WAKOLOSAI SURA 2:16
Mara nyingi nimekuwa nikiona watu wengi wakitumia fungu hili la Wakolosai 2:16, pasipo kujua maana yake halisi ni ipi?
Na hiki ndicho Petro anaonya juu ya nyaraka za Paulo:
2 #Petro 3:15-17
Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa;
vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe.
Niseme tu kwamba nyaraka za Paulo zimepotoshwa sana na baadhi ya viongozi wa Dini, kwa kuwakaririsha waumini wao upotofu.
Sasa Aya yenyewe inasema:
#Wakolosai 2:16-18
Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;
mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.
Sasa watu wengi hupenda kunukuu hilo fungu, kama nyundo kwa dhehebu la SDA, katika kipengere cha Chakula na Sabato tu, mengine wana yaacha.
Hebu leo tugeuze kibao kidogo.
1. Je, mlevi anayetumia bia, akitumia fungu hili kwamba Usimuhukumu juu ya vinywaji, je atakuwa amekosea?
2. Je, Muislamu naye akikwambia usimuhukumu juu ya sikukuu ya mwandamo wa mwezi, kwa kutumia aya hiyo atakuwa amekosea?
3. Je, wanaokula binadamu wenzao, nyoka, mbwa nk. Wakitumia aya hii kwamba usiwahukumu, juu ya chakula, je watakuwa wamekosea?
Kwa hiyo kabla hujajenga hoja juu ya sabato, na ulaji wa nguruwe, fikiriay kwanza endapo mlevi naye akakomaa na hilo fungu kwamba usimuhukumu juu ya vinywaji.
Hebu turudi kwenye pointi, Paulo wakati anaandika waraka huu kwa Wakolosai, tayari kulikuwa na walimu wa uwongo, walioingiza mafundisho potofu katika kanisa la Kolosai,
Sasa ili uielewe maana halisi ya Wakolosai 2:16, ni vizuri kuanzia #aya ya 14: inasema:
#Wakolosai 2:14-15
akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;
akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.
Paulo anasema Yesu aliifuta #HATI iliyokuwa inatushitaki kwa #hukumu zake.
Kipindi cha Musa, kulikuwa na sheria za aina Mbili.
#AMRI kumi za Mungu, Amri 10, ziliandikwa na Mungu mwenywe kwa kidole chake katika mbao mbili za Mawe.
#Kumbukumbu la Torati 4:13
Akawahubiri agano lake, alilowaamuru kulitenda, yaani, zile amri kumi; akaziandika juu ya mbao mbili za mawe.
#Kutoka 31:18 Hapo Bwana alipokuwa amekwisha zungumza na Musa katika mlima wa Sinai, akampa hizo mbao mbili za ushuhuda, mbao mbili za mawe, zilizoandikwa kwa chanda cha Mungu.
2) #SHERIA ZA MUSA, sheria hizi za Musa ziliandikwa na Musa yeye mwenyewe katika chuo,
#Kumbukumbu la Torati 31:9
Musa akaiandika torati hii, akawapa makuhani, wana wa Lawi, waliolichukua sanduku la agano la Bwana, na wazee wote wa Israeli.
Sasa katika torati ya Musa ndiko zilikoandikwa #Hukumu, na mambo yote yaliyokuwa ni Kivuli, kama jino kwa jino, Taraka, Tohara,Kupiga mawe wavunja sabato na wazinzi, Utaratibu wa ibada za kafara NK.
#Mfano wa hukumu ni
#Ø Katika Amri kumi za Mungu kuna amri, inasema #USIZINI inaishia hivyo tu, lakini ukienda kwenye torati ya Musa inasema, Mtu akikutwa anazini apigwe mawe hadi kufa. Kumbukumbu 22:22. Sasa kifo cha Yesu hakikuondoa Amri inayosema #USIZINI, bali kilichoondolewa ni hukumu ya kupiga mawe wazinzi.
#Ø Katika Amri kumi kuna amri: inasema #USIUE, inaishia hapo tu, lakini katika torati ya Musa inasema Mtu atakayeuwa naye Auawe, Kutoka 21:12, sasa kifo cha Yesu hakikuondoa amri ya USIUE, bali kilichoishia msalabani ni hukumu ya kuua muuaji.
