Torati katika Agano Jipya!
Zaburi 119:152 “Tokea zamani nimejua kwa shuhuda zako, Ya kuwa umeziweka zikae milele.”
Miaka 2000 sasa tangu Bwana wetu Yesu Kristo apae kwenda mbinguni, lakini waKristo wengi wanatangaza wazi kuwa sheria/amri za Mungu zilitanguka. Wanahubiri kwamba mKristo si lazima atii amri za Mungu ili kupata uzima wa milele, bali anaweza kuvunja amri za Mungu lakini bado atapata uzima wa milele. Hivyo wanafundisha kuwa kama ukimwamini Yesu tu, hata kama ukihalifu amri za Mungu utapata uzima wa milele.
Baada ya kusikiliza madai ya watu hawa kwa muda mrefu, nimeamua kuunda ukrasa huu wenye mafungu kadhaa ya Maandiko yanayothibitisha kuwa watu hawa wanatangaza uongo na wako kinyume na Neno la Mungu.
Sheria na Agano Jipya.
Baadhi ya watu hawa wameenda mbali sana hata kudai kuwa sheria ilipaswa kutunzwa katika agano la kale pekee, lakini sio katika agano jipya la damu ya Yesu Kristo, Lakini tukiangalia katika Maandiko yafuatayo tunaona wazi kuwa watu hawa wanafundisha uongo.
2Wakorinto 3:3 inasema, “mnadhihirishwa kwamba mmekuwa barua ya Kristo tuliyoikatibu, iliyoandikwa si kwa wino, bali kwa Roho wa Mungu aliye hai; si katika vibao vya mawe, ila katika vibao ambavyo ni mioyo ya nyama.”
Kumbe sisi (waKristo) tu barua ya Kristo iliyoandikwa kwa njia ya Roho wa Mungu ndani ya mioyo yetu. Katika Agano la kale barua ya Kristo iliandikwa kwa kidole cha Mungu Mwenyewe katika mbao mbili za mawe, lakini katika Agano jipya barua ileile ya Kristo inaandikwa katika moyo wa kila mKristo kwa njia ya Roho Mtakatifu. Hivyo, tofauti kati ya agano la kale na jipya ni kwamba, katika agano la kale barua ya Kristo iliandikwa katika mbao mbili za mawe, lakini katika agano jipya barua ya Kristo inaandikwa katika mbao za nyama ambazo ni mioyo yetu. Je barua hiyo ya Kristo ni nini? Barua ya Kristo ni sheria za Mungu zilizokuwa zimeandikwa zamani katika mbao za mawe!
Waebrania 8:8, 9, 10 inasema, “Angalia siku zinakuja, asema Bwana, Nami nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda AGANO JIPYA; Halitakuwa kama AGANO lile nililoagana na baba zao, Katika siku ile nilipowashika mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri…Maana hili ndilo AGANO nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu.”
Waebrania 10:16 pia inasema, “Hili ni agano (jipya) nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, Na katika nia zao nitaziandika.”
Barua ya Kristo ni sheria ya Mungu ambayo inawekwa katika nia zetu na inaandikwa katika mioyo yetu. Sehemu kubwa katika agano jipya ni imani. Hivyo katika agano jipya tunapomwamini Yesu kuwa ni Mwana wa Mungu na kubatizwa, tunazaliwa upya mara ya pili kwa njia ya ubatizo, tunapewa Roho Mtakatifu ambaye kwa kuendelea huzigeuza nia zetu zifanane na sheria ya Mungu, mpaka wakati ambapo tunafananishwa na sura ya Mungu kikamilifu na tabia zetu zinageuzwa kuwa kama tabia ya Mungu ambayo haiwezi kuasi sheria zake, kwa jinsi kama hiyo ndipo sheria (barua ya Kristo) inakuwa imeandikwa kikamilifu ndani ya mioyo na nia zetu.
Hivyo Agano jipya ambalo linahusika hasa na imani haliiondoi sheria ya Mungu, wala imani yetu katika Kristo haiiondoi sheria ya Mungu, bali imani inaleta Roho Mtakatifu ndani yetu, ambaye anatugeuza nia zetu zifanane na sheria ya Mungu, na hivyo tunakuwa na uwezo wa kuitenda sheria. Paulo anauliza, “Basi je twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? Hasha kinyume chake twaithibitisha sheria.” Warumi 3:31. Yaan, agano jipya haliitangui sheria kwa sababu ya imani, bali agano jipya ndilo hutusaidia sisi kupitia imani kwa njia ya ubatizo kupata Roho Mtakatifu ambaye hutufanya sisi tuitende sheria.
