666: Hesabu Ya Jina La Papa!

666: Hesabu Ya Jina La Papa!

Ufunuo 13:17, 18 “tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake…Na hesabu ya jina lake ni mia sita, sitini na sita.”

Tumeambiwa kuwa mnyama ana jina, na hesabu ya jina lake ni 666. Hivyo kupata jina la mnyama lenye namba 666, lazima kwanza tufahamu mnyama mwenyewe ni nani.

Unabii wote katika Biblia unathibitisha kuwa mnyama ni Roma ya Vaticani & kanisa la Romani Katoliki.

*. Ufunuo 17:3 “Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.”

Katika unabii mwanamke au bibi-arusi huwakilisha kanisa.

*. Ufunuo 21:9 “…Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi (au kanisa), mke wa Mwana-Kondoo (au Yesu).” Angalia pia Ezekieli 16:2-63

Na mnyama huwakilisha ufalme au taifa.

*. Danieli 7:17 “Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne watakaotokea duniani.”

*Danieli 7:23 “…Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia.”

Hivyo, mnyama ni taifa, na mwanamke ni kanisa. Je kuna kanisa lolote hapa duniani lililoketi juu ya taifa? Je kuna taifa lolote lenye mamlaka ya kidini na kisiasa kwa wakati mmoja? Au Je kuna mamlaka yeyote inayotawala juu ya kanisa na serikali kwa wakati mmoja? Ni kanisa la Romani Katoliki pekee lenye mamlaka kama hayo. Hivyo kanisa la Romani Katoliki na Upapa kwa ujumla vinatawala juu ya mnyama Roma aliye katika unabii. Kwa ushahidi zaidi tafadhari bofya hapa.

Tumegundua kuwa mnyama mwenyewe ni Dola la Roma linalotawaliwa na kanisa la Romani Katoliki. Lakini Je Biblia inasemaje kuhusu hesabu ya jina la mnyama huyu?

Ufunuo 13:18 “Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.”

Lakini Je, ni jina gani la mnyama lenye hesabu ya 666? Tafadhari soma kwa makini jarida la kanisa la Romani Katoliki hapo chini!

“Maneno yaliyoandikwa katika kilemba cha Papa ni haya ‘VICARIUS FILII DEI’. ambayo ni ya kilatini kwa ajili ya ‘KASISI WA MWANA WA MUNGU’. Wakatoliki huchukulia kwamba kanisa ambalo ni jumuiya ya kuonekana, lazima liwe na kichwa cha kuonekana. Kristo, kabla ya kupaa kwenda mbinguni, alimteua Mt. Petro kuwa kama mwakilishi wake. . . hata hivyo Asikofu wa Roma, kama kichwa cha kanisa, alipewa jina ‘KASISI WA YESU.'” –Our Sunday Vistor, (Catholic Weekly) “Bureau of Infomation,” Hantington, Indo, April 18, 1915

Kwa hiyo kanisa la Roma lazima liwe na Papa kama kichwa cha kanisa cha kuonekana, na jina la ‘VICARIUS FILII DEI’, ni jina analobeba kichwa huyu wa kanisa. Zingatia kwamba papa anatawala juu ya mnyama Roma na alipokea kiti cha enzi kutoka kwa Kaisari wa Roma. Papa Pius IX mwenyewe alijiita kaisari katika hotuba yake wakati aliposema: “Kaisari ambaye sasa anawahutubia, na ambaye peke yake anastahili utii na heshima ya kutosha.” — (Pope Pius IX in his Discorsi (I., p. 253)).

Chanzo kimoja kikizungumzia wakati, wa mwaka 500 BK, wakati Ufalme wa Kirumi ulipopasuka vipande vipande kinasema: “Hapana, Kanisa [Katoliki] halitateremka kaburini. Litauokoa Ufalme. . . Kwa kirefu ufalme wa pili utainuka, na katika ufalme huu Papa atakuwa bwana–zaidi ya hivyo, atakuwa bwana wa Ulaya. Ataamuru maagizo yake kwa wafalme ambao watamsikiliza” —(Andrea Lagarde, The Latin Church in the Middle Ages, 1915, p. vi.).

