BIBLIA INATAJA HASARA ISHIRINI ( 30 )
ZA KUTOSHIKA AMRI ZA MUNGU.
Kila ninaposoma Biblia yote toka Kitabu cha Mwanzo hadi ufunuo nakutana na faida nyingi za kushika amri na Sheria za Mungu; lakini pia nakutana na hasara nyingi za kutoshika amri na Sheria za Mungu. Ajabu Ni kuwa viongozi wa madhehebu wanawafundisha watu kudharau na kutoshika amri za Mungu. Hizi hapa chini Ni hasara 30 za kutoshika amri na Sheria za Mungu.
1. Hasara ya kwanza ya kutoshika amri za Mungu.
Wanaoacha amri za Mungu wanafanya ibada ya bure.
"Nao waniabudu bure wakifundisha Mafundisho yaliyo maagizo ya Wanadamu. Ninyi mwaiacha amri ya Mungu , na kuyashika mapokeo ya Wanadamu." (Marko 7:7,8)
"Akajibu, akawaambia, mbona ninyi nanyi huihalifu amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu? ...Nao waniabudu bure, wakifundisha Mafundisho yaliyo maagizo ya Wanadamu." (Mathayo 15:3,9)
2. Biblia inasema wasioshika amri na sheria za Mungu ni waongo.
"Yeye asemaye, nimemjua, wala hazishiki Amri zake, ni mwongo wala kweli haimo ndani yake." (1Yohana 2:4)
"Umewakataa wote wazikosao amri zako kwa maana hila zao ni uongo" (Zaburi 119:155)
"Kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya BWANA." (Isaya 30:9)
3. Anayeacha kushika amri moja amekosa juu ya amri zote.
"Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote. Kwa maana yeye aliyesema, usizini, pia alisema, usiue, Basi ujapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria." (Yakobo 2:10,11)
4. Yesu anasema ni unafiki kulipa zaka na kuacha mambo makuu ya sheria.
"Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria yaani, adili,na rehema,na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache." (Mathayo 23:23)
5. Mungu amewakataa wote wazikosao amri zake.
"Umewakataa wote wazikosao amri zako, kwa maana hila zao ni uongo."
(Zaburi 119:118)
"Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako. "
(Hosea 4:6)
"Hata na watu wa Yuda hawakuyashika maagizo ya BWANA, Mungu wao, lakini walikwenda katika amri za Israeli walizokuwa wamezifanya wenyewe. Basi, BWANA akakikataa kizazi chote cha Israeli, akawatesa, na kuwatia katika mikono ya watu wenye kuwateka nyara, hata alipokwisha kuwatupa, watoke machoni pake." (2Wafalme 17:19,20)
6. Wasiojifunza amri za Mungu wokovu u mbali nao.
"Wokovu u mbali na wasio haki, kwa maana haawajifunzi amri zako."
(Zaburi 119:155)
"Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; ..." (Mathayo 5:19)
7. Mungu atawaadhibu wote wasioshika amri zake.
"Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Yuda, naam , kwa manne, sitazuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wameikataa sheria ya BWANA; wala hawakuzishika amri zake..." (Amosi 2:4)
"Wanawe wakiiacha sheria yangu,...
Wakizihalifu amri zangu, Wasiyashike maagizo yangu, Basi, nitawarudi makosa yao kwa fimbo, Na uovu wao kwa mapigo."
(Zaburi 89:30-32)
"...nao wataikubali adhabu ya uovu wao; ni kwa sababu...roho zao zimezichukia amri zangu." (Walawi 26:43)
8. BWANA anawaghabikia sana waiachao sheria na amri zake.
"Wakaziacha amri zote za BWANA Mungu wao...Kwa hiyo BWANA anawaghabikia Israeli sana, akawahamisha mbali na uso wake, wala hapana aliyesalia ila kabila ya Yuda peke yake.". (2 Wafalme 17:16,18)
"Ghadhabu imenishika kwa sababu ya wasio haki, waiachao sheria yako." (Zaburi 119:53)
"Naam, walifanya mioyo yao kuwa kama jiwe gumu, wasije wakaisikia Sheria na maneno ya BWANA wa Majeshi, aliyoyapeleka kwa roho yake kwa mkono wa manabii wa kwanza, kwa sababu hiyo ghadhabu kuu kutoka kwa BWANA wa majeshi." (Zekaria 7:12)
9. Anayeacha amri za Mungu anamfuata miungu mingine na ni mtaabishaji wa watu wa Mungu.
"Naye akajibu, si mimi niliyewataabisha Israeli; bali ni wewe, na nyumba ya baba yako, kwa kuwa mmeziacha amri za BWANA; nawe umefuata mabaali." (1 Wafalme 18:18)
10. Biblia inasema, asiyetaka kuisikia sheria hata sala yake ni chukizo kwa Mungu.
"Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria, hata sala yake ni chukizo."
