TABIA 10 MBAYA ZILIZOZOELEKA MAKANISANI, AMBAZO NI MACHUKIZO MBELE ZA MUNGU.

TABIA 10 MBAYA ZILIZOZOELEKA MAKANISANI, AMBAZO NI MACHUKIZO MBELE ZA MUNGU.

⏺️ Je kati ya tabia hizi, wewe una ipi hapa ili upate kutubu leo???

1. Kuchati au kubofya bofya simu wakati wa Ibada Takatifu ikiendelea. Mawazo kuwa mbali na ibada, na kuja pale tu kupoteza muda na kuwafanya wengine mawazo yao yatoke
➖ Hii inaonyesha kwamba, unajali sana simu kuliko kile kinachoendelea Kanisani. Na inaonyesha MUNGU siyo namba moja, humpendi sana na inabidi utubu

2. Kukataa kuketi, mahali ambako umeelekezwa na Wahudumu (Kamati ya Ibada) sehemu sahihi ya kukaa.
➖ Hii inaonyesha kwamba, ni jinsi gani ulivyomkaidi na hufuati utaratibu.

3. Upo Kanisani wakati wa Ibada Takatifu ikiendelea, ghalfa simu yako inaita kwa sauti ya juu, unatoka nje haraka kwenda kuipokea.
➖ Hii inaonyesha kwamba, huna utii kabisa kwa Muumba wako.

4. Kuchelewa kuingia Ibadani kila siku kwa makusudi.
➖ Hii inaonyesha kwamba, Mungu sio kipaumbele cha kwanza kwenye maisha yako.

5. Kusinzia, kunong'onezana au kupiga story za chini kwa chini wakati wa Ibada Takatifu ikiendelea.
➖ Hii inaonyesha kwamba, wewe una dharau na hutaki kusikia Neno la Mungu.

6. Kukaa chini muda wote bila sababu za msingi, huku wenzako wakiwa wamesimama au kupiga magoti. MUNGU anaheshimiwa, ungepiga magoti kwa Raisi au mtu mkubwa
➖ Hii inaonyesha kwamba, wewe ni Mjuaji sana na huna maadili kwa Waongoza ibada.

7. Kuangalia saa ya ukutani au ya mkononi kila wakati huku mahubiri yakiwa yanaendelea, kama njia ya kujua leo mahubiri yamechukua muda gani kuisha. Usitimize wajibu wa kuwa kanisani
➖ Hii inaonyesha kwamba, Neno la Mungu sio sehemu ya maisha yako na huna muda wa kuisoma wala kuitafakari.

8. Kutoshiriki kikamilifu kwenye huduma mbalimbali zinazofanyika Kanisani. Mfano wenzako wanaimba, wewe unatazama huku na kule kuangalia nani aliyependeza leo Kanisani.
➖ Hii inaonyesha kwamba, hukuja Kanisani kwa lengo la kusali, bali kwa lengo la kujionyesha tu ili watu wajue kuwa wewe ni nani.

9. Kuondoka mapema Ibadani kabla haijaisha.
➖ Hii inaonyesha kwamba, unajali sana mambo yako kuliko ya Mungu.

10. Kukusanyika nje ya Kanisa huku Ibada Takatifu ikiendelea. na mna vigenge vyenu nje, na mambo ni ya dunia tupu, kweli tunamdanganya nani. Anania na SAfira walifanya uongo ndani na nyumba ila MUNGU alijua
➖ Hii inaonyesha kwamba, wale walioko Kanisani ni wajinga sana kuliko wewe uliyeko nje.

⏺️ BASI KAMA UNA TABIA MOJAWAPO KATIKA YA HIZI, NAOMBA UBADILIKE SASA. MAANA MUNGU HUWAPIGA WENYE KIBURI, NA KUWAPA NEEMA WANYENYEKEVU. (1PETRO 5:5-6)
 
SABATO NJEMA

Comments