Adolf Harnack anasema: “Vipengele vyovyote vya Kirumi ambavyo Wabarbario na Waario walivibakiza. . . [vilikuja] chini ya ulinzi wa Askofu wa Roma, ambaye alikuwa mtu mkuu huko baada ya kupotea kwa mfalme. Kanisa la Kirumi kwa njia hii kwa faragha lilijisukuma lenyewe katika nafasi ya Ufalme wa Ulimwengu wa Kirumi, ambao kwa kweli liliuendeleza.” —(Adolf Harnack, What is Christianity? (New York: Putnam, second edition, revised, 1901), pp. 269, 270)).

Alexander anasema: “Kanisa la Katoliki lenye nguvu halikuwa kidogo kuliko kuwa Ufalme wa Kirumi uliobatizwa. . . Mji mkuu wa Ufalme wa zamani wa Kirumi ulikuwa mji mkuu wa ufalme wa Kikristo. Ofisi ya pontifex Maximus iliendelea katika ile ya papa” —(Alexander Clarence Flick, The Rise of the Medieval church).

Papa alipokea mamlaka kutoka Roma ya kipagani, na akauendeleza ufalme wa Roma akiwa katika mji mkuu uleule wa Roma. Hiyo ndiyo sababu Unabii unasema Upapa ni “mwanamke aliyeketi juu ya mnyama”; ni kanisa lililokaa juu na linatawala juu ya mnyama ambaye ni ufalme wa Roma. Jina la Vicurias Filii Dei ambalo linamfanya papa kuwa kichwa cha ufalme wote na kanisa (Ufu. 13:3,4), kama gazeti la Katoliki hapo juu lilivyothibitisha, jina hilo liliandikwa kwa maandishi ya dhahabu katika kilemba cha papa. Hii ni kweli kwa kuwa mfumo wa Upapa umechanganya imani zote za kipagani, kibabeli, kigiriki, kikristo, kiyahudi, n.k. kwa pamoja (Ufu. 13:1,2). Wayahudi katika mfumo wao wa kikuhani, waliandika maneno “UTAKATIFU KWA BWANA” katika kilemba cha kuhani mkuu.

Kutoka 39:30,31 (KJV) “Nao wakafanya hilo bamba la hiyo taji takatifu la dhahabu safi, na kuandika juu yake andiko, mfano wa kuchorwa kwa muhuri, UTAKATIFU KWA BWANA. 31 Nao wakatia ukanda wa rangi ya samawi ili kulifunga katika hicho kilemba upande wa juu; vile vile kama Bwana alivyomwagiza Musa.”

Kama Upapa ulivyochanganya mambo ya dini mbalimbali katika mfumo wao, ulichanganya pia kilemba hiki pamoja na maandishi VICARIUS FILII DEI ambayo ni sawa na 666 kama tunavyoenda kuona.

Herufi za kilatini pia hutumika kama namba kwa mfano herufi “V” hutumika kama “5” au herufi “C” hutumika kama “100.” Pia (U) inaweza kutumika kama (V) kwa Kilatini. Herufi hizi siku hizi huitwa “Namba za Kirumi.”

“VICARIVS FILII DEI”

(Kasisi wa Mwana wa Mungu)

V5I1C100A0R0I1V5S0F0I1L50I1I1D500E0I1Jumla666VICARIVS=112FILII=53DEI=501Jumla=666

Vicurius – inamaanisha kuweka badala ya, au katika mahali pa.
Filii – Mwana
Dei – Mungu

Wakatoliki wengi watakataa kwamba jina Vicarius Filii Dei kamwe halijawahi kutumika katika mfumo wa kanisa lao, wengi wanashikilia kwamba papa ni kasisi wa Yesu Kristo, lakini sio na hajawahi kuitwa jina kama hilo la Kasisi wa Mwana wa Mungu. Hili ni wazo lisilo sahihi, mapapa kiukweli hulitumia kabisa jina la Vicarius Filii Dei, na ufuatao ni ushahidi asilimia mia kutoka katika machapisho na vitabu vya kanisa Katoliki lenyewe.

