MAAJABU YA KIFO CHA YESU

#MAAJABU YA KIFO CHA YESU:

Kifo cha msalabani kilikuwa ni moja ya kifo hatari sana kwa Warumi, na waliokuwa wanauwawa kupitia kifo cha msalabani, Walikuwa ni wale watu waliokuwa wameshindikana kabisa katika Taifa au jamii Kama Baraba.

Kuangikwa msalabani ilikuwa ni kutangaza kwamba huyo mtu amekataliwa kwa wanadamu na kwa  Mungu pia na ndio maana waliangikwa juu, ishara ya kukataliwa mbinguni na Duniani, Lakini ilikuwa ni ishara kwamba amelaaniwa. Wagalatia 3:13

Kifo hiki cha msalaba kilikuwa ni moja ya kifo cha aibu sana maana ilikuwa ni lazima uangikwe katikati ya mji au hata kwenye makutano ya barabara au barabara kuu ili kila mtu anayepita ashuhudie. Na ilikuwa lazima liwepo bango linaloonesha taarifa zako. Na ndio maana hata Paulo anapozungumzia kifo Cha Yesu hasemi tu kwamba Yesu alikufa, Bali anaonesha uzito wa aina ya kifo, kwa kusema "Naam mauti ya msalaba" Wafilipi 2:5-8, kuonesha kwamba kifo cha msalabani hakikuwa kifo cha kawaida.

Mbaya zaidi kifo cha msalaba kilitumiwa sana na Warumi kwa sababu wanasema ni moja ya kifo chenye mateso makali sana, na mtu aliyeangikwa msalabani, ilikuwa inachukua siku 3 hadi 4 ndio anakufa. Na ndio maana wale wezi walivunjwa miguu ili wafe haraka. Yohana 19:32,33
Basi askari wakaenda, wakamvunja miguu wa kwanza, na wa pili, aliyesulibiwa pamoja naye.
Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu;

Sasa Jambo ambalo ni la kushangaza na ambalo hata pilato halikumuingia akilini ni kile kitendo cha Yesu kufa ndani ya masaa 6 baadala ya siku 3 au 4, na ndio maana Pilato alipopewa taarifa kwamba Yesu amekufa ilikuwa vigumu kusadiki mpaka alipopata uhakika!!
Marko 15:44
Lakini Pilato akastaajabu, kwamba amekwisha kufa. Akamwita yule akida, akamwuliza kwamba amekufa kitambo.
Marko 15:45
Hata alipokwisha kupata hakika kwa yule akida, alimpa Yusufu yule maiti.

Hoja ni kwamba Unabii haudanganyi Yesu alikufa mapema ili unabii usije ukashindwa kutimia, maana ilitabiliwa kwamba Yesu hangevunjwa mfupa wowote,
#Kutoka 12:46 Na aliwe ndani ya nyumba moja; usiichukue nje ya nyumba nyama yake yo yote; wala msivunje mfupa wake uwao wote.

Na hivyo laiti Yesu angechelewa kufa Kama wale majambazi wawili naye akavunjwa miguu, Basi unabii ungekuwa wa uongo:

Kwa maajabu ya kifo hiki ndio ulikuwa ukombozi wa Mwanadamu aliyepaswa kufa milele.

Mungu akubariki

Comments