#UNABII WA #UFUNUO SURA YA 2 na 3:
Mungu ni mwema wana na binti za Mugu.
Karibu katika tafakari: Kwa neema ya Mungu naomba tujifunze mambo Machache katika kitabu cha ufunuo sura ya pili, na ya tatu:
Ufunuo sura ya pili na tatu inazungumzia Historia ya kanisa la Kristo tangu kipindi cha Mitume hadi Marejeo ya Yesu, katika Ufunuo sura ya kwanza Yohana anapewa ujumbe na Yesu kwamba aupeleke kwenye makanisa:
#Ufunuo wa Yohana 1:9-12
Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu.
Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,
ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.
Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami.
Yohana alikamatwa na Warumi na akapelekwa katika Kisiwa cha Patmo, ambacho kipo kwenye Bahari ya Aegean, hivyo wao wakadhani ndio mwisho wake, Lakini Mungu akamtumia hukohuko, kupokea Ujumbe kwa ajili ya Kanisa.
Hivyo Yohana alipewa ujumbe kwa ajili ya kanisa la Kristo jinsi litakavyo pitia katika shida, hadi Kurudi kwa Yesu.
Makanisa hayo yaliyoorodheshwa yanabeba tabia katika vipindi mbalimbali ambapo kanisa litapitia: haina maana alipewa ujumbe apeleke kweli kwenye kila kanisa. #Mfano ni katika Ufunuo 13, tunamuona mnyama mmoja lakini amebeba tabia za wanyama wane wa Daniel 7.
#KANISA LA #EFESO:
#Ufunuo wa Yohana 2:1-3
Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu.
Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo;
tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka.
Kanisa la Efeso linabeba tabia ya kanisa la Mungu kipindi cha Mitume, tangu mwaka wa 34-100 baada ya Yesu, Kanisa katika kipindi hiki lilikuwa na nguvu ya Roho Mtakatifu, na hata wale waliokuwa wanataka kujiingiza kwa siri ili kuliharibu kanisa hawakuweza, kanisa liliongezeka, upendo na mshikamano ulitawala.
#Matendo ya Mitume 2:46-47
Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe,
wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.
Baada ya mitume wengi kufa mbwa mwitu walianza kuingia kanisani kama Paulo alivyo tabiri.
#Matendo ya Mitume 20:29-30
Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi;
tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao.
Kanisa likaanza kupunguza upendo, imani ikaanza kupoa, umoja ukatoweka Nk. Na ndio maana onyo la Mungu ni hili:
#Ufunuo wa Yohana 2:4-5
Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza.
Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.
#KANISA LA #SMIRNA
Mwaka 100-313 Baada ya mbwa mwitu kuingia kanisani, kanisa likaanza kupata taabu, wapagani wakanza kuwauwa Wakristo, imani ikaanza kutafutwa kwa kumwaga Damu. Na wengine walifungwa gerezani kwa sababu ya kutetea imani.
#Ufunuo wa Yohana 2:8-10
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika; Haya ndiyo aneneyo yeye aliye wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai.
Naijua #dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani.
Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi #atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.
Kuna watu walijiingiza kanisani na kudai ni wayahudi kumbe walikuwa ni wapagani, na walipopingwa ikabidi waanze kuwauwa wakristo,
Lengo kubwa ilikuwa ni Kudhoofisha Ukristo,ili upagani ustawi maana wapagani waliona imani yao ya upagani inakosa nguvu kwa sababu watu wengi walijiunga na Kanisa la Kristo na Kadri walivyo wauwa ndivyo Ukristo ulivyozidi Kustawi.
#KANISA LA #PERGAMO:
Kipindi hiki cha historia ya Kanisa kilianza mwaka 313-538, Baada ya wapagani kuona suala la kuwauwa Wakristo ni sawa na kuzima moto kwa kutumia mafuta ya taa, yaani kadri walivyo wauwa ndivyo walivyozidi kuongezeka, mbaya zaidi Baadhi ya wapagani wenyewe wakawa wanajiunga na Ukristo, ndipo ikabi wabuni njia nyingine ya kuharibu Ukristo, Wakaona njia bora ni kuingiza mafundisho ya kipagani ili upagani ndio uabudiwe baadala ya Mungu ndani ya Kanisa.