Amri 10 Zote Katika Agano Jipya.
Agano Jipya na imani haviiondoi sheria ya Mungu bali vinatoa msaada kwa mtu ili aitimize sheria. Hapa tutaangalia sheria moja moja katika amri kumi za Mungu, Tutaangalia amri katika agano la kale, kisha tutaangalia uthibitisho katika agano jipya ambao unathibitisha kuwa waKristo wanapaswa kuitunza.
Amri ya Kwanza.
Kut 20:3 “Usiwe na miungu mingine ila mimi.”
Katika Agano Jipya Yesu akathibitisha kuwa amri hiyo bado inapaswa kutunzwa na watu wake, akasema,
“Na mmojawapo wa waandishi akafika, akawasikia wakisemezana naye, akatambua ya kuwa amewajibu vema, akamwuliza, Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza? Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.” Marko 12:28-29. “Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.” Mathayo 22:38.
Ukimpenda Mungu huwezi kuabudu miungu mingine.
Amri ya pili.
Kut 20:4-6 “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.”
Agano Jipya linathibitisha kuwa amri hii ya pili waKristo lazima waitii.
1Yohana 5:21 “Watoto wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu.”
1Wakolinto 10:14 “Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu ikimbieni ibaada ya sanamu.”
1Wakorinto 10:19-21 “Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au sanamu ni kitu? Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.”
2Wakorinto 6:16-17 “Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo, tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema BWANA.”
Amri ya Tatu.
Kut 20:7 “Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.”
Agano Jipya pia linathibitisha kuwa hatupaswi kulitaja bure jina la Mungu.
Mathayo 5:33:37 “Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana viapo vyako; lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu; wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu. Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.”
Yakobo 5:12 “Lakini zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, wala kwa mbingu wala kwa nchi; wala kwa kiapo kinginecho chote; bali diyo yenu na iwe ndiyo, na siyo yenu iwe siyo, msije mkaangukia hukumu.”
Je umeona ni jinsi gani Yesu alivyoitimiliza torati? Torati katika kipindi cha Wayahudi ilikuwa na mapungufu, Yesu alipokuja alitimiliza, akatuambia, tusilitaje jina la Mungu bure kama Waisraeli walivyolitaja wakati wa viapo. Yesu akatuambia kuwa “…Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.” Mathayo 5:20
Amri ya Nne.
Kut 20:8-11 “Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.”
Agano Jipya pia linathibitisha kuwa waKristo wote wanapaswa kutii amri hii ya nne. Yesu Mwenyewe ambaye ndiye Agano Jipya lenyewe alitii amri ya nne, tena kwake ilikuwa ni desturi.
Luka 4:16 “Akaenda nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.”
Pia Yesu alipokuwa anatabiri kuhusu kuangamizwa kwa mji wa Yerusalemu na mwisho wa dunia alisema,
Mathayo 24:20-21 “Ombeni, ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato. Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.”
Dhiki hii haikuwepo wakati wa Yesu, ni dhiki itakayotokea mwishoni kabisa mwa ulimwengu, na Yesu anatuambia “ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe katika siku ya sabato”. Yesu Mwenyewe anajua kuwa watu wake watatunza sabato hadi mwisho kabisa wa dunia. Hii ni ajabu kwa wale watakaoendelea kupinga ukweli wa kutii amri ya nne.
Baada ya Yesu kupaa mbinguni wanafunzi wake wote waliendelea kutunza sabato mpaka walipokufa. Siku ya pentekoste ilikuwa ni jumapili, hivyo jana yake ilikuwa ni jumamosi, na Biblia inasema, kuwa siku ya jumamosi wanafunzi wa Yesu walikutana nyumbani ili kusali (soma Matendo 1&2). Pia Paulo naye alitii amri ya nne, tena kwake ilikuwa ni desturi kama vile kwa Yesu,
Matendo 17:2 “Na Paulo kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu.”
Tena Paulo hakuhojiana na Wayahudi pekee siku ya sabato, bali na watu wa mataifa pia.