#Ø Amri ya Mungu inasema Ikumbuke siku ya sabato uitakase, lakini Torati ya Musa inasema Mtu akivunja sabato lazima Auawe, sasa kifo cha Yesu hakikuondoa Amri ya kuitunza sabato, bali kilichoondolewa ni ile hukumu ya kupiga mawe mvunja sabato. Kutoka 35:1-3
#Ø Amri ya Mungu inasema USILITAJE BURE JINA LA BWANA MUNGU WAKO, lakini torati ya Musa inasema mtu akitaja jina la Mungu bure ni lazima Auwawe, sasa kifo cha Yesu hakikuondoa Amri inayosema USILITAJE JINA LA MUNGU BURE, bali kilichoishia msalabani ni Hukumu ya kifo kwa anaye litaja jina la Mungu bure/ kukufuru.
Na Paulo anabainisha kwamba kifo cha Yesu kiliondoa Hukumu na sio Amri.

Na ndio maana sasa hivi hata ukimkuta mtu anazini au anavunja sabato, hawezi akapigwa mawe kwa sababu ile hukumu ya kupiga mawe Yesu aliigongomelea msalabani.
#Warumi 8:1-2
Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
Torati ya Musa ndio ilikuwa inatoa Hukumu zote.
#Matendo ya Mitume 13:39
na kwa yeye kila amwaminiye huhesabiwa haki katika mambo yale yote asiyoweza kuhesabiwa haki kwa torati ya Musa.
Hivyo kilicho gongomelewa ni ile #HATI iliyoandikwa na Musa, ambamo mlikuwa na hukumu za kila aina.
Sasa kabla ya kujua Paulo alikuwa anamaanisha nini katika #Wakolosai 2:16, inabidi kutafakari kwanza aya ya 17,
#Wakolosai 2:17-18

Kwa hiyo inabidi ujiulize ni mambo gani hayo yalikuwa ni kivuli, yakilenga mwili wa Kristo? Tumeshaona pia zile Hukumu ndio zilikuwa zikilenga Kifo cha Yesu msalabani.
Wakati Yesu alipokufa pale msalabani Pazia la Hekalu lilipasuka vipande viwili, hii iliashiria kwamba huduma zote zilizokuwa zikifanyika Hekaluni zilikuwa kivuli, zikielekeza kifo cha Yesu,
#Mathayo 27:50-52
Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake.
Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi
.
Na Paulo anathibitisha kwamba huduma za patakatifu/ Hekalu zilikuwa ni kivuli.
#Waebrania 8:5 watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.
Sasa mambo yote ambayo Paulo ameyaorodhesha katika #Wakolosai 2:16 yalikuwa yakifanyika Hekaluni, ikiwa na maana zaidi kwamba yalikuwa yakiambatana na utoaji wa kafara zilizofanyika Patakatifu/ Hekaluni. Na kafara zote zilikuwa zinamlenga Yesu.
#VYAKULA.
· Kulikuwa na mikate ya wonyesho, iliyokuwa inaliwa na Makuhani. Mambo ya walawi 24:5-9
· Malimbuko yote kilikuwa chakula cha makuhani. Kumbu 18:1-5
2. #VINYWAJI;
· Kulikuwa na malimbuko ya vinywaji, yaliyoambatana na utoaji wa kafara
Kutoka 22:29-30
Usikawie kuleta malimbuko ya matunda yako na ya vinywaji vyako.
Na Divai iliyokuwa inatolewa malimbuko, ilikuwa ni Kinywaji cha Makuhani, Kumbu 18:4
3. #SIKUKUU.
· Kulikuwa na sikukuu nyingi zilizoambatana na utoaji wa kafara ndani ya Patakatifu/ Hekalu.; kama sikuu ya Mavuno, sikukuu ya upatanisho, sikuu ya malimbuko NK. Soma Mambo ya walawi sura ya 23. Sherehe zote ziliambatana na utoaji wa kafara, ambazo ni kivuli cha Yesu.
