: Kwa neema ya MUNGU soma ujumbe huu wote
Siku moja Nchini Tanzania, kuna jambo lililonishangaza sana likanifanya kutafakari kwa kina kuhusu Safari ya Wokovu wangu.
TANGAZO lilisika linalosema hivi
"ifikapo tarehe fulani ni Marufuku kutumia Mifuko ya Plastic "
Siku ilipofika kwakweli hakuna hata Mmoja mwenye upungufu wa akili aliyevunja hiyo Amri
SWALI kubwa tunalopaswa kujiuliza ni hili
Sisi Wanadamu JE hivi ndivyo tunavyotii sheria za Mungu?? Sheria iliyo ya Milele?? Kwasababu yeye ndiye aliyetupatia Uhai tulionao
Kadhalika ndivyo ipo Mbiu inalia ikitusihi tuache Maovu , Maana hukumu ya Ulimwengu ipo karibu inakuja. JE ni nani atasimama??
Wapendwa Siku ya KIAMA ni ya kutisha Mno Maana itakuwa ni Ghadhabu ya Mvinyo bila Maji.
Wale pekee ambao wenye kusikia wito leo hivi ndio ambao Watasimama.
Ninapo Jihoji, JE Mwanadamu huyu Mwenye asili ya kuasi, je aliwezaje kutunza Agizo??
Ndipo napata kugundua siri hii iliyo jificha, ngoja nikueleze hiyo siri
Mwaka Fulani, Serikali ilitangaza tarehe ya Mwisho wa Ulimwengu. Watu wote walikesha kwa Maombi na kwa Makini.
Ole wetu sisi Wanadamu kwa Maana hatujui Saa ya kuja kwa Mwana wa Adamu hatutambui kuwa ni Mchana au Usiku.
Yesu angetangaza tarehe ya kuja, kumbe watu wengi wao wangemtii kwa hofu kwa kuogopa kifo.
Mungu anataka tumtii kwa Moyo wa Kumpenda na sio kwa Kushurutishwa.
Mimi nampenda kwa hiari yangu, Maana yeye alinipenda kwanza na kunifia pale Msalabani
hivyo ni Wajibu wetu kutii sheria zake.
SOMA MPAKA MWISHO
Tushike Amri za Mungu ambazo zipo katika Biblia kama zilivyoandikwa
Kutoka 20:1-17
1 Yohana 2:3
[3]Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake.
Wanaomjua Mungu ni hawa 👇👇
Biblia.
1 Yohana 2:3-4,7
[3]Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake.
[4]Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake.
[7]Wapenzi, siwaandikii amri mpya, ila amri ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo. Na hiyo amri ya zamani ni neno lile mlilolisikia.
Wanaompenda Mungu sifa kuu hii hapa
👇👇
1 Yohana 5:3
[3]Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.
Wanaomjua Mungu ni hawa hapa 👇👇
Biblia. 1 Yohana 3:24
[24]Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye naye ndani yake. Na katika hili tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa huyo Roho aliyetupa.
Kwanini Watu wengine hawatii Amri zote
Ufunuo wa Yohana 12:17
[17]Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.
Tumaini la Pekee kwa wanaotunza Amri za Mungu
Ufunuo wa Yohana 14:12
[12]Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.
Mungu akubariki unapokwenda kufanya Maamuzi ya kumtii katika Roho na Kweli
Usikose kutazama ujumbe huu
Toba ya Kweli
https://youtu.be/__d3Vdcy58Y
068988058
0627729770
Comments
Post a Comment