Matendo 18:4 “(Paulo) Akatoa hoja zake katatika sinagogi kila sabato, akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wayunani.”
Agano jipya kamwe haliondoi sheria ya nne, agizo lilitolewa katika Waebrania 4, kwamba waKristo lazima wafanye bidii kutunza sabato ili wasije kuangukia hukumu ya kuasi.
Waebrania 4:4, 9, 10, 11 “Kwa maana ameinena siku ya saba mahali fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote;…Basi imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu. Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake. Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu ye yote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi”
Amri ya Tano.
Kut 20:12 “Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.”
Agano Jipya pia linafundisha kwamba tuitii amri ya tano, tuwaheshimu wazazi.
Waefeso 6:1-4 “Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia. Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.”
Siku zote agano jipya haliitangui sheria ya zamani, bali linaithibitisha zaidi, linatufundisha kuwa lazima tuitii amri ya tano, tuwaheshimu wazazi. Lakini linawakumbusha wazazi pia kwamba, nao wanapaswa wawalee watoto wao katika adabu, wala wasiwachokoze watoto.
Maneno mengine ambayo hayawezi kupingika ni Maneno ya Yesu pale alipotuambia kuwa kama tukitaka uzima wa milele, lazima tuzitii amri 10 ikiwemo na amri ya kuwaheshimu wazazi wetu.
Mathayo 19:16-19 “Na tazama, mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu, nitende jambo gani jema, ili nipate uzima wa milele? Akamwambia…ukitaka kuingia katika uzima zishike amri. Akamwambia zipi? Yesu akasema, Ni hizi, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Waheshimu baba yako na mama yako, na Mpende jirani yako kama nafsi yako.”
Amri ya Sita.
Kut 20:13 “Usiue.”
Agano Jipya pia linathibitisha kuwa waKristo hawapaswi kuua, soma Mathayo 19:16-19 hapo juu. (angalia pia Marko 10:19; Luka 18:20).
Yakobo 2:11 “Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria.”
Aliyezitoa sheria ni mmoja, mtu akivunja sheria moja bado ana hatia ya kufanya dhambi. Kitu ninachokipenda sana katika Agano Jipya la damu ya Yesu Kristo ni kwamba, Agano Jipya linathibitisha wazi kabisa kuwa sheria haitanguki, kisha linaiongeza haki ambayo ilipungua katika Agano la kale, ili Upendo uzidi na uasi ukome. Yesu alikuja kulitimiliza torati wala si kulitangua (angalia Mt 5:15-17), Alipokuja alithibitisha kuwa amri ya 6 haitanguki, tena juu yake aliongeza haki ambayo huwa nafurahi sana kuiona pale, alisema,
Mathayo 5:21-22 “Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua itampasa hukumu. Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake itampasa baraza; na mtu akimwapiza itampasa jehanamu ya moto.”
Hii ndiyo sababu upendo ni amri kuu ya kwanza kuliko zingine zote, kwa maana ukimchukia mtu unakua na hatia ya mauaji, lakini ukiwa na upendo utatimiza sheria za Mungu zote bila kinyongo, wala hutajikwaa katika sheria yoyote. Hii ndiyo maana katika Agano Jipya tumepewa sheria ya upendo, kuwapenda watu wote hata maadui wetu (angalia Mathayo 5:43-48). Sheria ya upendo ndiyo kuu, nayo ndiyo inategemea torati yote.
Warumi 13:8-10 “Msiwiwe na mtu chochote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria. Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.”
Amri ya Saba.
Kut 20:14 “Usizini.”
Agano Jipya pia linathibitisha kuwa lazima tuitii amri ya 7, Yesu alisema,
Marko 10:11-12 “Akawaambia, Kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake; na mke, akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine, azini.”
1Kor 7:10-11 “Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe; lakini ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asmwache mkewe.”
Mathayo 5:31 “Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka; lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.”
Agano Jipya haliitangui sheria bali linaiongeza haki katika sheria, Yesu alituambia kuwa hata mtu akimwangalia mwanamke kwa kumtamani huyo anazini.
Mt. 5:27-29 “Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.”
Amri ya Nane.
Kut 20:15 “Usiibe.”
Agano Jipya halifundishi mahali popote kwamba waKristo waibe au wasiti amri ya nane, agano jipya pia linafundisha watu waitii amri ya 8 ya Mungu.
Waefeso 4:28 “Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji.”
