MUNGU ANAFANANA SANA NA SHERIA YAKE! SHERIA YAKE NDIYO TABIA YAKE!!
NA WANAOZISHIKA WANA TABIA YA MUNGU
1. I)MUNGU NI MTAKATIFU; II) NA AMRI ZAKE NI TAKATIFU; III) NA WANAOZISHIKA NI WATAKATIFU.
I)👉 Kwa kuwa mimi ni Bwana, Mungu wenu; takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu; ..."
(Walawi 11:44)
II)👉 "Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema. "
(Warumi 7:12)
III)👉 "Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu." (Ufunuo wa Yohana 14:12)
2. I) MUNGU NI WA MILELE; II) NA AMRI ZAKE
NI ZA MILELE; III) NA WANAOZISHIKA WATAISHI MILELE.
I) 👉 "....Kama alivyoamuru Mungu wa
milele..."(Warumi 16:26).
II) 👉"...hata milele na milele, ametoa
amri wala haitapita."" (Zaburi 148:6)
III) 👉 Mwalimu, nitende jambo gani jema, ili nipate uzima wa milele? ... Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri. "
(Mathayo 19:17)
3. I) MUNGU NI MWEMA; II) NA SHERIA NA AMRI ZAKE NI NJEMA; III) NA WANAOZISHIKA NI WATU WEMA.
I) 👉"...hakuna aliye mwema ila mmoja, naye ndiye Mungu." (Luka 18:19)
II- A) 👉"Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema." (Warumi 7:12)
II-B) 👉"Sheria ya kinywa chako ni njema kwangu...". (Zaburi 119:72)
III) 👉'"Basi mtu mmoja, Anania, mtauwa kwa kuifuata sheria, aliyeshuhudiwa wema na Wayahudi wote waliokaa huko,"
(Matendo ya Mitume 22:12)
4. I) MUNGU NI MKAMILIFU, II) SHERIA YA
BWANA NI KAMILIFU PIA, III) NA WANAOISHIKA NI WAKAMILIFU.
I) 👉"Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu". (Mathayo 5:45)
II) 👉"Sheria ya Bwana ni kamilifu, huiburudisha nafsi" (Zaburi 19:7)
III-A) 👉 "Heri walio kamili njia zao, Waendao katika sheria ya Bwana." (Zaburi 119:1)
III-B) 👉 " Na kwa habari za amri zake, sikuziacha...Nami nalikuwa mkamilifu kwake, Nikajilinda na uovu wangu."
(2 Samweli 22:24)
5. I)MUNGU NI WA KIROHO; II) NA SHERIA
ZA MUNGU NI ZA KIROHO; III) NA WANAOZISHIKA WANA ROHO MTAKATIFU.
I) 👉"Mungu ni Roho, wamwabuduo Yeye, imewapasa kumwabudu katika roho na mkweli" (Yohana 4:22)
II) 👉"Kwa maana twajua ya kuwa torati (sheria) asili yake ni ya Rohoni."
(Warumi 7:14).
III) 👉 "Mkinipenda, mtazishika amri zangu.
Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;
ndiye Roho wa kweli..." (Yohana 14:15-17)
6. I) MUNGU NI WA HAKI; II) NA SHERIA YAKE
NI YA HAKI; III) NA WANAOISHIKA WATAHESABIEA HAKI.
I) 👉"Yeye mwamba, kazi yake ni kamilifu, maana njia zake zote ni haki"
(Kumbukumbu 32:4)
II) 👉"Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema." (Warumi 7:12)
III- A)👉 "Kwa sababu sio wale waisikiao sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki." (Warumi 2:13)
III- B) 👉 "Nisikilizeni, ninyi mjuao haki, watu ambao mioyoni mwenu mna sheria yangu..."
(Isaya 51:7)
7. I) MUNGU NI WA UPENDO; II) NA SHERIA
ZAKE NI ZA UPENDO; III) NA WANAOZISHIKA WANA UPENDO.
