KWA WASOMAJI WA BIBLIA HEBU TUITAZAME AMRI/SHERIA YA MUNGU KWA MAPANA.
(Sehemu ya I)
Utangulizi:
Kanuni kuu za sheria ya Mungu zimeunganishwa katika Amri Kumi na zilifuatishwa katika maisha ya Kristo. Nazo zinadhihirisha upendo na mapenzi ya Mungu, na makusudi yake kuhusu mwenendo wa binadamu na mahusiano, nazo ni sharti kwa watu wote katika kila kizazi.
Amri hizi ni msingi wa agano la Mungu na watu na kanuni katika hukumu ya Mungu. Kupitia utendaji wa Roho Mtakatifu zinadhihirisha dhambi na kuamsha haja ya kumpata Mwokozi. Wokovu ni kwa neema, na si kwa matendo, lakini matunda yake ni utii kwa Amri Kumi.
Utii huu hukuza tabia ya Kikristo na huwa na matokeo ya ustawi. Ni ushuhuda wa upendo wetu kwa Bwana na wajibu wetu kwa wanadamu wenzetu.
Utii wa imani hudhihirisha uwezo wa Kikristo katika kubadilisha maisha, na hivyo kuimarisha ushuhuda wa Kikristo.
Rejea: (Kut. 20:1-17; Zab. 40:7,8, Mat. 22:36-40, Kumb. 28:1-14; Mat. 5:17-20; Ebr.8:8-10; Yoh. 15:7-10; Efe. 2:8-10; 1Yoh.5:3; Rum. 8: 3, 4; Zab. 19:7-14).”
Makusudi ya Sheria
Mungu alitoa sheria yake kwa watu ili kuwajaza mibaraka tele na kuwaongoza wapate kuingia kwenye mahusiano naye yenye kuokoa.
Madhumuni maalumu ya sheria ni:-
1. Hufunua mapenzi ya Mungu kwa Wanadamu
Kama maelezo ya tabia ya Mungu na mapenzi yake kwa wanadamu, sheria hudhihirisha nia yake na makusudi yake kwa wanadamu. Hudai utii mkamilifu, atakayetii yote akakosea juu ya moja, anakuwa amekosea juu ya yote (Yak. 2:10). Utii wa sheria kama kanuni ya maisha ni muhimu kwa wokovu wetu, Kristo mwenyewe alisema “kama ukitaka kuingia mbinguni, zishike amri” (Mt. 19:17). Utii unawezekana tu kwa uwezo wa Roho wa Mungu.
2. Ni msingi wa Agano la Mungu
Musa alipoandika Sheria na maelezo mengine, aliita Kitabu cha Agano (Kut. 20:1-24:8).
Baadaye aliziita Amri Kumi Mbao za Agano (Kumb. 9:9-. 4:13)
3. Ni kipimo cha Hukumu
Kama ilivyo tabia yake, Sheria ya Mungu nayo ni haki (Zab. 119:172). Kila moja wetu atahuAtendayewa sheria (Mh. 12:13,14. Yak. 2:12). Dhamiri za wanadamu hutofautiana. Zingine ni nyonge, na zingine zimenajisiwa, ovu au zimeunguzwa na pasi ya moto (1Kor. 7,12: Tit. 1:15; Ebr. 10:22; 1Tim. 4:2). Dhamiri zetu hutuambia tutende haki, lakini hazituambii haki yenyewe ni ipi. Hivyo sheria ndiyo kipimo cha hukumu.
4. Huonesha Dhambi
Bila Amri kumi, watu hawawezi kuuona utakatifu wa Mungu, hatia yao na hitaji la kutubu. Sheria ni kama kioo (Yak. 1:23-25) na wanaoitazama huona kasoro za tabia zao na kuona tunavyowajibika kwa Mungu (Rum. 3:19). Sheria hutufanya tuitambue dhambi (Rum. 3:20) kwa sababu dhambi ni uasi (1Yoh 3:4). Kama sheria isingekuwapo, tusingejua dhambi (Rum. 7:7).
5. Hutuongoza kuongoka
Sheria ya Mungu ni zana cha Roho Mtakatifu kutuongoza kutubu. Sheria ya Mungu ni kamilifu, huuburudisha moyo (Zab. 19:7). Sheria ni kiongozi kutuleta kwa Kristo ili tuhesabiwe haki (Gal. 3:24). Kama kioo kisivyoweza kuondoa uchafu, sheria hutufanya tuhitaji chemchemi iliyofunguliwa (Zek. 13:1) na kusafishwa na damu ya Mwana Kondoo (Uf 7:14).
6. Hutupatia Uhuru wa Kweli
Atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi (Yoh. 8:34). Nitakwenda panapo nafasi, kwa sababu nimejifunza kutii (Zab. 119:45). Yakobo aliita Sheria ya Mungu Sheria ya Kifalme, sheria ya Uhuru (Yak. 2:8; 1:25). Yesu anapotualika, hutuita kuchukua mzigo mwepesi na nira laini (Mt. 11:28, 29) na hiyo hutupa raha. Palipo na Roho wa Mungu, kuna uhuru (2 Kor. 3:17).
7. Hukinga maovu na huleta Baraka
Kuongezeka makosa ya jinai, udhalimu, kukosekana uadilifu, na kuongezeka uovu ambako kumeijaa dunia kwa sasa kunatokana na kudharau Amri Kumi.
Wakati sheria hii inapokubaliwa, hukinga dhambi, hukuza matendo mema na huwa njia ya kuimarisha haki.
Haki huinua taifa (Mith. 14:34; 16:12). Wale wanaokataa kutii Amri za Mungu hawawezi kuikwepa laana (Mith. 3:33; Kumb. 26; Kumb. 28). Kanuni hizi zina matokeo hata katika wakati wetu sasa.
Barikiwa!
Itaendelea sehemu ya pili..

Amen
ReplyDelete