NJAA KALI YA KUKOSA MANENO YA BWANA

*NJAA KALI YAKUKOSA KUYASIKIA MANENO YA BWANA YENYE KUKEMEA DHAMBI NDANI YA KANISA. (#njaa #imo #kanisani)

Amosi 8:11-12

*[11]Angalia, siku zinakuja, asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta njaa katika nchi; si njaa ya kukosa chakula, wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya BWANA.*

[12]Nao watatanga-tanga toka bahari hata bahari; na toka upande wa kaskazi hata upande wa mashariki; watapiga mbio, wakienda huko na huko, kulitafuta neno la BWANA, wasilione.

_*Hii njaa ni njaa ya kukosa kusikia maneno ya Bwana, yaani maneno ambayo yangewaeleza watu dhambi yao yatakuwa hayapo²* _²E.G. White, The Great Controversy, PPPA, 1911, uk, 234,235._

_*Biblia ipo  lakini ujumbe ule ambao ungewaonya watu utatoweka,* *hautakuwepo tena. Vitabu na mahubiri yatakuwa ya kawaida tu, ambayo hayawezi kumwamsha mtu. Yatakuwa ni mahubiri ambayo hayataji dhambi ya mtu.* *Mengine ni yale ya kumfanya mtu ajisikie kwamba si mdhambi,* *hata awe mwovu kiasi gani,* kama vile inavyosema, ile sura ya Yer. 8:11,"

[11]Kwa maana wameiponya jeraha ya binti ya watu wangu kwa juu-juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani."

Yaani itakuwa ujumbe wa amani tu.³*_* ³The Great Controversy, PPPA, 1911, uk, 234,235.*_

*Vitabu navyo vitaandika habari za upendo tu, na mambo ya ndoa, pamoja na namna ya kuishi. Kwa hyo ni njaa ya neno la Mungu. Hapatakuwa na neno la kuyaamsha makanisa. Yatashambuliwa na mambo ya starehe, kufurahi furahi, kuchezacheza, sherehe, kushangilia, kupiga makofi, hicho tu ndicho kitakachobaki. Lakini lile neno la kumfanya mtu aogope, lenye kumwonya, halipo tena. Wakati njaa hiyo ya Neno la kiroho inapokuja, watu duniani watasahau kuwa kuna vita kati ya wema na uovu vinaendelea.⁴*_⁴The American Catholic Quarterly Review, January, 1883, uk. 152, 139._

_*Wale ambao watahubiri Neno la Mungu la KUWAONYA WATU na kuwarudisha kwa Yesu wataonekana kwamba ni maadui katika makanisa mbalimbali. Wataanza kuonekana ni watu hatari, na watu wasiokuwa na  upendo.⁵*_ _⁵Arno Gaeleelien, Conflic of Ages, The Exporters,  p. 85._

*Watatafutiwa makosa, hawatatakiwa na makanisa yao. Nayo YATAWASHITAKI wainjilisti, wachungaji, na wahubiri hao. Wataonekana ni watu wenye VITUKO, na WATATENGENEZEWA MASHTAKA kwa sababu ya UJUMBE WAO. Ni ujumbe wa MAONYO. Watasemwa kuwa hawana upendo kwa washiriki, au wana mafundisho mageni au WANALIGAWA KANISA, tena licha ya KULIGAWA KANISA, ni watu ambao wakati mwingine hawana akili nzuri (TIMAMU).⁶*_⁶Conflic of Ages, The Exporters,  p. 85._

_*Ellen G White alioneshwa pia kazi ya kuionya dunia ITAKUWA NGUMU kwa sababu "MALAIKA WAOVU KATIKA SURA YA WANADAMU WAUMINI WATAKALIA VITI VYA UONGOZI MAKANISANI". Halafu sheria itatungwa kuhakikisha kuwa WAHUBIRI WAAMINIFU Kwa Mungu wao WASIPEWE RUHUSA YA KUZUNGUKA makanisani wakihubiri, maana watahitaji VIBALI kupitia ngazi nyingi ambazo hazitawapatia nafasi hiyo, kwani UJUMBE wao hauhitajiki na malaika wa giza. Wakati mwingine #BIMA flani itawekwa ili kupunguza mizunguko ya wahubiri. Wakati malaika waovu hao katika SURA YA WATAKATIFU wakizuia mahubiri yasienee, hasa KUKOMESHA fundisho la KUWAITA WATU WATOKE BABELI, "Mungu atatumia watu wake waifanye kazi kwa njia ambazo SI ZA KAWAIDA, ambazo kanisa HAWAJAZIZOEA", Namna ambayo ni kinyume na SHERIA ZA HILA zinazotungwa kwa SIRI.⁷*_ _⁷Ellen G White, Selected Messages, Volume 3, Mountain View, PPPH, 1911, uk. 412., Last Day Events, uk. 203._

