JE WATAKA KUINGIA MBINGUNI??


UKITAKA KUKOSA MBINGU BASI WEWE ENDELEA KUSEMA AMRI ZILIISHIA MSALABANI:

Isack Mussa

1. Huwezi kuurithi Ufalme wa Mungu ikiwa unavunja Amri za Mungu.
Mathayo 19:17, 18
Akamwambia Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri.
Akamwambia, Zipi? Yesu akasema, Ni hizi, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo,

2. Kiongozi Yeyote anayewafusha watu kwamba Amri ziliishia msalabani, yupo hatarini kukosa Mbingu.
#Mathayo 5:19
Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.

3. Mtu anayesema anampenda Mungu lakini anavunja Amri huyo ni Muongo:
1 Yohana 2:3
Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake.
Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni #mwongo, wala kweli haimo ndani yake.

4. Shetani anawachukia na anapambana na wale wanao shika Amri za Mungu.
Ufunuo wa Yohana 12:17
Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.

5. Shetani anawashinikiza watu kuvunja Amri za Mungu kwa sababu sifa za Mtakatifu ni mbili tu, kushika Amri na Kuwa na imani ya Yesu.
Ufunuo wa Yohana 14:12
Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.

6. Yesu mwenyewe alisema kigezo cha kujua kwamba unampenda sio kusema tu kwa maneno, Bali ni kwa kuzishika Amri.
Yohana 14:15
Mkinipenda, mtazishika amri zangu.

Mhubiri 12:13
Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.

Ushauri: ukitaka kuurithi Ufalme wa Mungu, Basi mche Mungu na kushika amri.

Mungu akubariki
0627729770
0689980058

Comments