MAONO JUU YA MPINGA KRISTO:

MAONO JUU YA MPINGA KRISTO:

Posted by Isack Mussa

Yohana alioneshwa mpinga Kristo akiwa anatawala Dunia, na uwezo wa mpinga Kristo ulikuwa juu ya Ulimwengu wote, hasa Watakatifu alipambana nao na kuwashinda.
Ufunuo wa Yohana 13:7
Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa.

Na hivyo kwa sababu amewashinda hata Watakatifu ikabidi aanze kumtukana hata Mungu wa Mbinguni Kama alivyofanya Senikarebi kwa Taifa la Israeli.
Ufunuo wa Yohana 13:6
Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni.

Mpinga Kristo alionekana kuiteka Dunia yote katika nyanja zote, Ina maana Kisiasa, Kiuchumi, Kiafya na Kidini. Licha kwamba shetani alionekana kuwashinda Watakatifu kwa nje, lakini Kiroho hakuweza na wala kwenye suala la kutaka kusujudiwa hawakukubali hata kidogo, Bali  watakaomsujudia ni wale ambao majina yao hayajaandikwa katika kitabu cha uzima.
Ufunuo wa Yohana 13:8
Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.

Kwa hiyo mtu yeyote ambaye Jina lake limeandikwa katika kitabu cha uzima hataweza kumsujudia shetani, maana watamshinda tu kwa Damu ya Mwanakondoo:
Ufunuo wa Yohana 12:11
Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.

Masherti makali yatawekwa katika maisha mtu hataweza kuhudumiwa ikiwa hajatimiza vigezo fulani, Wasio waaminifu wataona ni bora kutimiza ili maisha yaendelee, Bali walio wa Kristo watasema Ni bora kufa.
Ufunuo wa Yohana 13:17
tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.

Watakaoweza Kusimama katika kipindi hiki Ni wale Wanaoshika Amri za 10 na kuwa na ushuhuda wa Yesu pekee.
Ufunuo wa Yohana 14:12
Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.

Na hiki ndicho kipindi cha Dhiki kwa Watakatifu, lakini atawaokoa Watakatifu wake Kama alivyowaokoa Rafiki zake Danieli katika tanuru la moto na Kama alivyomuokoa Daniel katika Tundu la Simba, ndivyo ambavyo Mungu atawaokoa  watu wake. Isaya 43:2
Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.

Barikiwa

Comments