#Ufunuo wa Yohana 2:12
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili.
Wapagani wakatangaza kwamba mauaji yasiendelee, na wakaomba msamaha kwa Wakristo, kisha wakadai kwamba na wao wanataka kujiunga na Ukristo. Baada ya wapagani hawa kupokelewa kanisani akiwepo Mfalme Costantino, Ndipo wapagani hawa wakaweka mikakati na kuanza kuingiza Upagani ndani ya kanisa kwa kivuli cha Ukristo:
Wakaenda kuchukua Masanamu ya miungu yao wakayaleta kanisani, lakini wakayabatiza majina ya watakatifu ili wakristo wasigundue, ndipo zikaingizwa sanamu za Yesu, Mariamu, Yusufu na za watakatifu wengine.
#Jumapili ambayo ilikuwa ni yakumuabudu mungu jua, wakasema hii ni siku ya kufufuka Yesu:
#Krismas ambayo ni sikukuu ya kuzaliwa mungu Tamuzi, wakasema itakuwa sikukuu ya kuzaliwa Yesu.
#Easter/ Pasaka sikuku ya mungu wa uzazi, wakasema ni sikukuu ya kufufuka kwa Yesu. Yaani hadi sasa Wakristo bado hawajui kwamba Yesu alisherekea Pasaka kabla ya kifo chake na alipomaliza kusherekea Pasaka usiku huo huo akakamatwa, Sasa inakuwa msherekee kufufuka kwa Yesu wakati Yesu mwenyewe alisherekea?
#Ubatizo wa kunyunyiza na watoto wachanga, NK.
#Ibada za wafu.
Na upagani mwingine mwingi ukaingizwa ndani ya kanisa.
Na ndio maana Mungu anasema Kipindi hiki kanisa lilikuwa limekaa kwenye kiti cha shetani, kwa maana upagani uliingia ndani ya kanisa. Na wale waliojaribu kupinga huu upagani, waliishia kuuwawa na wengine wakakimbilia maporini.
#Ufunuo wa Yohana 2:13
Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.
Sasa kulikuwa na wakristo waliopenda kusifiwa na wapagani, na hawa wakawa ndio wachochezi kwa wale waliokuwa wanapinga upagani, Biblia inawafananisha sawa na wakina balamu, na wakina Nikolai:
#Ufunuo wa Yohana 2:14-15
Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini.
Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile.
Hivyo hicho ni kipindi ambacho upagani uliingizwa ndani ya Kanisa, na baadhi ya viongozi wakawa wanawafundisha watu kuupokea upagani, kwamba hauna madhara yoyote.
Hata leo wapo wakina Balamu na Wakina Nikolai katika makanisa wanaowaaminisha watu upagani kwamba hakuna shida yoyote kukumbatia huo upagani, wa Jumapili, Krismaa, ibada za wafu NK.
#KANISA LA #THIATIRA:
Baada ya upagani kuingia Kanisani, ndipo kanisa likaingia katika #ZAMA ZA #GIZA, kilichoanza mwaka wa 538-1517, #NB: Zama za giza hazikuishia mwaka 1517, bali kuanzia mwaka huo yalianza mapambazuko ya kiroho. Hiki ndicho kipindi Biblia iliwekwa pembeni, bali mapokeo ndio yakachukua nafasi. Biblia ikawa inasomwa na Papa, Askofu na Padri tu. Wengine wakawa wasikilizaji tu. Na huu mfumo bado haujaisha katika kanisa la RC.
#Ufunuo wa Yohana 2:18-19
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana.
Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.
Kanisa likalizika likapokea upagani wa kirumi, Rumi ya kidini/ Upapa unafananishwa na Yezeberi, ambaye aliingiza upagani katika Taifa la Israeli; Lakini Mungu alilipa nafasi kanisa la Cathoric litubu uovu wake lakini liligoma:
#Ufunuo wa Yohana 2:20-21
Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.
Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake.Hiki ndicho kanisa lilishikamana na Ulimwengu sana,
#KANISA LA #SARDI:
Hiki ni kipindi kilichoanza mwaka 1715-1798, Baada ya kanisa kukaa Gizani kwa muda, hatimaye nuru ilianza kuonekana, na kipindi hiki pia kinaitwa kipindi cha Kanisa la Waprontestant wa Matengenezo.
#Ufunuo wa Yohana 3:1-2
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa.
Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu.
Hiki ni kipindi ambacho wana Matengenezo kama #Martin Luther, #Wesley, #Whitefield na wengineo walianza kuinuka na kupinga upagani uliokuwa unaendelea ndani ya Kanisa Katoliki, Martini Luther ambaye alikuwa ni Mkatoliki mzuri, lakini baada ya kubaini ukweli, akasimamia ukweli pasipo kuyumba, na Ndio mwanzo wa jina #WAPRONTESTANT, likiwa na maana ni wapinzani wa mafundisho potofu ya RC, cha kushangaza siku hizi kuna watu wanajiita #Waprontestant, lakini bado wanafuata mafundisho ya Katoliki, sasa sijui wana #Protestnini kwa RC
Hawa wapinzani ndio Biblia inawaita watu wachache katika kipindi cha Kanisa la Sardi ambao walikataa kufuata Upagani wa RC:
#Ufunuo wa Yohana 3:4-5
Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili.
Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake.
#KANISA LA #FILADEFIA:
Hiki ni kipindi ambacho kulikuwa na mwamko mkubwa wa Injili, kipindi hiki kilikuwa mwaka 1798-1844, mnamo mwaka wa 1831, ndipo kulikuwa na utangazaji wa injili kwa nguvu kwamba Yesu anarudi, mwamko huu wa injili uliongozwa na William miller.
#Ufunuo wa Yohana 3:7-8
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye.
Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu.
Baada ya Papa Pius kuwa mateka chini ya Jemedari wa Ufaransa mnamo mwaka 1798 na kufa huko, na hivyo Kanisa Katoliki halikuwa na uwezo tena wa kutawala Dini na Serikali, Kwa hiyo injili ilianza kupamba moto, mnamo mwaka wa 1833, ndipo waliinuka wahubiri wengi akiwemo William Miller aliyekuwa Mbaptist, wakahubiri kwamba mwisho wa Dunia ni mwaka 1844, Hiki ni kipindi ambacho Biblia zilichapwa kwa wingi na zilisambazwa kila mahari
Lakini wapo watu ambao walijichanganya katika imani kwa lengo la kupotosha mwamko wa injili, lakini hawakuweza, kwa sababu kipindi hiki Kanisa lilianza kulishika Neno la Mungu, na sio mapokeo.
#Ufunuo wa Yohana 3:9-10
Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda.
Ulipofika mwaka 1844, watu walitegemea Yesu angerudi mwaka huo, lakini hakuonekana, Hili lilikuwa ni jaribu kubwa sana, wale waliokuwa wakifuata mkumbo tu wengi walikata tama na kurudi nyuma kwenye mambo ya Dunia kama mwanzo. Lakini wale waliokuwa na Imani thabiti waliendelea kusonga mbele.
#Ufunuo wa Yohana 3:9-10
Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.
#KANISA LA #LAODIKIA:
#Ufunuo wa Yohana 3:14-16
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.
Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
Katika historia ya Kanisa hiki ni kipindi cha kuanzia 1844 hadi kurudi kwa Yesu. Laodikia maana yake #KUWAHUKUMU #WATU, hiki ndicho kipindi Yohana anaona malaika/ wajumbe wa Mungu wakitangaza ujumbe wa siku za mwisho juu ya hukumu, kuwaita watu watoke Baberi.
#Ufunuo wa Yohana 14:6-7
Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa,
akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya #hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.