(Mithali 28:9)
11. Wasiotaka kuisikia sheria ya Mungu, na wavunja sheria Biblia inawaita waasi.
"Whosoever committeth sin transgresseth also the law: for sin is the transgression of the law." KJV 1 John 3: 4
"Kila atendaye dhambi afanya uasi wa sheria: kwa kuwa dhambi ni uasi wa sheria."
(1 Yohana 3:4)
"Kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya BWANA." (Isaya 30: 9)
"Lakini nyumba ya Israeli waliniasi jangwani; hawakuenda katika amri zangu, ...."
(Ezekieli 20:13)
12. Wasioenda kwa sheria na ushuhuda hawana asubuhi. (Wamo gizani)
"Na waende kwa sheria na Ushuhuda, ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi" (Isaya 8:20)
13. Wasioshika amri za Mungu laana zinawafuata.
"Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, usiangalie kuyafanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata." (Kumbukumbu 28: 15)
"Israeli wote wameihalifu sheria yako, kwa kugeuka upande, wasisikilize sauti yako, Basi kwa hiyo laana imemwagwa juu yetu..."
(Daniel 9:11)
"Na laana hizi zote zitakujilia juu yako, zitakuandama na kukupata, hata uangamizwe, kwa kuwa hukuisikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kushika maagizo yake na amri zake alizokuagiza." (Kumbukumbu 28:45)
"Tena dunia imetiwa unajisi kwa watu wanaoikaa; kwa maana wameziasi sheria, wameibadili amri, wamelivunja agano la milele. Ndiyo sababu laana imeila dunia hii, na hao wanaoikaa wameonekana kuwa na hatia," (Isaya 24:5,6).
14. Waliokuwa washika amri za Mungu, wakiacha kushika amri, wanafananishwa na mbwa anayekula matapiko yake.
"Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa.
Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni."
(2 Petro 2:21,22)
15. Wasioshika amri za Mungu wanamkasirisha na kumgadhabisha BWANA.
"Lakini nyumba ya Israeli waliniasi jangwani; hawakuenda katika amri zangu, ... na sabato zangu walizitia unajisi sana; ndipo nikasema, Nitamwaga hasira yangu juu yao jangwani, ili niwaangamize." (Ezekieli 20:13)
"Wakaziacha amri zote za Bwana, Mungu wao, wakajifanyizia sanamu za kusubu, yaani, ndama mbili, ......wakajiuza nafsi zao wapate kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, hata kumkasirisha.
(2 Wafalme 17:16,17)
16.Biblia inasema wasiofuata sheria za Mungu wana kiburi.
"Wenye kiburi wamenichimbia mashimo, Ambao hawaifuati sheria yako."
(Zaburi 119:85)
17.Wasioshika amri za Mungu; hatimaye mabaya yatawapata.
" nitaleta mabaya juu ya watu hawa, ...kwa sababu hawakuyasikiliza maneno yangu; tena kwa habari ya sheria yangu, wameikataa."
(Yeremia 6:19)
" nao wakaingia, wakaimiliki; lakini hawakuitii sauti yako, wala hawakuenda katika sheria yako; hawakutenda neno lo lote katika haya uliyowaagiza wayatende; basi, kwa sababu hii umeleta juu yao mabaya haya yote."
(Yeremia 32:23)
" Hawajanyenyekea hata leo, wala hawakuogopa, wala hawakuenenda katika sheria yangu, wala katika amri zangu, nilizoweka mbele yenu, na mbele ya baba zenu. ... Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitaelekeza uso wangu juu yenu, ili niwaletee mabaya, hata kukatilia mbali Yuda yote."
(Yeremia 44:10-11)
"... na kwa sababu mmetenda dhambi juu ya Bwana, wala hamkuitii sauti ya Bwana, wala hamkwenda katika ... amri zake,... ndiyo maana mabaya haya yamewapata kama ilivyo leo." (Yeremia 44:23)
18.Wasioshika sheria na amri za Mungu watakatiliwa mbali na kuangamizwa.
"Bali mkighairi, mkaacha kunifuata, ninyi na watoto wenu, msizishike sheria zangu na amri zangu, nilizoziweka mbele yenu, tena mkienda na kuitumikia miungu mingine na kuiabudu,
basi nitawakatilia Israeli mbali na nchi hii niliyowapa;..." (1 Wafalme 9:6,7)
"Lakini nyumba ya Israeli waliniasi jangwani; hawakuenda katika amri zangu,... na sabato zangu walizitia unajisi sana; ndipo nikasema, Nitamwaga hasira yangu juu yao jangwani, ili niwaangamize." (Ezekieli 20:13)
19.Wasioshika amri na sheria za Mungu wamemsahau Bwana.
"Jihadhari, usije ukamsahau Bwana, Mungu wako, kwa kutozishika amri zake, ...na sheria zake, ninazokuamuru leo."
(Kumbukumbu la Torati 8:11)
20. Wasioshika amri za Mungu wamemwacha Bwana, naye Bwana atawaacha.
"...akawaambia, Mungu asema hivi, Kwani ninyi kuzihalifu amri za Bwana, hata msiweze kufanikiwa? Kwa kuwa mmemwacha Bwana, yeye naye amewaacha ninyi. "
(2 Mambo ya Nyakati 24:20)
21.Wasioshika amri za Mungu wamejikosesha uwezo wa kutofautisha vitu vitakatifu na vya kutumiwa siku zote.
