhai wa kiroho wa watu.
Mathayo 12:5

Pili Wayahudi waliingiza mapokeo kwamba ikiwa ni siku ya sabato imekukutia ukiwa safarini, basi hauruhusiwi kula chochote ukiwa safarini mpaka sabato iishe, Na ndio maana Yesu ili kuondoa mapokeo yao anawarejesha kwa Daudi jinsi alipopatwa na njaa akiwa safarini na akala mikate ya Hekaluni ambayo haikuwa halali kwao kuila, lakini kwa sababu ya dharura walikula na haikuwa kosa. Mathayo 12:1-4.

Na hivyo basi wayahudi walimtuhumuYesu alivunja sabato kwa mujibu wa mapokeo yao, na sio kwa mujibu wa torati, maana katika torati hakuna aya inayokataza kwamba mtu hapaswi kuponywa siku ya sabato.

Mungu akubariki.

Kwa msaada wa kiroho piga
0627729770
0689980058

Comments