NAMNA YA KUSHIKA SABATO.

LEO UTAJUA NAMNA YA KUSHIKA SABATO.
Posted by Isack Mussa

Tenda vile Yesu Kristo alivyotenda siku ya sabato yaan kutenda mema siku ya sabato ni ruhusa.

1. Siku ya sabato Yesu Kristo aliponya wagonjwa, hapa dakitari usiache kwenda kuponya roho hospital kisa sabato, au polisi usiache kwenda kutuliza ghasia mahali fulan kisa sabato. Au fundi umeme imetokea moto uliosababishwa na nyanya au nguzo za umeme kuanguka au hatari yoyote inayoweza kusababisha kifo Cha watu inakupasa uende Mara moja kuokoa roho za watu, usiache kuenda kisa sabato au una gari lako au pikipiki na ametokea mgonjwa anataka kwenda hospital mpeleke hata Kama ni siku ya sabato. Yaan kuna kazi za kuponya roho zinaweza kujitokeza siku ya sabato hivyo usiache kwenda kutenda hizo kazi NENDA.

Mh: Usitende kazi zako Binafsi zisizo na utukufu kwa Mungu siku ya sabato maana ndo kuvunja Amri uko, mfano kwenda kupiga debe, kuuza dukan, kwenda shule au kufanya mtihan, kwenda shamba nk nk na kazi zingine zinazofanana na hizo.

2. Siku ya sabato Yesu Kristo alivunja masuke na kula, hapa tunajifunza swala la kula au kupika chakula halina unajisi wowote siku ya sabato, mfano huna chombo Cha kutunzia chakula na una watoto je utawalisha kiporo waugue? Au ww unawezaje kula kiporo ili hali moto upo?? Haya, Kuna watu ijumaa hawapati chakula na imetokea jmos wamesaidiwa pesa ya chakula je wasipike chakula au wasinunue chakula? Amekuja mgeni siku ya sabato kwako je, atashinda njaa?? Au mnasabato ya wageni na hamna vyombo vya kutunzia vyakula je siku ya sabato msipike wageni washinde njaa?? HAPANA. Katika mazingira hayo kula hotelin au kupika chakula siku ya sabato sio dhambi.

Mh. Ukiwa na chombo Cha kutunzia chakula, andaa chakula ijumaa Kisha tunza kwa ajiri ya sabato ili siku hiyo uwe na pumnziko kubwa la kimwili na kiroho pia.

3. Kupanda gari au boda boda siku ya sabato sio dhambi. Mfano ww ni mchungaji unahitajika ukatoe huduma sehem ya mbali kidogo na taarifa hiyo umeipokea jmos asubuhi je utaacha kutoa nauli au kuendesha gari ili ufike uko?? Haya, kwaya imeitwa kwenda kuimba siku ya sabato sehem ya mbali kidogo je itembee kwa miguu? (Japo kiyahudi hata kutembea ilikua hairuhusiwi siku ya sabato) je Yesu hakutembea siku ya sabato?? Jibu ni hapana.

Mwisho, SABATO SIO MZIGO. SABATO ILIFANYIKA KWA AJIRI YETU NA SIO SISI KWAAJIRI YA SABATO. AMRI YA SABATO IKO PALE PALE LAKINI YESU KRISTO ALIKUJA KUFUNDISHA NAMNA YA KUITAKASA SABATO.

Tenda Yale Yesu Kristo alitenda siku ya sabato ✅

Amina.

Comments