Ndoto ya Mfalme. Danieli 2
Danieli 2:1 “Hata katika mwaka wa pili wa kumiliki kwake Nebukadreza, Nebukadreza aliota ndoto; na roho yake ikafadhaika, usingizi wake ukamwacha.”
Katika mwaka wa 604 K.K. kulikuwa na mfalme aliyetawala juu ya ufalme wote wa babeli, mfalme huyu jina lake aliitwa Nebukadreza. Tena mfalme huyu, alikuwa amehusuru miji mipya mingi ikiwemo na Yerusalemu, ambapo aliwachukua mateka Wayahudi wengi akiwemo na nabii Danieli.
Siku moja usiku mfalme huyo aliota ndoto ya kusisimua sana, na alipoamka alikuwa ameisahau ndoto ile, Hivyo akatamani sana kujua ilikuwa ndoto gani.
Danieli 2:2 “Ndipo mfalme akatoa Amri kuwaita waganga, na wachawi, na wasihiri, na Wakaldayo, wapate kumweleza mfalme ndoto zake. Basi wakaingia, wakasimama mbele za mfalme.”
Kitu kigeni hapa ni kwamba, mfalme alitaka kujua tafsiri pamoja na ndoto yote aliyoiona usiku; yaani kila kitu alichokiona katika ile ndoto. hii iliwafanya waganga na wachawi wapigwe bumbuazi; maana kwao ilikuwa haiwezekani kumjulisha ndoto ile pamoja na tafsiri yake, bila kuijua ndoto yenyewe kwanza.
Danieli 2:4 “Ndipo hao wakaldayo wakamwambia mfalme, kwa lugha ya kiaramu, Ee mfalme, uishi milele; tuambie sisi watumishi wako ile ndoto, nasi tutakuonyesha tafsiri yake.”
Waliposhidwa kumwelezea mfalme ile ndoto, ndipo mfalme akagundua kwamba, hawa waganga na wachawi, hawakuwa na uwezo wowote, bali walikuwepo kwa ajili ya pesa. Ndipo mfalme akasema:
Danieli 2:9 “Lakini msiponijulisha ile ndoto, iko amri moja tu iwapasayo; maana mmepatana kusema maneno ya uongo, na maneno maovu, mbele zangu, hata zamani zitakapobadilika; basi niambieni ile ndoto, nami nitajua ya kuwa mwaweza kunionyesha tafsiri yake.”
Waganga hawa pamoja na wachawi, walishindwa kueleza ile ndoto, hii ilifanya hasira ya mfalme izidi kuwaka juu yao.
Danieli 2:12 “Basi kwa hiyo mfalme akaghadhibika sana, akaona hasira nyingi, akatoa amri kuwaangamiza wenye hekima wote wa Babeli.”
Tatizo ni kwamba nabii Danieli alikuwa mmojawapo katika wale wenye hekima wa Babeli, hivyo amri hii ya kifo naye ilimuhusu, Kwa hiyo akawahi kwa mfalme kuomba rehema ili apewe muda kwa ajili ya ile ndoto, Danieli alitaka kumuuliza Mungu wa kweli amjalie kuifahamu ndoto ile ya mfalme.
Basi, Danieli alienda nyumbani kwake, akawaambia wenzake kina Hanania, na Mishaeli, na Azaria; ili waombe rehema kwa Mungu kwa ajili ya ile siri, ili nao pia wasiangamizwe pamoja na wenye hekima wa babeli.
Danieli 2:19 “Ndipo Danieli alipofunuliwa siri hiyo katika njozi ya usiku. Basi Danieli akamhimidi Mungu wa mbinguni.”
