JE? MARIA MAMA YAKE YESU ANAPASWA KUABUDIWA??

JE? MARIA MAMA YAKE YESU ANAPASWA KUABUDIWA??

Posted Isack Mussa

A. Mariamu Alitenda Dhambi?

Kanisa Katoliki hufundisha kuwa Maria hakutenda dhambi na wala hakuwa na doa lolote la dhambi ya asili hili kamwe siyo fundisho la Biblia.

Biblia inasema, “wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Warumi 3:23).

“Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi;

sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa, kama upepo uondoavyo” (Isaya 64:6).

“Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja” (Zaburi 14:3; 53:3).

Aliye mwema ni Mungu pekee (Mathayo 19:16-17).
Rejea pia Warumi 3:10-23; 5:12.
B. Mariamu Alihitaji Wokovu Kama Sisi vile vile.

Luka 1:47 Mariamu mwenyewe humwita Yesu, “Mwokozi wangu.”

Iwapo yeye mwenyewe alimwitaji Mwokozi, anawezaje tena, wakati huohuo, kuwa mwokozi wetu? Kwa nini amwite Kristo kuwa ni Mwokozi wake?

Jibu ni rahisi: kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa mdhambi mwenye kuhitaji upatanisho kwa Mungu vilevile kama sisi.

Mtu asiyekuwa na dhambi hamwitaji Mwokozi. Kwa maneno ya Yesu:

“Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi” (Mathayo 9:12).

Marimu alikiri kuwa alikuwa mdhambi alimwitaji Mwokozi Yesu kwa ajili ya wokovu wake, vilevile kama sisi tunavyomwitaji Bwana Yesu.

C. Biblia Hufundisha Tuombe kwa Jina la Yesu.

Sehemu Kubwa ya Sala ya Rozari Humwelekea Maria.

Katika sala kuu Yesu aliwaelekeza wanafunzi Wake wanapoomba waseme, “Baba yetu uliye mbinguni…” (Mathayo 6:9).
Kila ombi katika Biblia humwelekea Mungu pekee.

Hakuna mfano hata mmoja kwenye Biblia wa mtu anayemwomba “mtakatifu” yeyote wala malaika, isipokuwa yale maombi ya waabudusanamu.

Na kila wakati mtu fulani alipojaribu kumsujudia mwanadamu mwingine, tofauti na Mungu, mtu huyo anaambia asifanye hivyo
(Matendo ya Mitume 10:25–26; 14:13–16; Mathayo 4:10; Ufunuo 19:10; 22:8–9).

Lakini Kanisa Katoliki hufundisha humwabudu Mungu na “kumstahi” Maria na watakatifu. Je, kuna tofauti gani?

Mtu anayeomba sala ya Rozari hutumia muda mwingi kumtaja Maria kuliko Mungu.

Kwa kila mmoja ya sifa kwa Mungu kwenye Rozari, kuna sifa 10 kwa Maria!
D. Yesu Pekee Ndiye Mpatanishi Wetu.

Sala ya Rozari humpatia wajibu Maria asiokuwanao kamwe katika Biblia.

Yesu ndiye Mkombozi wetu (Wagalatia 3:13; 4:4-5; Tito 2:14; 1 Petro 1:18-19; Ufunuo 5:9),

Mwombezi wetu aliye mbinguni (1 Yohana 2:1), na Mpatanishi wetu pekee (1 Timotheo 2:5).

Lakini sehemu ya sala hii ya “Salamu, Malkia Mtakatifu” kwenye Rozari humwita Maria “mtetezi mwenye fadhili kuu.”

Hili hupingana moja kwa moja na fundisho dhahiri la Maandiko kwa Yesu ndiye Mpatanishi wetu.

“Yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi Yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho”

(2 Wakorintho 5:19). “Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu” (1 Timothy 2:5).

E. Mariamu Hujiita, “Mjakazi wa Bwana.”
Sala ya Rozari huwahitaji Wakatoliki kumtaja Maria kama “Malkia mtakatifu.”

Katika Biblia mara moja tu ambapo jina hili hutumika, “Malkia wa Mbinguni” ni katika neno linalotumika katika maana hasi (Yeremia 7:17-19; 44:16-27). Kamwe Biblia haimtaji Mariamu kama malkia.

Mariamu anajiita mwenyewe kuwa ni “mjakazi wa Bwana” (Luka 1:38).

Kamwe hakupewa utawala wala mamlaka juu ya mbingu na dunia. Vilevile, je, ni sawa wakati wa kuomba sala ya Rozari kumwita Maria “u uhai wetu” na “tumaini letu?”

Kwa mara nyingine tena, haya ni maneno yanayotumika kwa Mungu peke Yake katika Maandiko (Yohana 1:1-14; Wakolosai 3:4; 1 Timotheo 1:1; Waefeso 2:12; Tito 2:13)
Hakuna mwanadamu yeyote anayestahili cheo hicho cha Mungu.

Kwa ufupi, Sala ya Rozari inapingana kabisa na Maandiko Matakatifu kwa namna mbalimbali.

Ni Mungu pekee ndiye awezaye kusikia maombi yetu. Ni Mungu pekee ndiye awezaye kuyajibu maombi yetu.

Tunaye Mpatanishi mmoja, ambaye ni Yesu, na ni katika jina Lake ndilo tupaswalo kuomba kwalo, siyo la Maria.

Hakuna msingi wa wowote wa Kibiblia wa
(1) kuomba kwa Maria
(2) kumtaja kama “mtakatifu,”
(3) kumwita “u uhai wetu” na “tumaini letu.”
Na wala hahusiki kwa namna yoyote ile na wokovu wetu.

“Ikawa alipokuwa akisema maneno hayo, mwanamke mmoja katika mkutano alipaza sauti yake, akamwambia [Yesu], Heri tumbo lililokuzaa, na matiti uliyonyonya.

Lakini Yeye alisema, Afadhali, heri walisikiao neno la Mungu na kulishika” (Luka 11:27, 28; linganisha pia Marko 3:31-35).

Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” (Matendo ya Mitume 4:12). “Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;

ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba” (Wafilipi 2:9-11).<<>>

Barikiwa

Comments