JINSI YA KUKUMBUKA KUFUFUKA KWA YESU:

INSI YA KUKUMBUKA KUFUFUKA KWA YESU:
Posted by Is ack Mussa

Watu wengi tumeaminishwa kwamba sikukuu ya Pasaka ni kukumbuka kufufuka kwa Yesu. Hii hoja haipo sahihi ufufuo wa Yesu haukumbukwi kwa njia ya Pasaka,

Kushereke kufufuka kwa Yesu si vibaya ni halali kabisa, Bali shida inakuja namna ya kusherea ndio tunakosea.

Je, BIBLIA inafundishaje jinsi ya kukumbuka kifo na kufufuka kwa Yesu?

Warumi:6.3
Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?

Kumbe suala la mtu kubatizwa katika maji mengi ni sawa na mauti/ kifo cha Yesu, Ikiwa na maana MAJI yanawakilisha kaburi.

Anaendelea kwa kusema

Warumi:6.4
Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo #alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.

Kumbe kitendo cha kuzamishwa katika maji ni sawa na kuzikwa katika kaburi Kama Yesu,, na kitendo cha kuinuliwa majini ni ishara ya Kufufuka, kutoka kwenye utu wa kale.

Kwa hivyo kwa Mkristo UFUFUO wa Yesu unakumbukwa siku ya kubatizwa katika maji mengi, na kufufuka ukiwa kiumbe kipya, kama Yesu alivyofufuka akiwa na Utukufu wa Baba.

#Wakolosai 2:12 inasema " Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo, na katika huo #mkafufuliwa pamoja naye....." Ubatizo ndio kumbukumbu ya kufa na kufufuka kwa Yesu, na hii inafanyika siku yoyote na tarehe yoyote.

Mitume hawajawahi kusherekea Pasaka kwamba ni sikukuu ya kufufuka kwa Yesu, Bali mitume walikuwa waliadhimisha kifo na mateso ya Yesu kwa njia ya Meza ya Bwana, yaani kumega mkate na kunywa divai. 1 Wakorintho 11:26
Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.

Kwa hiyo ufufuo wa Yesu haukumbukwi kwa kula wali na kunywa soda au kuvaa nguo mpya, Bali kufufuka kwa Yesu kunakumbukwa kwa kubatizwa katika maji mengi(ishara ya kufa) na kufufuka kutoka majini ukiwa kiumbe kipya na kuishi maisha matakatifu.

#Ushauri: ikiwa unataka kuadhimisha kufufuka kwa Yesu Basi ni ile siku ambayo ulimpokea Yesu kwa njia ya Ubatizo, ukazikwa katika maji na kuinuliwa(kufufuka) Kama kiumbe kipya. Tarehe Kama hiyo unaweza kufanya sherehe na familia na marafiki kwa kukumbuka siku uliyokufa na kufufuka Kama Yesu.

Lakini Easter kwa kweli sio sikukuu ya Kikristo ni upagani, ulianzishwa na Wakatoliki mwaka 325 katika Mtaguso wa Nikea.

MUNGU AKUBARIKI.

           BY.
                    0627729770

Comments