Lakini bado wahubiri wanaagizwa na Yesu katika kile kitabu cha  Matendo ya Mitume 1:8
*"[8]Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi." Ninyi nanyi mtapokea nguvu. Ujumbe utaanzia Yerusalemu (MAKANISA YA NYUMBANI), Uyahudi, Samaria, hata mwisho wa nchi.⁸*_⁸Bill Hughes, The Secret Terrorists Tangerine Triumphant Truth, 2000._

*Shetani anatumia pesa. Uwezo wa Joka ni pesa. Shina la mambo yote ni kupenda pesa. Lakini watakatifu nguvu yao ni Roho Mtakatifu. Sasa ni kipi cha kuombea kila siku? Ni PESA AU ROHO MTAKATIFU?⁹* _⁹Burke McCarty, The supressed Truth About the Assassination of Abraham Lincoln,  Arya Varta Publishing, 1924  uk.7.

LEO hali imebadilika makanisani huko, hali ya neno la MUNGU litetemeshalo moyo halimo vinywani mwa wanaojiita wahubiri wa mimbarani. Mahubiri ni mepesi sana kama ya kilokole na wakatoliki, ni kusimuliana hadithi na vichekesho mimbarani. Mioyo ya wana na binti za MUNGU bado haiguswi na injili hizi laini, na kila SABATO roho nyingi hurudi majumbani zikiwa na #NJAA YA #NENO LA #MUNGU .

Kama mjumbe wa MUNGU asemavyo, sheria zimewekwa katika baadhi ya makanisa ya kiadventista, MJUMBE mwenye UJUMBE wa karipio kali kutoka kwa BWANA hakikisheni asipewe nafasi ya kuhubiri. Jambo hili linamfurahisha Shetani na wafuasi wake, lakini linamuumiza YESU moyoni.

Hata kwenye vyombo vyetu vya habari tunavyovichangia sadaka kila sabato, masharti ya hovyohovyo yamewekwa dhidi ya wahubiri wenye ujumbe wenye karipio kali ili washindwe kufanya kazi ya utume. Tv zetu na radio zetu zinamilikiwa na watu wasiowaongofu na wasiojuwa masaa tuliyobakiwa nayo ili rehema ifungwe kwa waadventista wasabato. Ukitaka kuhubiri katika vyombo hivi na pia katika mikutano ya hadhara lazima urekodiwe kwanza na hawa wajanjawajanja, kisha wayakate maneno yenye ujumbe mkali, wayachuje, yawe mepesi kama ya kilokole na kikatoliki na ndipo yarushwe kwenye radio zetu au Tv zetu.

Ni wakati wa njaa kali ya neno la MUNGU ambao waumini wa kanisa tunapitia. Maneno haya ni ya kweli. Neno la MUNGU linazidi kututoka katika kumbukumbu zetu na tunabakia na ngonjera za kuishi kwa upendo na amani.

Rafiki zangu wasomaji, hii ni hatari kwani hata huko nje shetani ameweka vizuizi kwenye vyombo vya habari, hataki ujumbe wa karipio uhubiriwe kwani anajuwa kuwa watu wake aliowashikilia katika madanganyo watamkimbia. Hata mahubiri ya hadhara ,kuna ujumbe mwepesi mwepesi tu na ikiwa mhubiri ana ujumbe wa kuogofya, yumkini atasimamishwa asiendelee kuhubiri, atafungishwa virago aondoke. Huko ndiko watunza sabato tumefikia jamani.

Siku moja mimi na rafiki yangu tulienda kuhubiri kupitia radio moja hapa nchini,  tulikuwa na ujumbe wenye ujumbe. Rafiki yangu akiwa ni mhubiri na mimi nilikuwa msomaji wa maandiko ya BIBLIA . Siku hiyo tulikuwa tukishughulika na ufunuo sura ya 17 na 18 na pia kitabu cha daniel sura ya 7. Mpendwa msomaji, shetani amekaba kila kona, ujumbe ule ulikuwa ni mzito wa kuogopesha katika masikio ya wanahabari, hadi ilifikia hatua wakubwa wao waliwaamuru kuzima mitambo ya redio, sijui upande wa wasikilizaji huko nje ilikuwaje. Baada ya kuzima radio walituamuru kuondoka na wakatuambia tusiende tena hpo kwani watatafuta wainjilisti wengine๐Ÿ˜…

Rafiki msomaji, sijui kama mnanielewa๐Ÿค” namaanisha hivi, ikiwa watunza sabato ya BWANA tungeupeleka ujumbe wa malaika watatu pasipo woga wala kuzuiana makanisani huko, tungelikuwa tumeupindua ulimwengu juu chini na YESU angerudi mapema.