Danieli alibalikiwa kuota ndoto kama ile ile aliyoota mfalme, Danieli alimtukuza Mungu kwa kumfunulia siri kama hiyo, na kesho yake aliwahi kwa mfalme kwenda kumweleza ndoto ile, akasema:
Danieli 2:31-35 “Wewe, Ee mfalme, uliona, na tazama, sanamu kubwa sana, sanamu hii, iliyokuwa kubwa sana, na mwangaza wake mwingi sana, ilisimama mbele zako; na umbo lake lilikuwa lenye kutisha. Na sanamu hii kichwa chake kilikuwa ni cha dhahabu safi; kifua chake na mikono yake ni ya fedha; tumbo lake na viuno vyake ni vya shaba; miguu yake ni ya chuma; na nyayo za miguu yake nusu ya chuma na nusu ya udongo. Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande. Ndipo kile chuma, na ule udongo, na ile shaba, na ile fedha, na ile dhahabu, vilivujwa vipande vipande pamoja vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa hali; upepo ukavipeperusha hata pasionekane mahali pake; na lile jiwe lililoipiga hiyo sanamu likawa milima mikubwa, likaijaza dunia yote.”
1. Kichwa cha dhahabu2. Kifua na mikono ya
fedha3.Tumbo na viuno vya
shaba4. Miguu ya chuma5. Nyayo za miguu yake
nusu ya chuma nusu ya
udongo
Danieli alibarikiwa pia kujua tafsiri ya ndoto hiyo.
Danieli 2:36-38 “Hii ndiyo ile ndoto, nasi tutaihubiri tafsiri yake mbele ya mfalme. Wewe, Ee mfalme, u mfalme wa wafalme, na Mungu wa mbinguni amekupa ufalme, na uwezo, na nguvu, na utukufu; na kila mahali wakaapo wanadamu, wanyama wa kondeni na ndege wa angani amewatia mikononi mwako, naye amekumilikisha juu ya hao wote; wewe u kichwa kile cha dhahabu.”
Kama tulivyoona, kila sehemu ya sanamu hiyo aliyoota mfalme, inawakilisha UFALME, na wakwanza, kichwa cha dhahabu, ni ufalme wake wa Babeli, ambao ulitawala kutokea 606 K.K hadi 539 K.K.
Danieli 2:39 “Na baada ya zamani zako utainuka ufalme mwingine mdogo kuliko wewe…”
Baada ya ufalme wa Babeli kutawala miaka 67, babeli linyanganywa ufalme na “umedi na uajemi.” Ufalme wa umedi na uajemi ulitawala miaka 208, kutoka 539 K.K. hadi 331 K.K. Ufalme huu ndiyo uliwakilisha “kifua na mikono ya fedha” katika ile sanamu.
Danieli 2:39 “…na ufalme mwingine wa tatu utaitawala dunia yote.”
Historia inathibitisha kuwa, katika mwaka wa 331 K.K. majeshi ya Ugiriki yaliuvunja ufalme wa umedi na uajemi, ilikuwa ni wakati wa vita kali ya Arbela, Ugiriki ikaanza kutawala, na utawala wake ulichukua sehemu kubwa duniani. Na jina la mfalme wake aliitwa Alexander, Ufalme huu ulitawala takribani miaka 163, kutokea 331 K.K. hadi 168 K.K. Kwa hakika, ufalme huu ndiyo uliwakilisha “tumbo na viuno vya shaba” katika ile sanamu aliyoota mfalme.
Danieli 2:40 “Na ufalme wa nne utakuwa na nguvu mfano wa chuma; kwa maana chuma huvunja vitu vyote na kuvishinda; na kama chuma kisetavyo vitu hivi vyote, ndivyo utakavyovunja-vunja na kuseta.”
Mnamo mwaka 168 K.K. ufalme wa Rumi ulianza kutawala juu ya dunia, Ufalme huu katika ile sanamu umewakilishwa kama “miguu ya chuma” ikimaanisha kuwa, jeshi lake lina akili na nguvu nyingi, Ufalme huu wa rumi ulitawala dunia yote, nao uliisha mwaka 476 B.K.
Danieli 2:41 “Na kama vile ulivyoziona hizo nyayo za miguu na vidole vyake, kuwa nusu udongo wa mfinyanzi, na nusu chuma, ufalme ule utakuwa ufalme uliogawanyika; lakini ndani yake zitakuwako nguvu za chuma, kama vile ulivyoona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope.”