Katika kipindi hiki ndipo Sabato ambayo ni ishara ya kukumbuka Uumbaji ilitiwa nguvu tena baada ya kudhoofishwa na upagani katika kanisa la Pergamo/ ZAMA ZA GIZA, sasa Mungu aliwainua tena watu kutangaza ujumbe wa Malaika wa kwanza juu ya ibada ya kweli. Na ndio maana wito wa Mungu ni kwamba watu #wamsujudu yeye aliyeumba mbingu na nchi na bahari, ina maana kwa muda mrefu watu walikuwa katika giza wakimtumikia shetani pasipo kujua kwa kuitukuza Jumapili. Kwa sababu ukweli ulifichwa. Hadi sasa ujumbe huu unaendelea kutangazwa kila mahali ikiwemo kwenye mitandao humu, kuwaita watu watoke kwenye mapokeo ya ibada ya jumapili, inayomtukuza Papa, Lakini watu bado mioyo ni migumu kama kipindi cha Nuhu. Na hata watu hawajiulizi kwanini SABATO inajadiliwa sana kwenye mitandao kuliko masomo mengine? Ni mpango wa Mungu watu waujue huu ukweli, ili uwe ushuhuda siku ya mwisho.
Hatari ya kipindi hiki cha Laodikia watu wanajiona ni mataji wa kiroho, wakati sio.
#Ufunuo wa Yohana 3:15-18

Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.
#Ufunuo wa Yohana 3:18
Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
#Dhahabu ni Imani ya Yesu
#Mavazi meupe ni Haki ya Yesu
#Dawa ya macho ni Roho mtakatifu.
Hiki hakika ni kipindi chetu, Makanisa yanazidi kuongezeka, na watu wanajiona wako sahihi kwa kila jambo. Imani haijajengwa kwa Yesu bali imejengwa kwa Viongozi wa dini, watu hawamtafuti Mungu makanisani, bali asilimia kubwa wanatafuta #Miujiza, #Utajiri, #Kujionesha NK, ndio maana wanaonekana ni Vuguvugu, Kumpenda Mungu kupo na kuupenda ulimwengu kupo, Watu wamechanganya mambo ya Dunia na mambo ya Mungu kuwa sehemu ya Ibada,
1. Mapambo ya Kidunia yamekuwa ndio mapambo ya washiriki ndani ya Kanisa.
2. Muziki wa kidunia unabadilishwa tu maneno na kuwekwa maneno ya Mungu, lakini midundo ni ileile.
3. Style za kucheza za kidunia ndio zimekuwa zikitumika Makanisani. Mfano Viduku.
4. Wachungaji hawahubiri injili za kuwafanya watu waache dhambi, bali injili ni zile LAINI kama miujiza, Utajiri, Uponyaji, Amani,Upendo Nk.
Injili ngumu za kuonesha hatari inayoujia ulimwengu wengi hawapendi, ni mara chache sana watu kufundishwa UNABII, Kukemea dhambi, watu wanataka uhuru, sheria hawataki wanaona zinaingilia anasa zao:
#Isaya 30:9-11
Kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia #sheria ya Bwana;
wawaambiao waonaji, Msione; na manabii, Msitoe unabii wa mambo ya haki, tuambieni maneno laini, hubirini maneno yadanganyayo;
Wito wa Mungu kwa Kanisa la Laodikia ni huu:
#Ufunuo wa Yohana 3:20-21
Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.
Watu wengi wamefunga milango ya mioyo yao kwa kung’ang’ania mafundisho ambayo ni mapokeo ya wanadamu, na wakati huo wanajiona ni matajiri wa kiroho, wanajiona wameridhika na imani walizo nazo kana kwamba ndio tiketi ya kuelekea mbinguni.
Kanisa hili la Laodikia ndilo kanisa linaloenda kufunga Historia ya ULIMWENGU, Sasa wengi wanataka kufunga historia kwa kukumbatia Mapokeo na sio imani ya Yesu.
Mungu akuongoze katika kufanya uchaguzi wa kumtii katika Roho na Kweli
Mawasiliano
0627729770

Comments
Post a Comment