NAMBA_666 NI KITU_GANI?

NAMBA_666 NI KITU_GANI?

Posted Isack Mussa

Suala la namba 666 limekuwa ni gumzo kwa watu wengi na kila mtu anajaribu kutoa tafsiri yake kwa jinsi anavyojisikia kulingana na mtizamo wake. Baadhi ya watu wamekuwa na mtizamo wa kudhani kwamba namba 666 ni hakika kwamba watu watapigwa kweli chapa katika paji la uso na itaonekana kwa macho.

Lakini wengine wamekuwa wakidai namba 666 ni Computer, wengine wamedai namba 666 ni Bacod zinazotumika katika biashara, Wengine Wamekuwa wakidai namba 666 ni ugonjwa wa Corona, wengine wanasema namba 666 ni Mfalme Nero na wengine wamekuwa wakidai namba 666 ni jina la ELLEN G WHITE.

Hizo ni baadhi tu ya tafsiri kuhusu namba 666, lakini zipo tafsiri nyingi sana, na hii inaonesha kwamba hoja ya namba 666 ni mtambuka kwa watu wengi na shetani anajitahidi kuvumbua tafsiri nyingi sana ili watu wasijue ukweli halisi. Lakini kuwa na Tafsiri nyingi hivi ni dhahiri pia kwamba watu hatusomi maandiko matakatifu bali wengi tunabuni tu.

Katika Biblia fungu linalotaja namba 666 katika mtizamo wa siku za mwisho ni fungu moja tu, ijapokuwa yapo mafungu mengine yanayotaja namba 666 lakini yakiwa na maana nyingine tu, katika Ufunuo wa Yohana 13:18 Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.

Sasa ili uweze kupata maana au mtizamo halisi juu ya namba 666 ni lazima urudi nyuma kidogo kuanzia fungu la 15, ambapo Ufunuo 13:11-18 inazungumzia juu ya ufalme au mamlaka ya kisiasa itakayolazimisha ulimwengu kumfanyia mnyama sanamu, na hii sanamu itabidi iabudiwe kwa lazima na wakazi wote wa Dunia:  Ufunuo wa Yohana 13:15 Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe.
#Note: Kuna mnyama na kuna sanamu ya mnyama, na hii sanamu ya Mnyama ndio inabidi ISUJUDIWE, na wale wote watakaokataa kuisujudia hii sanamu ndio itabidi Wauawe:  #MNYAMA ni ufalme au mamlaka ya Kidini itakayotawala Dunia katika nyakati hizi za mwisho: Danieli 7:23 Akanena hivi, Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia, utakaokuwa mbali na falme zile zote, nao utakula dunia yote, na kuikanyaga, na kuivunja vipande vipande.

Na huu mfumo wa Kidini utaunda  ibada bandia kinyume na Ibada ya Mungu na kuwataka watu wote Duniani wasujudu au Kufanya ibada katika hii sanamu. Sasa sanamu ni mfano wa kitu ambacho sio halisi, kwa mantiki hiyo Sanamu ya mnyama ambayo inasujudiwa ni mfumo bandia wa Ibada Iliyo kinyume na ibada halisi ya Mungu wa Mbinguni.

Mtume paul akizungumza juu ya hili, yeye anauita huu ufalme au huyu mnyama kwamba ni mtu wa kuasi, sasa ameasi nini? Bila shaka ameasi Ibada halisi ya Mungu na kubuni ibada yake ya Bandia( sanamu) 2 Wathesalonike 2:3
yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.

#Note: huyu mtu wa kuasi anaabudiwa katika makanisa kwa kuingiza mafundisho potofu, likiwemo la Ibada bandia iliyo kinyume na Ibada halisi.

Ufunuo wa Yohana 13:16 Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;

#Note: Wale watakaokataa kufanya Ibada ya bandia itabidi wauawe au kupata mateso, na wale wote watakaokubali kufanya ibada bandia(sanamu ya Mnyama) ndio watapokea Chapa ya mnyama katika kipaji cha uso au katika mkono wa kuume, Hii chapa ya mnyama ndio namba 666 ambayo ni alama ya Utambulisho kwa wale wote waliokubali Kufanya ibada Bandia.