Je umeona Unabii huu, hausemi, kwamba kutakuwa na ufalme wa tano, badala yake unasema, “Ufalme huo wa nne utagawanyika?” Danieli 7:7 inathibitisha wazi kwamba, “ufalme huu wa nne (ufalme wa rumi) una mataifa kumi, (pembe kumi,) na Danieli 7:8, 24. zinasema, “katika hayo mataifa 10 (pembe 10) litatokea kanisa la roman katoliki (“pembe ndogo”) nalo litayang’oa mataifa 3 (pembe 3)
Ukweli wa historia ni kwamba, mataifa ya wababario yaliushamburia ufalme wa Rumi yakaushinda, Rumi iliposhindwa, ikanguka, iligawanyika katika mataifa 10 = pembe 10, na kanisa la roma = pembe ndogo, liliyaondoa mataifa 3 katika yale 10.
Sababu kuu ya kuyaondoa hayo mataifa 3 ni kwamba, mataifa 3 haya, hayakukubali mipango yote iliyopangwa na Upapa, hivyo kufikia 538 B.K. upapa ulikuwa umefanikisha kuyaondoa yote 3.
Baada ya ufalme wa Rumi kuanguka (476 B.K.) uligawanyika katika mataifa 10 (pembe 10) yafuatayo…
1. Saxon, kwa sasa ni
taifa la Uingereza.2. Frank, kwa sasa ni
taifa la Ufaransa.3. Alamanni, kwa sasa ni
taifa la Ujerumani.4. Visigoth, kwa sasa ni
taifa la Uhispania.5. Suevi, kwa sasa ni taifa
la Ureno.6. Lombard, kwa sasa ni
taifa la Italia.7. Burgundia, kwa sasa
ni taifa la Uswidi.8. Heruli, liling’olewa na
pembe ndogo 493 B.K.9. Vandal, liling’olewa na
pembe ndogo 534 B.K.10. Ostrogoth,
liling’olewa na pembe
ndogo 538 B.K.
Tukiangalia katika ndoto tunaona sehemu tano za sanamu…
Sehemu ya
SanamuUfalme1. Kichwa cha dhahabuUfalme wa Babeli
606K.K. – 539K.K.2. Kifua na mikono ya
fedhaUfalme wa
Umedi na Uajemi
539K.K – 331K.K.3. Tumbo na viuno vya
shabaUfalme wa
Ugiriki
331K.K – 168K.K.4. Miguu ya chumaUfalme wa Rumi
168K.K. – 476B.K.5. Vidole vya nyayo
za miguu, nusu chuma
na nusu udongoMataifa 10 ya
Umoja wa Ulaya [EU]
476B.K. mpaka leo.
Kumbuka: Umoja wa Ulaya sasa unaundwa na mataifa 7 tu, hii ni kwa sababu mataifa 3 yanayowakilishwa kama pembe 3 yaling’olewa!

Kulikuwa na wakati ambapo dola la Rumi lilitawala kama chuma pekee, na lilikuwa la kikatili na lenye nguvu nyingi mno. Lakini kama unabii unavyotabiri kwamba utawala ungehama kutoka “miguu ya chuma” hadi kuwa “vidole vya nyayo ambavyo nusu ni udongo na nusu ni chuma”; kama ukihesabu idadi ya vidole utapata 10, hii inamaanisha, katika hatua ya utawala wa nyayo za dola hilo la Rumi ungegawanyika katika wafalme au mataifa 10 ndani ya dola moja. Lakini pia ingekuwepo nguvu ya chuma pia ya kikatili na uuaji.
Danieli 2:42 “Na kama vidole vya zile nyayo vilikuwa nusu chuma na nusu udongo, kadhalika ufalme ule utakuwa nusu yake una nguvu, na nusu yake umevunjika.”
