CHIMBUKO LA UPAPA AU PEMBE NDOGO KATIKA UNABII WA BIBLIA?.

CHIMBUKO LA UPAPA  AU PEMBE NDOGO KATIKA UNABII WA BIBLIA?.

Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne watakaotokea dunia..............na habari za zile pembe kumi zilizokuwa kichwani mwake, na ile pembe nyingine iliyozuka, ambayo mbele yake zilianguka pembe tatu; yaani, pembe ile yenye macho, na kanwa lililonena makuu, ambayo kuonekana kwake kulikuwa hodari kuliko wenzake. Nikatazama, na pembe iyo hiyo ilifanya vita na watakatifu, ikawashinda , Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati DANIELI 7 ;17-22,25 . Na kama vile ulivyoziona hizo nyayo za miguu na vidole vyake, kuwa nusu udongo wa mfinyanzi, na nusu chuma, ufalme ule utakuwa ufalme uliogawanyika; lakini ndani yake zitakuwako nguvu za chuma, kama vile ulivyoona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope.  Na kama vidole vya zile nyayo vilikuwa nusu chuma na nusu udongo, kadhalika ufalme ule utakuwa nusu yake una nguvu, na nusu yake umevunjika DANIELI 2:;41-42  

Maelezo😈😈

🧡Jambo la kuzingatia ni hili baada ya utawala huu wa RUMI YA UPAGANI ulifuata RUMI YA UKRISTO ina maana kwamba Rumi ya upangani iliungana na Rumi ya ukristo kuwa kitu kimoja

🛑PEMBE KUMI ZILITOKANA NA NINI?- Zilitokana na ufalme wa nne wa RUMI YA UPAGANI ufalme huu haukutawaliwa na mwingine ila ilipofikia mwisho uligawanyika katika falme kumi . 🧡

🛑PEMBE KUMI NA VIDOLE KUMI ZILIWAKILISHA NINI -  Zinawakilisha  ufalme wa RUMI YA  UKRISTO

🛑FALME TATU AU PEMBE TATU ZILIZOANGUSHWA  ZILIWAKILISHA NINI –Pembe tatu au falme tatu zilizoangushwa kwa kushambuliwa na pembe ndogo ambazo ni HERULI,VANDALS,NA OSTROGOTHS

🛑FALME SABA AU PEMBE SABA ZILIZOBAKI NI NCHI GANI?-Pembe au Falme saba zilizobaki ambazo ni England,France,Spain,Portugal,Germany,Switzeland ,Italy

🛑UTAWALA HUU   WA RUMI YA UKRISTO -Ulianza kutawala dunia tangu mwaka   476 A.D  utaende hadi mwisho  wa kufunga historia ya ulimwengu na baada tu  ya utawala huu  Yesu anakuja katika Mawingu ya Mbinguni;

🛑PEMBE NDOGO NINANI? JIFUNZE YAFUATAYO

♨️♨️MAMBO SITA YANAYOHUSU PAPA AU PEMBE NDOGO♨️♨️

✅1. PEMBE NDOGO, ATATOKEA KATIKA UFALME WA WARUMI, LAKINI ATAKUWA MBALI NAZO.
Hivyo Pembe ndogo si ufalme tu kama falme zingine kumi lakini ni NGUVU ZA KIDINI ZILIZOINUKA MIONGONI MWA SERIKARI Maneno  ya askofu wa Rumi kwanza yalionekana kama  yatoka  kwa mshauri na ndugu mkubwa Miaka ilipoendelea mbele maneno yake yalianza kupokelewa kama yatoka kwa baba.Ufalme wa  Rumi  ulipozidi kudhoofika askofu (sasa aitwaye PAPA maana yake (baba katika  kilatini akaanza  kuheshimiwa kama BWANA Mwisho yalifanywa  madai ya kiburi ya kuwa PAPA ni MUNGU  hapa duniani.

