KWANINI WAKRISTO WENGI WANASALI JUMAPILI??

*KWANINI TUNASALI JUMAPILI WA KATOLIKI HUKU MADHEHEBU YA KIPENTEKOSTE YAANI WALOKOLE WAKITUFUATA BILA KUJUA KUWA SISI NDIO WANZILISHI WA IBADA YA JUMAPILI?*

JIBU

*TULIONELEA KANISA KATOLIKI  KUBADILI SABATO YA BWANA KUTOKA SIKU YA SABA (YAANI JUMAMOSI ) KWENDA SIKU YA KWANZA YA JUMA  (YAANI JUMAPILI )*

Nanukuu kitabu cha

BUSTANI YA KATEKISTA CHA PADRE RAPHAEL ROGEAU W.F.

PUBLISHING-benedictine publications ndanda-peramiho ukurasa wa 74

Swali: KWA NINI TUNASALI SIKU YA JUMAPILI SIO SABATO?

Jibu: Kihistoria tunaelewa kwamba wakristo wa kwanza waliendelea kuadhimisha siku ya Bwana Jumamosi, walivyozoea wayahudi; hasa wakristo waliotoka dini ya kiyahudi......

Wale ambao walikuwa wanatoka upagani, hawakujisikia kuwa wanabanwa na sheria zile.........

Sababu nyingine ya kusali Jumapili ni hii; wafuasi wa Yesu walitaka kujitofautisha na waamini wa dini ya kiyahudi walioadhimisha ibada siku ya Jumamosi......

Polepole wakristo wakaanza kuzoea kukutana, kusali, kusoma masomo yao na kumega mkate siku ya kwanza.....

Ndivyo, tarehe 03/03/321, mfalme Konstantino alivyotangaza rasmi kwamba Jumapili iwe SIKU YA BWANA, wakristo wapumzike na kusali. Hayo ndiyo mapokeo ya Makanisa mengi ya JUMAPILI

SWALI  KATI YA  MFALME KONSTANTINO NA MUNGU YUPI TUMFUATE JE KUNA AYA KUNA AYA NDANI YA BIBLIA KUWA SABATO TAKATIFU NI JUMAPILI? WAPI MANABII NA WALIFUATA MITUME WALIMFUATA KONSTANTINO BADALA YA MWENYEZI MUNGU?

MUNGU ALIIBARIKI,ALIITAKASA,NA  ALISTAREHE  SIKU YA SABA  AMABAYO NDIYO SABATO TAKATIFU YAKE NA SI SIKU YA KWANZA YA JUMA

NA KUITAKASA  ,

✔(Mwanzo 2 )

------------

1 Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote.

2 Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya.

3 Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.

YESU KRISTO HAKUBILI SABATO KWENDA JUMAPILI

✔(Luka 4 )

------------

14 Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando.

15 Naye alikuwa akifundisha katika masinagogi yao, akitukuzwa na watu wote.

16 Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.

17 Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa,

18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,

19 Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.

20 Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho.

MITUME WALITUNZA SABATO YA MWENYEZI MUNGU

✔(Matendo  16 )

------------

13 Hata siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale.

14 Mwanamke mmoja, jina lake Lidia, mwenye kuuza rangi ya zambarau, mwenyeji wa Thiatira, mcha Mungu, akatusikiliza, ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana, ayatunze maneno yaliyonenwa na Paulo.

15 Hata alipokwisha kubatizwa, yeye na nyumba yake, akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani mwangu mkakae. Akatushurutisha.

✔(Matendo 17 )

------------

1 Wakiisha kupita kati ya Amfipoli na Apolonia wakafika Thesalonike, ambapo palikuwa na sinagogi la Wayahudi.

2 Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu,

3 akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kwamba, Yesu huyu ninayewapasha ninyi habari zake ndiye Kristo.

4 Wengine miongoni mwao wakaamini, wakashikamana na Paulo na Sila; na Wayunani waliomcha Mungu, wengi sana, na wanawake wenye cheo si wachache.

WALIOONGOLEWA KWA INJILI KWA KUPITIA MITUME WA YESU KRISTO WALITUNZA SABATO YA MWENYEZI MUNGU  HAKUNA ALIYEMFATA MFALME KONSTANTINO

✔(Matendo 13 )

------------

42 Na walipokuwa wakitoka, wakawasihi waambiwe maneno haya sabato ya pili.

43 Sinagogi ilipofumukana, Wayahudi na waongofu watauwa wengi wakashikamana na Paulo na Barnaba; ambao, wakisema nao, wakawatia moyo kudumu katika neema ya Mungu.

44 Hata sabato ya pili, watu wengi, karibu mji wote, wakakusanyika walisikie neno la Mungu.

-----------------------------------------------

NANUKUU KITABU KINGINE CHA KIKATOLIKI KIITWACHO

MUNGU NA WANADAMU 1988 MWANDISHI PETER UKRASA 72

SWALI KWANINI  TUNASALI JUMAPILI,

JIBU

KANISA KATOLIKI LIONELEA KUHAMISHA UTUKUFU WA SABATO YA MUNGU KUTOKA SIKU YA SABA (YAANI JUMAMOSI ) KWENDA  SIKU YA KWANZA YA JUMA  (YAANI JUMAPILI )

--------------------------------------------------

HUU USHAHIDI WA KUONELEA KUBADILI SABATO YA BWANA MUNGU KWENDA JUMAPILI, UMEJIRUDIA SANA KWENYE VITABU VIFUATAVYO  KUTOKA KWENYE MAKTABA YA KIKATOLIKI

------------------------------------------------------

1:KATEKISIMU YA KANISA KATOLIKI  UKRASA WA  483 KWENYE VIPENGELE VIFUATAVYO

                ✔2171

                ✔ 2173

                ✔ 2174

------------------------------------------------------

2:KATEKISIMU YA WAUMINI  1977 MWANDISHI PETER  UKRASA WA 50

------------------------------------------------------

3: MUNGU NA WANADAMU  TOLEO LA PILI 1988 UKRASA WA 72

Ukweli upo wazi asikiaye  Neno la Mungu ndiye atakaye okolewa

Comments