“Udongo” katika maandiko unawakilisha “mioyo ya wacha Mungu”; Kristo alisema: “Naye aliyepandwa penye udongo mzuri, huyo ndiye alisikiaye lile neno, na kuelewa nalo; yeye ndiye azaaye matunda, huyu mia, na huyu sitini, na huyu thelathini.” (Mathayo 13:23). Mvua huwakilisha Roho Mtakatifu (Yoeli 2:23,28), na wakati mvua inaponyesha juu ya udongo au nchi inawakilisha Roho Mtakatifu kuja ndani ya moyo (Hosea 6:3). Hivyo ufalme huo kugawanyika katika mataifa 10, ambayo nusu ni udongo na nusu ni chuma, inawakilisha kwamba baadhi ya mataifa yangekuwa moyo wa kumcha Mungu, wakati mengine hapana. “Chuma” kama ilivyofafanuliwa na Danieli mwenyewe inawakilisha ukatili, au uuaji.

Danieli 7:7 “Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.”
Danieli 7:19 “Kisha nalitaka kujua maana ya yule mnyama wa nne, aliyekuwa mbali na wenziwe wote, mwenye kutisha sana, ambaye meno yake yalikuwa ya chuma, na makucha yake ya shaba; aliyekula, na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake;”
Hivyo “chuma” katika unabii inamaanisha kuwa na ujasili ukatili na nguvu nyingi za kukanyaga na kuvunjavunja na kuharibu bila kuogopa, hasa katika vita. Na hii ingemaanisha nusu ambayo ni udongo wangekuwa ni watulivu na wasio na nguvu za kupigana vita, wakati ile nusu nyingine ambayo ni chuma wangekuwa ni wakatili na wenye nguvu nyingi mno na uwezo wa kupigana na kushinda vita.
Unabii huo ulikuwa ni ukweli asilimia mia; kwa maana baadhi ya mataifa miongoni mwa yale kumi katika ufalme huo uliogawanyika yalikuwa ya wacha Mungu na yalikuwa hayana nguvu za kushinda katika vita. Kwa mfano mataifa matatu ya Wakristo wa kiario, yanayowakilishwa kama pembe tatu zilizong’olewa za Danieli 7:8 yalikuwa hayana uwezo wa kushinda vita,, hivyo wakati yalipokataa kutii amri za kanisa Katoliki yalishambuliwa na mfumo wa Upapa na kuangamizwa kabisa mwaka 538bk, kila taifa jingine ambalo kama lingepinga kutii amri za Ukatoliki lisingepata nguvu, bali lingeangamizwa kabisa. Upapa uliwakilisha “chuma”, kwani ulikuwa na uwezo wa kuangamiza, kuharibu, na kuwavunjavunja wapinzani wake wote. Lakini kwa sababu wengine walikuwa watulivu au wapole na wengine wakatili, hiyo ndiyo sababu kuu ufalme huo ulishindwa kushikamana, bali ukabaki umegawanyika; maana udongo (utulivu) na chuma (ukatili) haviwezi kushikamana kamwe.
Danieli 2:43 “Na kama vile ulivyoona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope, watajichanganya nafisi zao kwa mbegu za wanadamu; lakini hawatashikamana, kama vile chuma kisivyoshikamana na udongo.”
Tafsiri ya ndoto hii inatuambia kwamba, mataifa yaliyotokea baada ya ufalme wa Rumi kuanguka, hata kama yakijaribu kiasi gani, hayataweza kuungana tena kuwa taifa moja; kwa sababu udongo na chuma haviwezi kushikamana. Japokuwa wengi wamejaribu kuifanya ulaya kuwa taifa moja na kuiweka chini ya kiongozi mmoja, kwa mfano, Louis XIV, Hitler, Napoleon, Charlemagne. hawa wamejaribu kufanya hivyo lakini walishindwa. Papa ndiye anatawala juu ya mataifa yote hayo na juu ya dunia nzima, lakini hata hivyo mataifa hayo bado yako chini ya wafalme wengi na sio mmoja peke yake. Lakini Ufunuo 17:18 inatuambia kwamba Upapa ni: “ufalme [unaotawala] juu ya wafalme wa nchi”. Kwamba Upapa unatawala juu ya wale wafalme wa ulaya na dunia nzima kwa ujumla.
Ufunuo 17:12 “Na zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi, ambao hawajapokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme muda wa saa moja pamoja na yule mnyama.”
Danieli 2:44 “Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.”