1The 4:11-12 “Tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe, kama tulivyowaagiza; ili mwenende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na haja ya kitu chochote.”
Kwa ajili ya mafungu mengine yanayowakataza waKristo wasivunje amri ya 8 angalia Mathayo 19:18; Marko 10:19; Luka 18:20; Warumi 13:9 na 1Timotheo 1:10.
Amri ya Tisa.
Kut 20:16 “Usimshuhudie jirani yako uongo.”
Agano Jipya linathibitisha kuwa waKristo lazima wasiseme uongo, na kwamba waongo wote kamwe hawatauingia ufalme wa mbinguni.
Waefeso 4:25 “Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha mwenzake.”
Wakolosai 3:9 “Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake; mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba.”
Wale watakaoingia katika ufalme wa Mungu uongo haukuonekana katika midomo yao.
Ufunuo 14:4-5 “Hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo. Na katika vinywa vyao haukuonekana uongo. Maana hawana mawaa.”
Waongo watatupwa jehanamu wafe kifo cha milele.
Ufunuo 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wanzinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa la moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.”
Amri ya Kumi.
Kut 20:17 “Usitamani nyumba ya jirani yako, usitamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.”
Agano Jipya linathibitisha kuwa lazima waKristo wote watii amri hii, hawapaswi kuwa na tamaa, wala kutamani.
Waefeso 5:3 “Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu.”
Wakolosai 3:5 “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibaada ya sanamu; kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu.”
Yesu alisema mtu akitazama mwanamke kwa kumtamani, huyo amezini naye moyon mwake, hivyo mfano huu unaweza kutumika katika amri za Mungu zote; kwa mfano mtu akitamani kitu cha mtu, huyo ameiba kitu hicho moyoni mwake.
Mt 5:27-28 “Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.”
Wenye tamaa wote hawataurithi uzima wa milele.
Waefeso 5:5 “Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu.” (soma pia 1Kor 6:9-10)
Mpaka hapa tumeona hakuna moja katika amri kumi za Mungu ambayo Wakristo wanaweza kuivunja, Agano Jipya linazithibitisha amri zote ya kuwa zinapaswa kutunzwa na waKristo wote. Kuna amri nyingi sana ambazo waKristo wanawiwa kutii, lakini hapa nimetoa uthibitisho wa amri 10 tu zilizoandikwa kwa kidole cha Mungu Mwenyewe. Hii haimaanishi kwamba tunapaswa kutii amri 10 hizo pekee. Hapana! Bali tunapaswa kutii Maneno yote ya Mungu ambayo Agano Jipya linayathibitisha kuwa tunapaswa kuyatenda.
Msimamo wa Yesu na Mitume juu ya Torati.
Yesu anasema…
Mathayo 5:17-18 “Msidhani ya kuwa nalikuja kulitangua torati au manabii; la, sikuja kulitangua bali kulitimiliza. Kwa maana amini nawaambia, mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.”
Luka 16:15-17 “Akawaambia, Ninyi ndinyi mnaojidai haki mbele ya wanadamu, lakini Mungu awajua mioyo yenu; kwa kuwa lililotukuka kwa wanadamu huwa chukizo mbele za Mungu. Torati na manabii vilikuwepo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu. Lakini ni vyepesi zaidi mbingu na nchi vitoweke kuliko itanguke nukta moja ya torati.”
Yesu alisema kama tunataka kupata uzima wa milele lazima tuzishike amri za kwenye torati.
Mathayo 19:16-17 “Na tazama, mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu, nitende jambo gani jema, ili nipate uzima wa milele? (Yesu) Akamwambia…ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri.”
Marko 10:17-20 “Hata alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele? Yesu akamwambia…Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako. Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu utoto wangu.”
Kama tunampenda Yesu tutazishika amri zake. (Na tafadhari kumbuka kwamba: Kama tukizishika amri zake dipo tunadhihirishwa kuwa tumekuwa barua (sheria) yake ambayo haijaandikwa juu ya mbao mbili za mawe kama ile ya mlima sinai, bali kupitia imani sheria hiyo hiyo anaindika juu ya mioyo na nia zetu kwa Roho wa Mungu, ili tuitende sheria (angalia 2Kor 3:3&Ebr 10:16).
Yohana 14:15-18 “Mkinipenda, mtazishika amri zangu. (16)Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; (17)ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.”
