NANI ANAYEABUDU SIKU?

NANI ANAYEABUDU SIKU?

Mnaosema Waadventista Wasabato wanaabudu siku kwa kupumzika na Kufanya ibada siku ya sabato.

#Swali: siku ya Jumapili ambayo mamilioni ya Waumini mnakusanyika Kufanya ibada, je hiyo Jumapili mnayokusanyika sio siku, na je hamkusanyiki kwa ajili ya Kuabudu au kufanya kazi,?

Kama hamuabudu siku inakuwaje miaka yote mng'ang'anie jumapili tu ,  kwanini isiwe jumatatu, jumanne, jumatano, Alhamisi au Ijumaa?

Ni Nini kilichojificha nyuma ya jumapili, ?????

Kwa sababu Kama siku zote ni sawa mbona hatuwaoni siku nyingine mkiwa mmevaa suti na kwenda makanisani Asubuhi, inakuwaje mpaka ifike jumapili tu.? Je huko sio kuabudu Siku?

#Swali: Ni kwamba Kati ya Waadventista Wasabato na madhehebu ya Jumapili ni wakina Nani wanaabudu siku?

Sisi Waadventista Wasabato tumeagizwa na Mungu kwamba ibada ni siku ya sabato: Ezekieli 46:3
Watu wa nchi nao #wataabudu mbele ya mlango wa lile lango mbele za BWANA, siku za sabato, na siku za mwezi mpya.

Mitume nao waliabudu siku ya sabato: Matendo ya Mitume 16:13
Hata siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa #kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale.

Kwa hiyo sisi hatuiabudu siku Bali tunamuabudu Mungu wa Mbinguni katika siku ambayo Mungu mwenyewe katuagiza na sio Mwanadamu. Kutoka 20:8,9
Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;

#Swali: Wewe unaabudu Jumapili kwa idhini ya Nani ? Ya Mungu au Mwanadamu?
HISTORIA YA KANISA VIPINDI VYAKE SABA uk 24 inasema

"Mwaka 313 Kaisaria Konstantino hakukawia kutangaza uhuru wa kanisa kwa
"Tangazo la  Milano". Basi, wakristu walipata uhuru uleule wa dini kama wapagani. Walirudishiwa makanisa na mali waliyokuwa wamenyimwa wakati wa udhalimu. Kaisaria alitangaza pia Jumapili iadhimishwe kama "Siku ya Bwana", na watu waukumbuke Ufufuko wa Kristu wala wasifanye kazi".

Je Kostantino ni Mungu au Mwanadamu? Je ni bora kumtii Mungu au Kostantino?
Matendo ya Mitume 5:29
Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.

Na Yesu anasema katika Mathayo 15:9
Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.

Kwa hiyo Wanaoabudu siku ya sabato wanafuata maagizo ya Mungu na wanaoabudu jumapili ni kwa mujibu wa mapokeo(maagizo) ya Kostantino ambaye ni Mwanadamu

Hivyo Basi anayeabudu siku ni yule anayeitumikia na Kufanya ibada katika siku iliyo kinyume na maagizo ya Mungu.

Mungu akubariki

Comments