Katika siku hizi za hao wafalme wa Ulaya ambao wanatawala pamoja na Upapa katika mnyama huyo ambaye ni Roma, Mungu naye atasimamisha Ufalme wa milele ambao utazivunja hizo falme zao zote. Sasa hivi tunasubiri kuona mnyama wa pili ambaye ni Marekaniakimpa mamlaka yake mnyama wa kwanza ambaye ni Roma. Wakati Roma kupitia Upapa itakapopata nguvu kamili tena za kuvunja vunja kama “chuma”, ndipo Yesu anakuja katika siku hizo kuziangamiza falme zote na kuanzisha Ufalme wake wa milele. Unabii huu ulikuwa ni wa hakika na umetimia na leo tuko hatua ya mwisho ya utawala wa vidole kwenye nyayo za miguu.
Danieli 2:45 “Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lililochongwa mlimani bila kazi ya mikono, na ya kuwa lilivunja-vunja kile chuma, na ile shaba na ule udongo, na ile fedha, na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye; na ndoto hii ni ya hakika, tafsiri yake ni thabiti.”
Jiwe humwakilisha Bwana Yesu Kristo kama mafungu yafuatayo yanavyothibitisha.
Matendo 4:11 “Yeye aliye Jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limekuwa Jiwe kuu la pembeni.”
1 Wakorinto 10:4 “wote wakanywa kinywaji kile kile cha Roho; kwa maana waliunywea Mwamba wa Roho uliowafuata; na Mwamba ule ulikuwa ni Kristo.”
Waefeso 2:20 “Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni Jiwe kuu la pembeni.”
Mathayo 21:42, 44 “Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa Jiwe kuu la pembeni. . . Naye aangukaye juu ya Jiwe hilo atavunjika-vunjika; naye ye yote ambaye litamwangukia, litamsaga tikitiki.”
Jiwe hilo litaanguka juu ya ile sanamu na kuisaga saga tikitiki. Hivyo siku Yesu atakapokuja kila jicho litamwona, na mataifa yote na falme zote za dunia zitasagwa-sagwa na kuwa kama mavumbi; kwa maana imeandikwa pia:
Isaya 24:1, 3, 5, 6 “Tazama, BWANA ameifanya dunia kuwa tupu, aifanya ukiwa, aipindua, na kuwatawanya wakaao ndani yake. . . Dunia hii itafanywa tupu kabisa, na kuharibiwa kabisa, maana BWANA amenena neno hilo. . . Tena dunia imetiwa unajisi kwa watu waikaao; kwa maana wameziasi sheria, wameibadili amuri, wamelivunja agano la milele. Ndiyo sababu laana imeila dunia hii, na hao waikaao wameonekana kuwa na hatia, ndiyo sababu watu wanaoikaa dunia wameteketea, watu waliosalia wakawa wachache tu.”
Falme hizi za dunia zitaharibiwa kwa sababu zinadharau amri za Mungu na kuti amri za wanadamu hivyo kusababisha laana juu ya dunia. Wachache tu ndio watasalia na kuokolewa, na kulingana na Biblia watakao okolewa ni wale tu wanaotii amri za Mungu kikamilifu, hao pekee ndio watakao salia wasiharibiwe.
Ufunuo 12:17 “WALIOSALIA, wazishikao amri za MUNGU, na kuwa na ushuhuda wa YESU”
Ufunuo 14:12 “watakatifu, hao wazishikao amuri za Mungu, na imani ya Yesu.”
Ni hatari kupuuzia amri za Mungu; kwani Mungu naye atakupuuzia na kukusaga saga siku ya mwisho.
Hosea 4:6 “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa MAARIFA; kwakuwa wewe umeyakataa MAARIFA, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeishau SHERIA ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.”
Kama unataka kukimbia hukumu na kupata uzima kama Yesu alivyosema unapaswa kumwamini yeye na kutii amri za Baba yake, hakuna njia nyingine ya kukwepa hayo.
Mathayo 19:17 “ukitaka kuingia katika uzima [wa milele] zishike AMRI.”

Comments
Post a Comment