Kumbe tukimpenda na kuzishika amri zake, Yeye anatupa msaidizi mwingine ambaye ni Roho Mtakatifu ili tuweze kuzitii amri zake.
Yohana 14:21 “Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.”
Kama tukimjua Yesu lazima tuzishike amri zake.
1Yohana 2:4 “Yeye asemaye, nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake.”
Kama tukikaa ndani ya Yesu inatupasa tuenende vilevile kama Yeye alivyoenenda.
Yohana 2:6 “Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda.”
Je unadhani Yesu alienendaje nini ilikuwa desturi yake?

Kama tukivunja sheria moja katika torati tunaangukia hukumu ya kuvunja zote.
Yakobo 2:10 “Maana mtu awaye yote atakayeshika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.”
Mitume wote pamoja na Paulo waliamini kuwa torati haijatanguka, katika maisha yao yote hadi kifo chao walitunza sheria zote ikiwemo na sheria ya Sabato, Paulo alisema anaamini torati na manabii.
Matendo 24:14 “Ila neno hili naungama kwako ya kwamba kwa Njia ile ambayo waiita uzushi, ndivyo ninavyomwabudu Mungu wa baba zetu, nikiyaamini yote yanayopatana na torati na yaliyoandikwa katika vyuo vya manabii.”
Mitume wote walitunza amri zote za Mungu ikiwemo na amri ya Sabato, Lakini sasa hivi kuna maelfu ya watu wanaohubiri kwamba sabato ya amri ya 4 ni kivuli cha mambo yajayo. Wengi hunukuu maelezo ya Paulo katika Wakolosai 2:16 ili kusema ni halali kuvunja amri ya nne ya Mungu, Lakini sabato zilizotajwa hapo kwenye Wakolosai 2:16 ni sabato za mwaka, wala si sabato ya wiki ya amri ya Mungu (angalia Walawi 23:23-38).
Tangu Paulo ahubiri ukweli kuhusu kuhesabiwa haki kwa njia ya imani pekee, na sio kwa matendo ya sheria. Wengi wanaopenda kuenenda katika tamaa zao wameharakisha sana kusema, waKristo hawapaswi kutunza sheria za Mungu, bali kuwa na imani tu; ni kana kwamba wafunafundisha kuwa, wakriso wanapaswa kuwa na imani isyozaa matunda. Lakini Paulo mwenyewe hakufundisha hivyo, bali alisema, “Basi je twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? Hasha kinyume chake twaithibitisha sheria.” Warumi 3:31
Yakobo 2:14, 17, 19-20, 24, 26 “Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! Ile imani yaweza kumwokoa?…imani isipokuwa na matendo imekufa nafsini mwake…Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka. Lakini wataka kujua wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai?…mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake…Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.”
Ni mpaka imani yetu iwe imani inayothibitisha sheria, lakini tukiwa na imani inayobatilisha sheria. Ndugu natuangalie; Maana Maandiko hayafundishi kitu kama hicho. “Basi je twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? Hasha kinyume chake twaithibitisha sheria.” Warumi 3:31
Wakristo wa kweli wa leo ni wale wanaoshika amri za Mungu na kuwa na imani ya Yesu.
Ufunuo 12:17 “Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.”
Ufunuo 14:12 “Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.”
Ufunuo 22:14 “Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.”
Tunajua wengi wanaohubiri kuwa sheria ilitanguka, hasa hasa wanapinga amri ya 4 ya Sabato, wanasema kuwa amri hiyo ni kivuli cha mambo yajayo. Sasa swali langu ni kwamba, kama sabato ya amri ya Mungu ni kivuli, na Paulo mwenyewe aliitunza mpaka siku ya kifo chake. Je mnahubiri kwamba Paulo naye alikuwa chini ya kivuli? Na kama kutunza sheria na sabato ni kuwa chini ya sheria kama mnavyodai, na Paulo mwenyewe alitunza sheria na sabato. Je mnamaanisha kuwa Paulo naye alikuwa chini ya sheria? Ninauhakika kabisa kuwa yawezekana katika siku zetu hizi asiwepo mtu anayehubiri haki kwa imani pekee, kama vile alivyohubiri Paulo zamani zile, lakini Paulo alitunza sheria na sabato. Fikiria kuhusu hilo.

Comments
Post a Comment