4. #MWANDAMO WA MWEZI:
· Kila mwezi ulipoandama kulikuwa na sikukuu, pia iliambatana na utoaji wa kafara. Hesabu 28:11, 10:10, Zaburi 81:3
Zaburi 81:3
Pigeni panda mwandamo wa mwezi, Wakati wa mbalamwezi, sikukuu yetu.
5. #SABATO:
· Sasa hapa naomba tuwe makini kwa sababu, ndipo penye changamoto kubwa.
Agano la kale kulikuwa na Sabato zaidi ya moja
· SABATO YA SIKU YA SABA./ Sabato kabla ya dhambi.
#NB: sabato ya siku ya saba, ilikuwepo kabla ya dhambi kuingia Duniani, na hivyo laiti Adamu na Hawa hawangetenda dhambi, Sabato ingeendelea tu kuwepo kwa sababu ni kumbukumbu ya Uumbaji wa Mungu
#Kutoka 20:11
Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
Na hivyo kifo cha Yesu kilikuwa ni kwa ajili ya dhambi, na sabato ya siku ya saba ilikuwepo kabla ya dhambi, na hivyo sabato haikuwa na kosa lolote kama, ilivyo katika
Ndoa, kwa sababu ukiondoa sabato unatangaza kwamba Dunia haijaumbwa na Mungu, bali imeibuka.
SABATO BAADA YA DHAMBI:
Kwa hiyo baada ya dhambi kuingia zikatokea sabato nyingine, zilizokuwa zinaambatana na utoaji wa kafara.
· Sabato ya Nchi, sabato hii ilikuwa inaadhimishwa, kwa kulima shamba miaka 6, na unapofika mwaka wa saba, nchi ilikuwa inasherekea sabato.
#Mambo ya Walawi 25:2-5
Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapoingia katika nchi niwapayo, ndipo hiyo nchi itashika Sabato kwa ajili ya Bwana.
Panda shamba lako miaka sita, na miaka sita lipelee shamba lako la mizabibu, na kuyachuma matunda yake;
lakini katika mwaka wa saba itakuwa ni Sabato ya kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi, ni Sabato kwa Bwana; usipande shamba lako, wala usipelee shamba lako la mizabibu.
Sabato hii iliambatana na utoaji wa kafara, ambapo kafara zilikuwa ni kivuli, au kielelezo cha Yesu.
· SABATO YA KILA SIKUKUU
Sikukuu zote walizokuwa wanasherekea wana wa Israeli, zilikuwa ni SABATO, yaani hiyo sherehe haijalishi imeangukia jumatatu, jumanne au siku yoyote, basi siku hiyo ilikuwa inaitwa sabato
#Mambo ya Walawi 23:26-33
Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,
Lakini siku ya kumi ya mwezi huo wa saba ni siku ya upatanisho; itakuwa kusanyiko takatifu kwenu, nanyi mtazitesa nafsi zenu; nanyi mtasongeza sadaka kwa Bwana kwa njia ya moto……Itakuwa kwenu #sabato ya kustarehe kabisa, nanyi mtazitesa nafsi zenu; siku ya kenda ya mwezi wakati wa jioni, tangu jioni hata jioni, mtaishika hiyo Sabato yenu.
Kwa hiyo kila mwaka tarehe 10 mwezi wa 7, ilikuwa ni sabato haijalishi ni juma ngapi, bora mradi iwe tarehe 10/7
· SABATO YA KUSAMEHE MADENI
Wapo watu walikuwa wanakopa lakini hawana uwezo wa kulipa madeni, hivyo ndani ya miaka 6, ndio mtu aliruhusiwa kudai madeni, lakini ukifika mwaka wa saba, ulikuwa ni SABATO, kwa wadeni kusamehewa madeni yao. #Kumbu 15:1-11
· SABATO YA KUACHILIA WATUMWA
Watumwa wote walikuwa wanafanya kazi kwa miaka 6, ukifika mwaka wa saba, ilikuwa ni Sabato kwa watumwa kuachwa huru bila kutumikishwa. #Kutoka 21 :1-3
Sasa baada ya Yesu kuja baadhi ya watu hawakumwamini na hata hawakujua uthamani wa kifo chake pale msalabani bali walikuwa wanaendeleza zile kawaida za agano la kale ambazo zilikuwa ni kivuli. Na watu hawa wakafika hadi Kolosai, na wakaanza kuwafundisha watu kwamba
Ni lazima, Kupiga mawe wazinzi,
Ni lazima Kupiga mawe wavunja sabato,
Ni lazima kuadhimisha mwandamo wa mwezi.