“Nguvu ya muda katika mikono ya Mtakatifu Gregory I ilikuwa ni utawala wa kibaba na wa kizee juu ya mataifa ambao haujawahi kupunguzwa kwa utaratibu wa kiraia. Katika mikono ya Mtakatifu Leo III ikawa nguvu ya kujenga falme. Katika mikono ya Mtakatifu Gregory VII ilikuwa ni janga la kuyaadhibu. Katika mikono ya Alexander III ilikuwa ni nasaba, kutawala kwa nguvu zaidi, kwa jina la Mungu, juu ya mamlaka za ulimwengu. . . Kwa hiyo naweza kusema kamwe hapakuwa na wakati ambao uwezo wa muda wa Kasisi wa Mwana wa Mungu, ingawa ulipigwa kama tunavyouona, ulikuwa imara na wenye mizizi katika umoja wote wa Kanisa Katoliki.
“Ilikuwa ni utii wa heshima kusujududu kwa Kasisi wa Mwana wa Mungu, na kusuluhisha usuluhisho wa malalamiko yao kwa mtu ambaye wote wangekubali kutii.” —(The Temporal Power of the Vicar of Jesus Christ, pp. 231-232 na Henry Edward Kadinali Manning, toleo la pili, London: Burns and Lambert, 1862).

“Swali. Je ni maneno gani yanayochukuliwa kuwa katika taji ya Papa, na yanaashiria nini kama kuna chochote?
Jibu. Maneno yaliyoandikwa katika kilemba cha Papa ni haya Vicarius Filii Dei. ambayo ni ya kilatini kwa ajili ya‘KASISI WA MWANA WA MUNGU’. Wakatoliki huchukulia kwamba kanisa ambalo ni jumuiya ya kuonekana, lazima liwe na kichwa cha kuonekana. Kristo, kabla ya kupaa kwenda mbinguni, alimteua Mtk. Petro kuwa kama mwakilishi wake. Juu ya kifo cha Petro mtu ambaye alifuata kwenye Ofisi ya Petro alitambuliwa kama kichwa cha kanisa. Hata hivyo Asikofu wa Roma, kama kichwa cha kanisa, alipewa jina ‘KASISI WA YESU.’
“Maadui wa Upapa hukanusha jina hili kama dhana mbaya lakini Biblia inatuambia kwamba Kristo hakuwapa Kanisa lake mamlaka ya kufundisha tu, bali pia mamlaka ya kutawala. Kudai kuwa na mamlaka ya kutawala katika ufalme wa Kristo wa kiroho, katika nafasi ya Kristo , sio madhara zaidi kuliko kudai kuwa na mamlaka ya kufundisha kwa jina la Kristo. Na swala hili kila mtumishi wa Kikristo analifanya.” —(Our Sunday Visitor, (Gazeti la Katoliki la kila wiki), April 18, 1915, swali la 30 chini ya ‘Bureau of Information’, p. 3)).Angalia kopi ya dokomenti hii hapa.

Dokomenti nyingine inatoka kwenye gazeti la katoliki la OUR SUNDAY VISITOR, toleo la Novemba 15, 1914, ambalo linakiri wazi kwamba jina la  Vicarius Filii Dei lipo kwenye kilemba cha papa na lina hesabu ya 666, linasomeka hivi:  “Jina la Papa katika Roma ni Vicarius Filii Dei. Jina hili limeandikwa kwenye kilemba chake[*]; na kama ukizichukua herufi za jina lake ambazo zinawakisha namba za Kilatini na kuzijumlisha kwa pamoja zinaleta 666.” —(Our Sunday Visitor, (Gazeti la Katoliki la kila wiki), November 15, 1914, chini ya ‘Bureau of Information’, p. 3)). Angalia kopi ya dokomenti hii hapa.