"Makuhani wake wameihalifu sheria yangu, wametia unajisi vitu vyangu vitakatifu; hawakuweka tofauti ya vitu vitakatifu na vitu vya kutumiwa sikuzote; wala hawakuwafundisha watu kupambanua vitu vichafu na vitu vilivyo safi, nao wamefumba macho yao, wasiziangalie sabato zangu, nami nimetiwa unajisi kati yao."
(Ezekieli 22:26)
22. Kukataa kushika amri na sheria za Mungu ni kutoitii sauti ya Mungu.
"wala hatukuitii sauti ya Bwana, Mungu wetu, kwa kwenda katika sheria zake, alizoziweka mbele yetu kwa kinywa cha watumishi wake, manabii." ( Danieli 9:10)
" Naye Bwana asema, Ni kwa sababu wameiacha sheria yangu niliyoweka mbele yao, wala hawakuitii sauti yangu,..."
(Yeremia 9:13)
" Walakini hawakukutii, wakakuasi, wakaitupa sheria yako nyuma yao, wakawaua manabii wako walioshuhudu juu yao wapate kuwarejeza kwako; wakatenda machukizo makuu. (Nehemia 9:
23.Waisraeli waliondolewa katika nchi yao na kupelekwa utumwani kwa sababu ya kuziacha amri za Mungu.
" Lakini mkigeuka, na kuziacha sheria zangu na amri zangu nilizoweka mbele yenu, mkienda, na kuitumikia miungu mingine, na kuiabudu; ndipo nitawang'oa katika nchi yangu niliyowapa; ..."
(2 Mambo ya Nyakati 7:19-20)
"Naye Bwana asema, Ni kwa sababu wameiacha sheria yangu niliyoweka mbele yao, wala hawakuitii sauti yangu, wala kuenenda katika hiyo;
Nami nitawatawanya kati ya mataifa, ambao wao hawakuwajua; wala baba zao, nami nitatuma upanga nyuma yao, hata nitakapowaangamiza kabisa.
(Yeremia 9:13,16)
24.Kutoshika sheria na amri za Mungu ni kutomtumikia Mungu.
"na wafalme wetu, na wakuu wetu, na makuhani wetu, na baba zetu, hawakuishika sheria yako, wala hawakuzisikiliza amri zako na shuhuda zako, ulizowashuhudia.
Kwa kuwa hawakukutumikia wewe.... wala hawakughairi na kuyaacha mabaya yao.
(Nehemia 9:34-35)
25.Kutoshika sheria na amri za Mungu ni kutenda uovu.
"Tumetenda maovu mengi juu yako, wala hatukuzishika amri, wala sheria,..."
(Nehemia 1:7)
"Wao waiachao sheria huwasifu waovu; Bali wao waishikao hushindana nao. "
(Mithali 28:4)
26.Kutoshika amri na sheria za Mungu ni kuwa na shingo ngumu.
" ukawashuhudia ili uwarudishe tena katika sheria yako; lakini walitakabari, wasizisikilize amri zako, ... nao wakayaondoa mabega yao, wakafanya shingo zao kuwa ngumu, wasitake kusikiliza. (Nehemia 9:29)
27. kutoshika amri za Mungu ni kukosa unyenyekevu.
"Hawajanyenyekea hata leo, wala hawakuogopa, wala hawakuenenda katika sheria yangu, wala katika amri zangu, ... (Yeremia 44:10)
28.Wasioshika amri za Mungu wanatenda dhambi.
"Kwa sababu...mmetenda dhambi juu ya Bwana, wala hamkuitii sauti ya Bwana, wala hamkwenda katika...amri zake,.. ndiyo maana mabaya haya yamewapata...." (Yeremia 44:23)
"Hawakulishika agano la Mungu; Wakakataa kuenenda katika sheria yake; Lakini wakazidi kumtenda dhambi, Walipomwasi Aliye juu ..." (Zaburi 78:10,17)
29. Kuziasi sheria za Mungu ni kuongeza unajisi duniani.
"Tena dunia imetiwa unajisi kwa watu wanaoikaa; kwa maana wameziasi sheria, wameibadili amri, wamelivunja agano la milele." (Isaya 24:5)
30. Kufanya vita dhidi ya amri za Mungu ni kufanya kilekile anachokifanya shetani.
"Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari."
Ufunuo wa Yohana 12:17
AMRI 10 ZA MUNGU HIZI HAPA.
(Kutoka 20:3-17)
1. Usiwe na miungu mingine.
2.Usitumikie na kuabudu sanamu
3.Usilitaje bure jina la BWANA Mungu wako.
4.Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
5.Waheshimu baba yako na mama yako.
6.Usiue
7.Usizini
8. Usiibe
9.Usishuhudie uongo
10. Usitamani mali na mke wa jirani yako.
Mungu akubariki sana unapotafakari na kuchukua hatua.

Comments
Post a Comment