✅2, ATAPIGANA KWA NGUVU KUTIISHA FALME TATU ZILIZOPINGA NIA YAKE.
Falme tatu zilizongolewa kabisa mbele ya papa ni HERULI chini ya Odoace, VANDALi Na OSTROGOSTHS chini ya Theodoric

✅3. ATANENA MANENO MAKUU (YA KUFURU –TAZAMA UFUNUO 13:5) JUU YAKE MUNGU ALIYE JUU
Pembe ndogo itanena maneno mkuu kinyume chake aliye juu .madai yake ya kiburi na kufuru yaliyofanywa na PAPA yasemwayo hapa yametwaliwa kutoka katika FERRIS ECCLESIASTICAL DICTIONARY
Papa ni mwenye kuheshimiwa  sana  na aliyetukuzwa ,yeye si mtu tu ,bali  ni kama aliye  Mungu ,na kasisi wa Mungu PAPA huvishwa taji iliyo Na matabaka MATATU ya kuwa Ni mfalme wa Mbinguni na wa Duniani na AHERA

✅4. ATAWADHOOFISHA.MAANA YAKE ATAWATESA WATAKATIFU ALIYE JUU
Wakati wa zama za giza ,ambao ulianza  katika mwaka 538 B.K kanisa la kirumi na madhehebu yake  liliwatesa wakristo  wapatao  50,000,000 mpaka kufa .habari   hii ya kuogofya  ni historia moja  ya giza kabisa  katika historia ya mwanadamu .

✅5. ATAJARIBU KUBADIILI MAJIRA NA SHERIA YA MUNGU.
Pembe ndogo  atajaribu  kubadili nyakati na  na sheria  ya Mungu tutumie maneno machache kutoka katika ROMANI  COTHOLIC PROMTA BIBLOTHECA YALIYOANDIKWA NA FERRARIS;Papa Ni mwenye  mamlaka makuu  na uweza hata aweza kugeuza?(kubadili) kueleza au  kutafsiri sheria takatifu VOL ,UK,29 KATIKA KATEKISIMU ZA KANISA  LA KIRUMI zitumiwazo kuwafundisha wanafunzi sheria ya Mungu  imegeuzwa kidogo ,kwa sababu hiyo amri  ya pili  inayokataza kuabudu sanamu  imefutwa .Amri ya nne imefupishwa  ili  kuendeleza kushika  SIKU YA KWANZA YA JUMA (sunday)mahali pa sabato ya kweli.Amri ya kumi imegawanywa kuwa amri mbili.

✅6. ATAENDELEA KWA WAKATI NA NYAKATI MBILI NA NUSU ⁵ 13:5)
Siku moja katika unabii huwakilisha –mwaka mmoja ,EZEKIELI 4:6, Tena utakapozitimiza hizo, utalala kwa ubavu wako wa4 kuume, nawe utauchukua uovu wa nyumba ya Yuda; siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagizia (AU HESABU 14:24)
JASTINIA alitoa  amri katika mwaka 5 wa 538 B.K akimpa papa  mamlaka yasiyo na mpaka   juu ya makanisa5 yote.amri hiyo  ilitimilizwa katika5 mwaka wa 538 B.K  wakati pembe tatu  zilizopinga kanisa la Rumi  na madhehebu yake  zilipoangamizwa kwa vita.hivyo wakati wa kuanza  miaka 1260 baadaye ,PAPA ALIPOTEZA MAMLAKA YAKE  KWA MUDA KATIKA FEBRUARI 20,1798 BERTHIER JEMEDARI  WA JESHI LA UFARANSA CHINI YA NAPOLEONI alimteka Papa  na kumfunga katika Rumi,ndio ulikuwa mwisho wa kanisa  la Rumi  na madhehebu yake  kwa  muda .baada ya wakati  huo  hakukutokea  mateso ya watakatifu ULAYA  walikuwa huru kumwabudu MUNGU.

Comments