I) 👉"...kwa maana Mungu ni
upendo"(1Yohana 4:8)
II) 👉"...Basi pendo ndilo utimilifu
wa sheria " (Warumi 13:10)
III) 👉 "Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake. (1Yohana 5:2)
8. I) MUNGU NI NURU; II) NA SHERIA YAKE NI
NURU; III) NA WANAOZISHIKA MACHO YAO YANA NURU.
I) 👉"...ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza lolote hamna ndani yake". (1Yohana 1:5)
II) 👉"Maana maagizo hayo ni taa, na sheria hiyo ni nuru..." (Mithali 6:23)
III) 👉 "... Amri ya Bwana ni safi, Huyatia macho nuru. (Zaburi 19:8)
9. I) MUNGU YUKO MBINGUNI; II) NA
SANDUKU LA AGANO LENYE AMRI
KUMI LIKO MBINGUNI; III) NA WANAOZISHI WATAENDA MBINGUNI.
IA) 👉"...basi uyasikie maombi yao na dua yao, huko mbinguni makao yako..."
(1Wafalme 8:49)
IB) 👉 "...Baba yetu uliye mbinguni.."
(Mathayo 6:9
II)👉"Kisha hekalu la Mungu lililoko Mbinguni likafunguliwa Sanduku la agano lake
likaonekana ndani ya Hekalu lake..."
(Ufunuo 11:19)
III) 👉 "Blessed are they that do his commandments, that they may have right to the tree of life, and may enter in through the gates into the city. (KJV Revelation 22:14)
👉III) "Heri wazitendao amri zake, wawe na haki kwenda kwenye mti wa uzima, na kuuingia mji kupitia malango yake.
( KJV - Ufunuo wa Yohana 22:14)
10. I) MUNGU ANATUKUZWA, II) NA SHERIA
YAKE AMEITUKUZA, III) NA WANAOZISHIKA AMRI ZAKE ANAWATUKUZA.
I) 👉 "Baba yetu uliye mbinguni jina
lako litukuzwe" (Mathayo 6:9)
II) 👉 "BWANA akapendezwa kwa ajili
ya haki yake, kuitukuza sheria na
kuiadhimisha" (Isaya 42:21). III) 👉 "Umemwungama Bwana leo, kuwa ndiye Mungu wako, na kuwa yakupasa kutembea katika njia zake, na kushika amri zake na kuwa atakutukuza juu ya mataifa yote aliyoyafanya, kwa sifa, na jina, na heshima.."
(Kumbukumbu la Torati 26:17,19)
11. I)MUNGU ANA HEKIMA; II) NA SHERIA NA AMRI ZAKE NI ZA HEKIMA ; III) NA WANAOZISHIKA WANA HEKIMA.
I) 👉 "Hekima na amri zina yeye [Mungu]; Yeye anayo mashauri na fahamu."
(Ayubu 12:13)
II) 👉"Zishikeni basi, mkazitende, maana hii ndiyo hekima yenu na akili zenu, machoni pa mataifa watakaozisikia amri hizi zote, nao watasema, Hakika taifa hili kubwa ni watu wenye hekima na akili."
(Kumbukumbu la Torati 4:6 )
III) 👉" Yeye aishikaye sheria ni mwana mwenye hekima; ..." (Mithali 28:7)
12. I) MUNGU NI MSAFI, II) NA SHERIA ZAKE NI SAFI, III) NA WANAOZISHIKA WAKO SAFI MBELE ZA MUNGU.- WAMESAFISHA TABIA.
I) 👉" Basi, kila mtu aliye na tumaini hili katika Kristo, hujiweka safi kama vile Kristo alivyo safi kabisa." ( BHN - 1 Yohane 3: 3 )
II) 👉 "... Amri ya Bwana ni safi, Huyatia macho nuru." (Zaburi 19:8)
III) 👉 "Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake. " (Ufunuo 22:14)
Mpenwa ifurahie sheria ya Mungu kama Paulo.
👉 " Kwa maana naifurahia SHERIA
ya Mungu kwa utu wa ndani"
(Warumi 7:22)
Kwa ushauri wa Kiroho piga namba
0627729770 Au 0712336509
Comments
Post a Comment