CHIMBUKO LA KUTOKUFA KWA ROHO:

CHIMBUKO LA KUTOKUFA KWA ROHO:

Unaweza ukawa Mkristo lakini ukawa una mafundisho yanayopingana na Ukristo au maagizo ya Mungu. Wakristo wengi tumejikuta tukiuunga mkono kauli ya shetani bila kujijua.

Sikia Mungu alimwambia hivi Adamu na Hawa:
Mwanzo 2:17
walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo #utakufa_hakika.

Kauli ya Mungu ni kwamba kifo cha Adamu baada ya kula tunda ni kifo cha hakika.
Lakini tunaona shetani anakuja kumpinga Mungu kwamba Mwanadamu hawezi kufa hakika.
# Mwanzo 3:4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,

Hizi kauli mbili zenye utata ndio ambazo zimejenga misingi ya imani zetu katika Dini, wapo watu wanaunga mkono kauli ya shetani kwamba mtu hafi hakika akifa Roho haifi, inaendelea kuishi Mbinguni, hili ni fundisho lilelile la shetani kwamba mtu hawezi kufa hakika, Ina maana kama Roho haifi, bila shaka kuna Uhai baada ya kifo, na ndio maana imepelekea kuwa na ibada za wafu, kuwaomba wafu na kuwatolea sadaka ili wasamehewe dhambi zao, fundisho la kuwaka kwa jehanamu, Fundisho la pargatori nk.

Kwa sababu huwezi ukamuombea mtu asamehewe dhambi ikiwa hayuko hai.

Fundisho la Biblia ni kwamba mtu akifa anakufa hakika, hajui Jambo lolote: Mhubiri 9:5
kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.

Baadhi ya watu wametumia kisa cha Lazaro na Tajiri, kudhani kwamba mtu akifa anaendelea kuishi Tena. Habari ya Lazaro na Tajiri ilikuwa ni moja ya Fundisho la Yesu kwa njia ya mfano kwa Waandishi na Mafarisayo.

Yesu alitoa mfano huu akiwa amewalenga Waandishi na Mafarisayo ambao walikuwa wameacha jukumu la kupeleka injili na wakageukia mambo ya Utajiri, na walikuwa wanaamini kwamba mtu akiwa maskini na mgonjwa Kama Lazaro, Basi kalaaniwa na wala hawezi kuurithi uzima wa Milele.

Na hivyo Yesu alikuwa anataka kuondoa fikra na Dhana potofu zilizojengeka akilini mwao. Yesu alikuwa anawapa uthibitisho kwamba kuwa Tajiri sio tiketi ya kurithi Ufalme wa Mungu, na Wala kuwa Maskini sio kwamba mtu katenda dhambi au kalaaniwa.

Lakini Yesu alikuwa anataka kuwaonesha kwamba muda wa Kufanya matengenezo ni wakati upo hai na sio baada ya kufa, na ndio maana yule Tajiri alijaribu kuomba rehema lakini ilishindikana.

Mungu akubariki

Comments