Rafiki yangu mmoja kutoka arusha aliitwa kwenda kuendesha mahubiri ya hadhara kanisa flani hpa Tanzania . Aliendesha hayo mahubiri na alipofika katikati ya zile wiki na kuanza kuuhubiri ujumbe wa malaika watatu pamoja na ujumbe wa afya, ghafla Mchungaji na wazee wa kanisa wa mtaa huo walimpiga STOP! Sababu! Kwanini unahubiri ujumbe mkali wa kutugawanya??? Haya tunakuamuru uondoke! Rafiki yangu huyo aliondoka maana hakukubaliana nao katika jumbe laini laini.

Watu katika mtaa huo walibaki na njaa๐Ÿค”

Saa yaja njaa ya neno la BWANA lenye kuonya itaenea kila nyumba ya muumini na kila kanisa na hatimaye duniani kote kwa Wanadamu . Watu watalitafuta neno hili zuri lakini halitakuwepo kabisa maana ni wakati wa kunyamaza.

Kipindi cha kuhani eli neno la BWANA lilikuwa adimu katika israeli, watu walifanya waonavyo vyema machoni pao. 1samweli 3:1

Hata sasa waadventista Wasabato hatuzioni ishara, wala hakuna nabii kama kipindi kile cha israeli katika uasi, ndivyo tulivyo leo kanisa, tunazidi kurudi nyuma. Zaburi 74:9

Madhara yatakuja juu ya madhara, na habari ya shari juu ya habari ya shari, nao watakwenda kwa nabii kutaka maono, lakini hiyo sheria itampotea kuhani, na mashauri yatawapotea wazee๐Ÿค”

Endeleeni kuchapa usingizi na kuikataa sheria ya BWANA na maonyo makali hamyataki, mda utafika na roho zenu zitatamani kuyasikia mashauri ya BWANA , mtawatafuta wale waliosema ukweli bila kuwaficha, lakini hawatakumbuka lolote, kwani ni wakati wa kunyamaza kabisa. Ezekieli 7:26

๐Ÿ‘‰๐ŸปKwa hiyo itakuwa usiku kwenu, msipate kuona maono, tena itakuwa giza kwenu, msiweze kubashiri, nalo jua litawachwea manabii, nao mchana utakuwa mweusi juu yao, Na hao waonaji watatahayarika, na wenye kubashiri watafadhaika, naam hao wote watajifunika MIDOMO YAO , kwa maana hapana jawabu la MUNGU ๐Ÿค”. Mika 3:6-7

Wahubiri wote mnaompenda BWANA na kupenda kuja kwake haraka, lihubirini lile Neno bila kuogopa vikwazo. Ushirika wako wa kanisa siyo DHAMANA YA WOKOVU.

Hali ya mahubiri ya kila sabato na mikutano mikubwa ya injili hairidhishi mbele za BWANA aliyetutuma, ubaridi na hofu ya vikwazo na kunyimwa mishahara imetawala ndani ya mioyo ya wachungaji na wainjilisti . Uoga umetawala kwa waumini wakihofia kutengwa na makanisa yao mahalia, hata wakikutenga na kufuta ushirika wako kwenye kitabu cha kanisa kwasababu za kusema kweli ya MUNGU bila kuogopa, jina lako mbinguni limetunzwa vizuri katika kitabu cha uzima. TUAMKE TUFANYE KAZI TWENDE MBINGUNI, MDA UMEISHA. Hebu Gaweni vitabu vya PAMBANO KUU , tawanyeni hivi vitabu kama majani maana vitafanya kazi ile ambayo mmezuiliwa kuifanya.

Sema neno hili moyoni mwako: BALI MIMI HAKIKA NIMEJAA NGUVU KWA ROHO YA BWANA , NIMEJAA HUKUMU NA UWEZO , NIMUHUBIRI YAKOBO KOSA LAKE, NA ISRAELI DHAMBI YAKE.

Mungu atusaidie kweli, maana sasa ugonjwa wa kwashakoo ya kukosa neno la BWANA unazidi kuambukiza mtu hadi mtu, kanisa hadi kanisa na hii kwashakoo itawakaba hadi mataifa wote/yote.

Baba yetu wa MBINGUNI , utukumbuke, tunakuomba kwa rehema zako na subira yako, utuepushe na injili danganyifu! Katika Jina la YESU !

                    Amina!๐Ÿ™๐Ÿป

Comments