TUJIKUMBUSHE KIDOGO
UNABII WA DANIELI SURA YA 7:
kati ya masomo muhimu sana katika nyakati hizi za mwisho ni pamoja na Unabii, lakini pia ni kati ya masomo yanayoogopwa na wengi ni unabii. Sasa watu wengi wanaogopa unabii kwa sababu umetumia sana lugha za picha au mifano, Kwa sehemu kubwa katika vitabu vya Danieli na Ufunuo Mungu ametumia sana mifano kwa sababu: kuilinda Biblia iwe salama kwa sababu Mifano mingi iliyotumika katika vitabu hivi inawahusu Viongozi wa siasa na Dini na hata Mataifa mbalimbali, kama tutakavyoona mbeleni.
Hivyo Unabii unakuwa mwepesi endapo utajua maana ya mafumbo yaliyotumika na unabii unakuwa mgumu endapo hujui maana ya mafumbo au mifano iliyotumiwa katika uandishi.
Katika somo hili tupate mwongozo wa baadhi ya lugha za picha katika kitabu cha Daniel sura ya 7.
1.BAHARI- inaashiria watu wengi(mataifa)- Ufunuo 17:15, Isaya 17:12-13.
2. PEPO(UPEPO)- Huashiria machafuko(vita) Yeremia 49:36-37
3. WANYAMA- Inaashiria Ufalme/Utawala- Daniel 7:17,23
4. VICHWA/KICHWA- Inaashiria Kiongozi/ mtawala 1Korintho 11:3
5. PEMBE- Inaashiria Mfalme /Ufalme Daniel 7:24, Daniel 8:5,21,22.
6. MABAWA YA TAI- Inaashiria Kasi/ wepesi. Habakuki 1:6-8
BIBLIA inasema: #Danieli:7:2-4 "Danieli akanena, akisema, Naliona katika maono yangu wakati wa usiku; na tazama, hizo pepo nne za mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa. Ndipo wanyama wakubwa wanne wakatoka baharini, wote wa namna mbalimbali. Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa kibinadamu.
Danieli sura ya 7 inazungumzia kuinuka kwa mfumo wa utawala wa kisiasa na dini utakaotawala Dunia tangu kipindi cha Ufalme wa Babeli mpaka mwisho wa Dunia. Maana aya ya 17 inasema "Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne watakaotokea duniani"
Sasa ikiwa Wanyama ni Wafame na Bahari ni Mataifa na PEPO ni vita au machafuko kama tulivyoona, hii inamaana kwamba #Danieli aliona vita/ machafuko ya kisiasa na Dini yakifanyika Duniani, na wakati vita vikipigwa walikuwa wakiinuka Wafalme kuitawala Dunia.
Daniel anaona mnyama wa kwanza kuinuka alikuwa na mfano wa SIMBA. Mnyama #Simba# anawakilisha Ufalme/utawala wa Babeli uliotawala Dunia tangu mwaka 605-539. #NB: zamani kabla ya kuzaliwa kwa Yesu miaka ilihesabiwa kutoka juu kuja chini. Simba huyu alikuwa na mabawa ya tai, ikiashiria Ufalme wa Babeli ulikuwa na kasi/ wepesi katika kuteka majimbo.Utawala huu wa Baberi ulikuwa tajiri, lakini ni moja ya utawala uliokuwa unaabudu sana sanamu, hata katika majengo yao kulikuwa na masanamu, na ndio kipindi hiki ambapo wale rafiiki zake Danieli walitupwa kwenye tanuru la moto kwa sababu walikataa kuisujudia sanamu ya mfalme.
MNYAMA WA PILI ALIKUWA KAMA DUBU
Biblia inasema: #Danieli:7:5 Na tazama, mnyama mwingine, wa pili, kama dubu, naye aliinuliwa upande mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo kinywani mwake katika meno yake; wakamwambia mnyama huyo hivi, Inuka, ule nyama tele.
