MCHAKATO WA WOKOVU
:
Ili dhambi iwepo ni lazima iwepo sheria, Ina maana ukiondoa sheria Basi hakuna Dhambi. Warumi 5:13
maana kabla ya sheria dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria;
Kwa hiyo kazi ya sheria sio kumuokoa mtu, Bali Kazi ya sheria ni kutuonesha kosa na kutuelekeza kwa Yesu:
Warumi 7:7 Tusemeje, basi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalitambua dhambi ila kwa sheria; kwa kuwa singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani.
Kwa hiyo baada ya mtu kuvunja sheria anakuwa ametenda dhambi, na hivyo anapaswa kufa, maana mshahara wa dhambi ni Mauti (kifo). Warumi 6:23
Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Kwa hiyo tunaona Mwanadamu anapovunja sheria anakuwa ametenda dhambi, na mshahara wa dhambi ni Mauti/kifo cha Milele. Na hivyo Mwanadamu anahitaji msaada ili asife .
Ndipo kabla Mwanadamu hajafa, Mungu anaingilia kati kwa kumtoa Mwanae Pekee Yesu Kristo ili afe kwa ajili ya Mwanadamu
Warumi 5:8
Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.
Na hii ndio inaitwa Neema ni upendeleo tu hatukustahili,
Waefeso 2:8
Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
Na hivyo tunaweza kusema kwamba
Ukiondoa(kukataa) sheria kwamba haipo, Ina maana umekataa kwamba hakuna dhambi Duniani,, maana bila sheria hakuna dhambi.
Na Kama dhambi haipo Duniani, Ina maana hakuna kifo, maana mshahara wa dhambi ni Mauti.
Na Kama hakuna mauti inayotukabili Basi hakuna haja ya Neema, ambaye ni Yesu Kristo. Na hivyo pia Hakuna haja ya kuutafuta uzima wa Milele.
#Note mfano: mtu akizini anakuwa Amevunja sheria inayosema Usizini, na hivyo anakuwa ametenda Dhambi ya uzinzi, mtu huyu anakuwa anakabiliwa na Mauti ya Milele, Ufunuo wa Yohana 21:8
Bali.. wauaji, na #wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
Na hivyo huyu mzinzi ili asije kufa Milele katika Moto wa Jehanamu anapaswa kupokea zawadi ya Neema kwa kuamini kifo cha Yesu pale msalabani, Yohana 3:16
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Na hatimaye mzinzi huyu anakuwa na nafasi katika Uzima wa Milele.
Mungu akubariki

Comments
Post a Comment