SUMU YA KIROHO ILIYOPAKWA SUKARI



kwa  Nje      Wengi  wanashawishika kufikiri kwamba wao wako katika njia ile iendayo mbinguni ati  kwa sababu tu wanakiri kumwamini Kristo, wakati wanaikataa Sheria ya Mungu [Amri Kumi].

Lakini hao watagundua mwishoni kwamba walikuwa katika njia ile iendayo kwenye uharibifu badala ya ile iendayo mbinguni.  Sumu ya kiroho inapakwa sukari kwa nje kwa njia  ya fundisho [potofu] la utakaso, na kuwapa watu waimeze.  Maelfu kwa hamu kubwa huimeza, wakijisikia ya kwamba ikiwa wao ni waaminifu tu katika imani yao hiyo, basi, watakuwa salama.

Lakini uaminifu huo hautaweza kamwe kuligeuza kosa [fundisho potofu] kuwa kweli. 

Mtu anaweza kumeza sumu, akidhani kwamba ni chakula;  lakini uaminifu wake [katika kuamini hivyo] hautaweza kumwokoa kutokana na madhara ya sumu hiyo aliyoimeza.
     Mungu  ametupa sisi Neno lake kuwa kiongozi wetu.  Kristo amesema,  "Mwayachunguza [Chunguzeni] Maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake;  na hayo ndiyo yanayonishuhudia" (Yohana 5:39, KJV).  Aliwaombea wanafunzi wake, akisema,  "Uwatakase kwa ile kweli;  neno lako ndiyo kweli"  (Yohana 17:17).  Paulo asema hivi,  "Kweli, mimi mwenyewe naliona ndani ya nafsi yangu kwamba yanipasa kutenda mambo mengi yaliyopingamana na jina lake Yesu Mnazareti" (Matendo ya Mitume 26:9).  Lakini imani hiyo haikuifanya njia yake iwe ya kweli.
       👇
Paulo alipoipokea injili ya  Yesu Kristo, ilimfanya kiumbe kipya.  Alibadilika kabisa;  kweli iliyopandwa moyoni mwake ilimpatia imani ile na ujasiri ule aliokuwa nao kama mfuasi wake Kristo hata upinzani wo wote ule haukuweza kumtikisa, wala mateso kumtia hofu.    
   👇👇
Watu wanaweza  kutoa udhuru wo wote wanaotaka kama sababu ya kuikataa Sheria ya Mungu [Amri Kumi];  lakini hakuna udhuru wo wote utakaokubaliwa katika siku ile ya hukumu [ambayo inaendelea hivi sasa huko mbinguni].

👉 Wale wanaoshindana na Mungu na kuzitia nguvu nafsi zao zenye hatia kwa kuendelea kuivunja Sheria ya Mungu [Amri Kumi], hivi punde watalazimika kukabiliana na Mtoa-Sheria Mkuu juu ya Sheria yake iliyovunjwa [Amri Kumi].      Siku  ya kisasi cha Mungu yaja  ----  siku ile ya ghadhabu yake kali sana.  Ni nani atakayesimama [atakayestahimili] siku ile ya kuja kwake?  Wanadamu wameifanya mioyo yao kuwa migumu kwa kumpinga Roho wa Mungu, lakini mishale ya ghadhabu yake itapenya mpaka ndani ya mioyo yao mahali pale iliposhindwa kupenya mishale ile ya kuwathibitishia  dhambi zao. 

👉Si mbali kuanzia sasa Mungu ataondoka kuja kumshughulikia mwenye dhambi [yule asiyetaka kutubu].  Je!  yule mchungaji wake wa uongo atamkinga mvunja sheria [Amri Kumi] huyo siku ile?

Je. !  anaweza kusamehewa yule aliyeandamana na mkutano katika  njia ile ya uasi?  [ _Kutoka_ 23:2].  Je!  kule kupendwa [Je!  anaweza kusamehewa yule aliyeandamana na mkutano katika  njia ile ya uasi?  [Kutoka 23:2].  Je!  kule kupendwa [kwa fundisho hilo potofu] na watu wengi au idadi kubwa [ya waumini] kutaweza kumfanya mtu ye yote asiwe na hatia?  Haya ndiyo maswali ambayo wale walio wavivu na wasiojali [kusoma Neno la Mungu kujua  linavyosema juu ya Sheria yake] wanapaswa kuyatafakari na kukata shauri wao wenyewe juu ya kile watakachofanya. SURA  YA  3 Kristo  Ni  Haki  Yetu fundisho hilo potofu] na watu wengi au idadi kubwa [ya waumini] kutaweza kumfanya mtu ye yote asiwe na hatia?  Haya ndiyo maswali ambayo wale walio wavivu na wasiojali [kusoma Neno la Mungu kujua  linavyosema juu ya Sheria yake] wanapaswa kuyatafakari na kukata shauri wao wenyewe juu ya kile watakachofanya. SURA  YA  3 Kristo  Ni  Haki  Yetu.
*
Usikose kutazama video hii you tube

Mapigo saba baada ya Sheria ya Jumapili kupitishwa
*       👇
*https://youtu.be/YNypV-79ik8*

MUNGU AKUBARIKI

Isack Mussa

_Kwa Mawasiliano_
*0627729770*
*0712336509*

Comments