N lazima watu washerekee sikuu za upatanisho, Malimbuko NK
Ni lazima watu waendelee kutoa sadaka za vinywaji
Ni lazima kuadhimisha sabato za nchi NK,
Na ndipo sasa Paulo anapata habari juu ya hawa waalimu wa uwongo, na sasa Paulo anawaandikia Wakolosai kwamba #wasihukumiwe juu ya Mambo hayo maana yalikuwa ni Kivuli tu, bali yalikamilishwa kupita mwili wa Kristo pale msalabani.
#Waebrania 9:10
kwa kuwa ni sheria za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kutawadha kwingine kwingine, zilizoamriwa hata wakati wa matengenezo mapya.
Kwa hiyo ndugu zangu Paulo alipokuwa anasema mtu asiwahukumu juu ya #Sabato na #Vyakula, hakumaanisha kualalisha ulaji wa vitu najisi kama nguruwe, na wala aliposema mtu asiwahukumu juu ya Sabato hakumaanisha Sabato ile ya siku ya saba hapana, bali alikuwa anazungumzia sabato za nchi, sabato za sikuu NK. Maana sabato hizi ndo ziliambatana na utoaji wa kafara, ambapo kafara hizo zilikuwa ni kivuli cha Yesu ambaye ndiye kafara kuu.
Sabato ni moja ya Amri kumi za Mungu, na hivyo ikiwa sabato iliishia msalabani, basi ilibidi amri zote kumi ziishie msalabani, Huwezi ukasema,
1. Kuwa na miungu ni Dhambi
2. Kuchonga sanamu ni Dhambi
3. Kutaja bure jina la Mungu ni Dhambi
4. Kuvunja Sabato SIO Dhambi
5. Kuto waheshimu wazazi ni Dhambi
6. Kuua ni Dhambi
7. Kuzini ni Dhambi.
8. Kuiba ni Dhambi
9. Kusema uwongo ni Dhambi
10. Kutamani ni Dhambi
Jamani hebu ifike wakati tujiongeze sio kila kitu cha kushabikia wewe unadanganywa kwamba sabato walipewa Wayahudi. Je hizo amri nyingine 9, mbona walipewa hao hao Wayahudi, lakini mbona unazitunza.?
Unadanganywa kwamba Ukimpoke Yesu tayari hakuna haja ya kutunza sabato, kwa sababu Biblia inasema:
#Marko 2:28 Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia.
Jamani aya hii haisemi Mwana wa Adamu ndiye Sabato. Hapana
Kuna kiunganishi “WA” kinachoonesha Yesu ndiye mmiliki au mwasisi wa Sabato, Ikiwa na maana kwamba kwa sababu yeye Yesu ni Mungu ndiye aliyeiweka sabato na niya kwake.
Mfano: nikisema Mimi Isaka ndiye bwana “wa” hili shamba. Je kwa kauli hiyo inanifanya mimi Isaka Kuwa nyumba? Jibu ni Hapana, Bali kama una hitaji shamba mimi ndiye ninaye jua taratibu na mipaka yote ya Shamba kwa sababu ninalimiliki.
Kwa hiyo ndivyo ilivyo kauli ya Yesu, Anaposema Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato,Ana maana kwamba yeye ndiye anayejua usahihi wa sabato kwa sababu ni yake.
Na aya nyingine ni hii: #Mathayo 11:28
Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
Wito wa Yesu hapa sio watu waache kupumzika siku ya sabato hapana, bali wanaoitwa hapa kupumzishwa ni wale wenye mizigo ya Dhambi, Nguvu za Giza, Magonjwa NK. ndio wanaoitwa wapumzishwe, Hiki ndicho kilichomleta Yesu Duniani,
soma #Luka 4:18
Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,
Hivyo kupumzika siku ya sabato ni Matokeo ya kukombolewa, kutoka katika utumwa wa Dhambi.
Mungu akubariki
0627729770
0689980058

Mtumishi ubarikiwe Sana kwa ujumbe
ReplyDelete