Angalia Dokomenti za kilatini zifuatazo kutoka kanisa katoliki, ambazo kwa wazi zinatumia jina Vicarius Filii Dei . . .

“Ut sicut Beatus Petrus in terris vicarius Filii Dei fuit constitutus, ita et Pontifices eius successores in terris principatus potestatem amplius, quam terrenae imperialis nostrae seremitatis mansuetudo habere videtur.” —(Prompta Bibliotheca Canonica, Juridica, Moralis, Theologica, Ascetica, Polemica, Rubristica, Historica, by Lucius Ferraris, Volume V, makala ya “Papa, Article II”, yenye kichwa “Concerning the extent of Papal dignity, authority, or dominion and infallibility”, point #20, column 1828, ilichapishwa katika Petit-Montrouge (Paris) na J. P. Migne, toleo la 1858)). 

Ikitafsiriwa kwa kiswahili dokomenti hii inasomeka: “Kama vile Petro mbarikiwa alifanyika Kasisi wa Mwana wa Mungu duniani, kwa hiyo inaonekana kwamba maaskofu wakuu, waandamizi wake, wanashikilia kutoka kwetu na ufalme wetu nguvu ya ukuu duniani ya juu kuliko uzuri wa utulivu wetu wa kifalme duniani.”

“Beatus Petrus in terris Vicarius filii Dei videtur esse constitutus.” —(Decretum Gratiani, prima pars, dist. xcvi, col. 472, (kwanza ilichapishwa katika Bologna mwaka 1148, na ikachapwa tena mwaka 1555)). Dokomenti hii ilitafsiriwa katika kiingereza na Christopher B. Coleman, Ph. D., katika kitabu kinachoitwa “The Treatise of Lorenzo Vallo on the Donation of Constantine,” p. 13. New Haven: Yale University Press, 1922. Ikitafsiriwa katika kiswahili inasomeka: “Petro mbarikiwa anaonekana kuwa amefanyika kasisi wa mwana wa Mungu duniani.”

Nukuu mbili za kilatini zifuatazo zote zina maana ileile kama ya moja hapo juu, na zote zinatumia jina la Vicarius Filii Dei

“Beatus Petrus in terris vicarius Filii Dei esse videtur constitutus.” —(Corpus Juris Canonici, Gregorii XIII, Pontif. Max., Auctoritate, Distinctio 96, Column 286, Canon Constantinus 14, Magdeburg, 1747.
Jina alilopewa Papa ni “Vicarius Filii Dei.” Sacrosancta concilia ad regitionem exacta, na Philippe Labbe, SJ., Vol. I, p 1534: Paris, 1671).

“Beatus Petrus in terris Vicarius filii Dei esse videtur constitutus.” —(Corpus Juris Canonici Emendatum et Notis Illustratum Gregorii XIII. Pont. Max., Lvgdvn., MDCXXII, col. 295).

Bonyeza hapa kuangalia dokomenti nyingine nyingi za RCC zinazothibitisha jina la Vicarius Filii Dei.

Inafurahisha kwamba sio jina la Vicarius Filii Dei tu katika mfumo wa Upapa ambalo ni 666, kuna majina mengi kama tunavyoona hapa. Papa Yohana Paulo II ni papa ambaye jina lake kwa lugha ya kilatini moja kwa moja ni 666, angalia jedwali lifuatalo.

“IOANES PAVLVS SECVNDO”(Yohane Paulo II)I–1O–0A–0N–0E–0S–0P–0A–0V–5L–50V–5S–0S–0E–0C–100V–5N–0D–500O–0Jumla– 666IOANES(Yohane)=1PAVLVS(Paulo)=60SECVNDO(II)=605(Jumla)160605=666


Comments