Mnyama Dubu huwakilisha Ufalme wa UMEDI NA UAJEMI. Baada ya mfalme Belteshaza kunajisi vyombo vitakatifu kwa kunywea pombe Mungu ikabidi autoweshe Ufalme wa Babeli kwa kuangushwa na Wamedi na Waajemi( rejea Daniel sura ya 5) Ufalme wa Umedi na Uajemi ulifanikiwa kuuangusha Ufalme wa Babeli mnamo mwaka 539,
Ufalme huu ulitawala Dunia yote tangu mwaka 539-331. Biblia inasema mnyama Dubu alikuwa na mifupa mitatu mdomoni, mifupa iliyokuwa mdomoni iliashiria Majimbo makuu matatu waliyo tawala Wamedi na Waajemi 1. Babeli 2. Misri 3. Lidya. Ufalme huu ulikuwa na wafame mbalimbali walioongoza kama Dario, Koreshi, Artashasta, Ahusuero nk.Umedi na Uajemi ni moja ya ufalme uliokuwa katiri kwa sababu sheria zao zilikuwa hazibadiliki, na ndio kipindi hiki Daniel alitupwa katika tundu la Simba, na hata mfame alishindwa kumuokoa Daniel kutokana na misimamo yao ya kisheria,
Hivyo hata utawala utakaoenda kufunga historia ya Dunia umebeba sifa za Wanyama hawa wote( soma Ufunuo 13). Watu wa Mungu watawekewa sheria Kali zisizoweza kubadilika, hivyo wengine watatupwa magerezani, wengine kufukuzwa kazi, wengine kupokonywa Mali zao kwa sababu wamekataa kutii sheria za kidunia zinazopingana na utaratibu wa Mungu Kama ilivyo kuwa kwa DANIELI,
Lakini Yesu anasema Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka# Matha 24:13 ,Daniel alivumilia #Akaokoka# katika tundu la Simba. Dhiki kwa watakatifu ni lazima Biblia inasema # Imetupasa kuingia katika Ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi# Matendo 14:22
Umedi na Uajemi haupo kiutawala lakini mfumo wake wa kiutendaji ndio utakaotumika kuwatesa watakatifu.
MNYAMA WA 3 KAMA CHUI,
Biblia inasema: #Danieli:7:6 Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.
Mnyama Chui sio mnyama mkubwa wa kutisha, bali ni hatari, # mnyama huyu Chui anawakilisha Ufalme wa Uyunani/ Ugiriki, uliotikisa Dunia baada ya kuuvamia Ufalme wa Umedi na Uajemi mnamo mwaka 331, Kijana mashuhuri anayefahamika sana hata katika historia ambaye anaitwa Alexander Mkuu(Alexander the great) ndiye aliye uangusha Ufalme wa Umedi na Uajemi, ufalme huu ulitawala Dunia kuanzia mwaka 331BC- 168BC. Mfame huyu alihakikisha anateka Dunia, na ili kuiteka Dunia yote alianzisha vyuo ambavyo watu walijifunza sana mambo ya Dunia kuliko mambo ya Mungu, na alihakikisha lugha ya Kigiriki inasambaa duniani, ndio maana hata BIBLIA agano jipya imeandikwa Kigiriki, baadala ya Kiebrania.
Alexander, inasemekana alikufa akiwa kijana wa miaka 32 kutokana na ulevi. Biblia inasema Chui alikuwa na vichwa vinne (4), hii inaashiria Majemedari wanne wa Alexander, baada ya Alexander kufa majemedari wake waligawana Majimbo, pande zote, kusini, kaskazini, mashariki na magharibi.
Baada ya Alexander kufa, na majemedari kugawana Majimbo, basi utawala wa Uyunani ulidhohofu na maadui wakapata mwanya wa kuvamia mnamo mwaka 168,
Lakini SIKU za mwisho utawala utakaotawala Dunia utakuwa na tabia kama za Uyunani ( rejea Ufunuo 13)
#MNYAMA WA 4, NI MNYAMA WA KUTISHA.
Danieli:7:7 Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.
Wanyama wengine wote Daniel aliwatambua majina yao, lakini mnyama wa 4 Danieli alishindwa kumjua anafanana na mnyama gani, na akaishia kusema ni mnyama wa kutisha, na ikamfanya Danieli atake kujua kuhusu huyu mnyama aliyekuwa tofauti na wengine.
Utawala huu si mwingine bali ni utawala wa RUMI YA KIPAGANI, Rumi ilitawala Dunia tangu mwaka 168BC -476AD,
Wakati Yesu anazaliwa Rumi ndio ilikuwa inajiimarisha vizuri katika utawala, na hivyo ili kuitawala vizuri Dunia ilibidi kupata sensa ya watu wote Duniani (luka 2:1), Na ndio maana hata Yesu alisulubishwa na Askari wa Kirumi, isitoshe hata wanafunzi wengi wa Yesu walifia Rumi kama Paul, Petro, Bathromayo NK., maana ndiko yalikuwa makao makuu ya Dola ya Kirumi ,mahakama na magereza; Utawala huu ulikuwa unasimamiwa na Kiongozi mwenye cheo cha KAISARI.
Ilipofika mwaka 476, Rumi ilidhoofu katika utawaa, hivyo haikuweza kutawala Dunia vizuri, na ikapelekea utawala huu kugawanyika, na yakainuka Mataifa 10 maarufu katika bara la Ulaya, ambazo ndio zile pembe 10 za mnyama. Mataifa hayo ni pamoja na Uingereza, Ujerumani, Italia, Ufaransa, Hispania, Ureno, Uswizi, Heluli, Vandali na Othrogoth.
Lakini taratibu Rumi ilianza kujiingiza kwenye dini, na baadaye ikachanganya dini na serikali, na ndio maana Daniel anashindwa kumtambua huyu mnyama, maana kwenye dini Yupo na kwenye serikali Yupo, wakati wanyama watatu wa kwanza walikuwa kwenye siasa(serikali) peke yake.