#Ufunuo wa Yohana 13:17 tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.
#Note: Anasema Chapa ya mnyama yaani ni jina la Mnyama au hesabu ya jina lake. Kwa hiyo namba 666 ndio Chapa ya mnyama ambayo ni alama ya mamlaka ya Utii kwa mpinga Kristo. Wale wote watakaokataa kufanya ibada bandia ndio watapitia mateso(dhiki kuu) maana kwanza Hawataweza kufanya huduma yoyote ya kijamii maana hawatambuliwi kisheria, na ili utambuliwe Kisheria ni lazima ukubali kufanya ibada bandia na upigwe chapa katika paji la uso au katika mkono wa Kuume.

Kwa hyo tuelewe kwamba Namba 666(Chapa ya mnyama)  ni alama ya Mamlaka ya Utii kwa Mpinga Kristo, yaani kila mtu atakaye kubali kufanya Ibada bandia huyu tayari anakuwa ameonesha mamlaka ya utii kwa Mpinga Kristo na hivyo mtu kama huyo atatambuliwa kisheria na ataweza kufanya huduma yoyote ya kijamii na atahudumiwa mahali popote.

#NOTE: Na ndio maana kwa sasa Dunia inapelekwa katika mfumo wa Kiteknolojia zaidi, ina maana itafika wakati mtu hautaweza kutambuliwa kisheria na hata katika kufanya huduma za kijamii, kama haujakubaliana na suala la Ibada bandia.

Kama tulivyoona CHAPA YA MNYAMA, ndio JINA LA MNYAMA lakini pia Hesabu ya jina hili ndio namba 666, sasa hili jina ni la Mamlaka ya utawala gani? Ambao huo utawala utashinikiza Ibada bandia kwa wakazi wa Dunia?
Cheo cha Papa kwa lugha ya Kilatini ni VICARIUS FILII DEI, yaani  Mwakilishi wa Mwana wa Mungu. Kwa mujibu wa Namba za Kirumi, namba zinasimama pia baadala ya Herufi: hivyo jina VICARIUS FILII DEI ukizihesabu zinaleta namba 666 ambacho ndio Cheo cha PAPA.
V=5, I=1, C= 100, A=0, R= 0, I=1, U ni sawa na V= 5, S= 0, F= 0, I=1, L=50, I= 1, I= 1, D= 500, E=0, I= 1.
Kwa hiyo ukijumlisha: 5+1+100+1+5+1+50+1+1+500+1 =666
Hivyo 666 ni sawa na kusema VICARIU FILII DEI ni kitu kilekile ikiwa na maana Mwakilishi wa Mwana wa Mungu.
HIVYO BASI wale watakao kubali Muungano wa Kiibada siku ya Jumapili, watakuwa wanakubaliana kwa hiyari yao katika akili zao kwamba Papa ni Mwakilishi wa Mwana wa Mungu.

Na hivyo wapendwa suala la namba 666 ni Ishara ya Utii kwa mamlaka ya Mpinga Kristo kwa wale wote watakaokubaliana na Ibada bandia. Na ndio maana vita na uhasama hauwezi ukaisha juu ya mvutano wa Ibada kati ya Sabato ya Bwana na Sabato bandia ya Jumapili. Sabato ya Jumamosi ni alama ya Utii kwa mamlaka ya Mungu kwamba ndio Muumbaji wa Mbinguni na nchi na Ibada ya Jumapili ni alama ya Mamlaka ya Utii kwa Kanisa Katoliki. Kwa hiyo tafsiri ya namba 666 ime base kwenye hoja ya ibada na sio Ugonjwa Corona au Computer nk.

Na ndio maana siku zote wanaoabudu Jumapili Wanauhasama na Amri za Mungu hawataki kusikia amri 10, hoja kubwa katika zile Amri 10 ni Kupinga Amri ya 4 tu inayohusu Kupumzika na kufanya Ibada siku ya Sabato. Na huu ndio ukweli ijapokuwa ni mchungu lakini ndivyo ilivyo kwamba Wale wote wanaopinga Ibada halisi ya Sabato na kung’ang’ania Ibada Bandia ya jumapili(sanamu ya mnyama) tufanye matengenezo ya kuufuta Ukweli vinginevyo tutaingia katika zahama ya kupokea Chapa ya mnyama au Namba 666.

#NAMBA_666 NI #KITU_GANI?

Mungu akubariki akubariki

Comments