KUINUKA KWA VATICAN (UPAPA)
BIBLIA inasema #Danieli:7.8 Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang'olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu. Nikatazama, na pembe iyo hiyo ilifanya vita na watakatifu, ikawashinda;
Wakati Daniel akitazama utawala wa Kirumi, na kuinuka kwa mataifa 10, anaona katikati ya yale mataifa moja wapo, likajitokeza Taifa(ufalme). Kilichomshangaza zaidi Danieli ni kwamba anaona Miongoni mwa yale mataifa(pembe) likazaliwa taifa jingine, yaani mfano Nchi ya Tanzania, ndani yake tena kuwe na nchi nyingine tena..
Cha ajabu ni kwamba utawala huu ukawa una nguvu kuliko mataifa makongwe, na ukafanya mambo yafuatayo.
1. Ukazing'oa pembe 3(mataifa 3) miongoni mwa yale 10.(Dan 7:8)
2. Ukamkufuru Mungu(Dan 7:8)
3. Ukawatesa watakatifu(Dan 7:21)
4. Ukabadili majira na sheria(Dan 7:25)
Huu utawala si mwaingine, Bali ni utawala wa Vatican (Upapa), Maana BIBLIA inasema pembe ndogo itainuka katikati ya moja ya zile pembe 10 na itang'oa pembe 3.
Katika Dunia hakuna Nchi iliyo ndani ya nchi ambayo inajihusisha na mambo ya Dini, zaidi ya nchi ya Vatican iliyo ndani ya Nchi ya Itali. Vatican ni moja ya nchi ndogo Duniani, na yenye watu wachache, na kiongozi wake ni Papa, na ina mabalozi wake kila nchi Duniani, na ina Jeshi lake.
Utawala huu ulipoanza kuinuka ulitokea kwenye upagani, LAKINI taratibu ukajiingiza kwenye mambo ya Dini, na ulipoanza kuinuka baadhi ya mataifa yalikataa kutawaliwa na yakang'olewa kabisa, mataifa hayo hayapo kabisa Duniani, ambayo ni Heluli, Vandari na Othrogoth.
Utawala huu wa Kipapa ili kutawala kwa urahisi ilibidi Iwaangamize Watakatifu, waliokuwa wakipinga mafundisho potofu. Ndio maana Biblia inasema: Danieli 7:25 Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, #naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati. Na baada ya kufanikiwa kuwadhoofisha Watakatifu ndipo ikabadili Amri ya Ibada kutoka jumamosi na kuipeleka jumapili
Wakaingiza Ibada za sanamu, ubatazo wa kunyunyiza, Krismas, Easter nk. Pia wakabadili majira baadala ya siku kuisha jua linapozama wakasema siku inaisha SAA 6 usiku.Mwaka una siku 360, wao wakachakachua hadi ukawa na siku 365 Miezi yote ina siku 30, lakini wakachakachua hadi sasa kuna miezi yenye siku 28, 29, 30 na 31.
Hii ndio KAZI ya pembe ndogo. Baada ya kufanikiwa kuwadoofisha watakatifu, ndipo mapokeo hayo ya kipagani yakafanywa sehemu ya mafundisho ya dini, Kwa hiyo kuanzi miaka ya 538 hadi miaka ya 1517, Ukataoliki ukawa unatawala dini na serikali.
Mnamo mwaka wa 1798, ndipo upapa, uliangushwa baada ya Papa Pius kuchukuliwa mateka na kupelekwa Ufaransa na akafia huko, na hapa ndipo Upapa ulipopata jeraha la mauti, maana ulinyang’anywa mamlaka ya kutawala Dini na Serikali, na ikabakiwa na mamlaka ya Dini peke yake.
Ufunuo wa Yohana 13:3-4 Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.
;Kwa hiyo mikakati ya Dunia kwa sasa ni kuirejesha tena Vatican kutawala Dunia katika Dini na Serikali kama ilivyokuwa mwanzo. Hivyo kwa sasa wanajitahidi kuunganisha madhehbu yote kuwa kitu kimoja,(UMOJA WA MAKANISA) kwa kigezo cha kutafuta amani, kisha itafuata kuunganisha Dini na Serikali, na hapa ndipo Upapa utatawala Dini na Serikali, lakini Biblia inasema:
1 Wathesalonike 5:3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.
Sasa hivi imesha zoeleka hata katika Nchi yetu utasikia kuna Maombi ya kuombea Amani, Viongozi wa Dini wanazunguka katika Dunia wakisema wanatafuta Amani, lakini Biblia inasema: Ezekieli 7:25-26 Uharibifu unakuja; nao watatafuta amani, lakini haitapatikana. Madhara yatakuja juu ya madhara, na habari ya shari juu ya habari ya shari;
Hii ndio hatari inayoendelea Duniani,
………….Mungu Akubariki……………….
0627729770
0689980058

Comments
Post a Comment